Kwanini vijiji vingi vya usukumani havina wezi kama kwingineko?

1. Pesa/mali kila mtu anayo ya kutosha siyo kama zile sehemu za wazee wa sokoni 7days/week.
2. Hawana tamaa za hovyo hovyo juu ya mali ya mtu
3. Maadili mema ni jadi yao
Kuhusu maadili siyo kweli ni sungusungu na UCHAWI vijana wengi wanaogopa kuiba kwani watageuzwa misukule (Mutunga) labda watoto WA kike ndo wenye maadili lakini midume hovyoooo
 
Kuhusu maadili siyo kweli ni sungusungu na UCHAWI vijana wengi wanaogopa kuiba kwani watageuzwa misukule (Mutunga) labda watoto WA kike ndo wenye maadili lakini midume hovyoooo
Kama kinachoogopwa ni uchawi japo si kwa kila mtu, kwa nini Sumbawanga na Kigoma kwa wachawi na waganga wa kila aina kuna wizi? Zanzibar na Pwani kote kwa watu wenye ulinzi shirikishi wa majini na maruhani kuna wizi hadi wa yebo katika nyumba za ibada, kwenyewe wazi hawagopi?
 
Nimekaa vijiji kadhaa, na kupita katika harakati zangu nimeona tofauti kubwa.

Usukumani ndani kabisa vijijini hakuna wiziwizi wa ajabu.

Huwezi kusikia wizi wa mifugo.
Watu wanaweka magunia ya mipunga bila ulinzi wa kutisha na unayakuta.

Cha ajabu hata vijiji vya wasukuma waliohamia Sumbawanga na Morogoro hivyohivyo.

Unatembea usiku hakuna mtu mwenye hamu ya kukukaba. Ukisahau pembejeo shambani unazikuta.

Jamaa wengi sio wezi, babda utokee ukame na kuwe na baa la njaa. Ila kwingineko huko tunakopitapita jamaa ni wepesi sana, tena ukiwa mgeni lazima uonewe.

Nini chanzo cha hii kitu
Mwizi akikutwa hawacheleweshi. So watu wanajua hao jamaa hawana kukupeleka polisi ni moto halafu wanasema umewatoroka.
 
Kuhusu maadili siyo kweli ni sungusungu na UCHAWI vijana wengi wanaogopa kuiba kwani watageuzwa misukule (Mutunga) labda watoto WA kike ndo wenye maadili lakini midume hovyoooo
Mtu unaamka saa tisa usiku na sheli yako unalima mpaka saa tatu hapo unatoka shamba ng,ombe wakapumzike na wapate malisho ww unarudi shamba kurendelea kusaidia wapandaji mda unao kuja kupata kupumzika ni usiku na tena ni masaa machache huo mda wa kuwaza ukaibe cha mtu unaupata wapi.Hata tukisha vuna ndo mda mzuri wa kutembelea ndugu na jamaaa na kwenda kuuza mazao mwaka mzima unakuta tuko bize.Sasa huku pwani mtu anaamka hana kazi ya kufanya akiona hata chuma chakavu tu kwa jirani limekaa kihasara anapita nalo akauze screpa.Wazee wetu nawapongeza sana kutupa akili ya kupenda kufuga na kilimo ndo maana mikoa yote lazima ukutane na wasukuma na lazima utawakuta wanapambna sana
 
Vijiji vingi vikishapata maendeleo na wageni basi utaratibu wa maisha hubadilika,nakumbuka kyela ghala za kuhifadhia nafaka(ndamba) zilikuwa nje bila lock,ngombe walifungwa mbugani mbali na makazi ya watu,wachuuzi wa samaki wanaacha baiskeli zao na kuvuka kufuata samaki mbali hakukuwa na wizi.Ila sasa kesi za wizi zipo.Muingiliano wa jamii tofauti hubadilisha utaratibu wa sehemu husika.vijiji vingi vya wasukuma wanaishi wao tu.
 
Wasukuma asili yao ni waungwana sana na waaminifu
Tunaenda na cash hela ndefu wakati ule tunakusanya mazao wiki nzima na tunawapa hela siku tunafika watuwekee
Hakuna kuiba wala nini
Wana utu na ukifika unashiba kwanza Salaam baadae
Ila wengi wamejichanganya na makabila mengine wamebadilika sana
Ila ndani ndani huko mbona hata mifugo tunawekeza kwao?
 
Nimekaa vijiji kadhaa, na kupita katika harakati zangu nimeona tofauti kubwa.

Usukumani ndani kabisa vijijini hakuna wiziwizi wa ajabu.

Huwezi kusikia wizi wa mifugo.
Watu wanaweka magunia ya mipunga bila ulinzi wa kutisha na unayakuta.

Cha ajabu hata vijiji vya wasukuma waliohamia Sumbawanga na Morogoro hivyohivyo.

Unatembea usiku hakuna mtu mwenye hamu ya kukukaba. Ukisahau pembejeo shambani unazikuta.

Jamaa wengi sio wezi, babda utokee ukame na kuwe na baa la njaa. Ila kwingineko huko tunakopitapita jamaa ni wepesi sana, tena ukiwa mgeni lazima uonewe.

Nini chanzo cha hii kitu
Wasukuma na uchawi ni kama pete na kidole,,mimi nimeishi pale geita,nimetembelea vijiji kadhaa,kiukweli vibaka wanaogopa kuiba kwa sababu mifugo,mashamba,mali na biashara zote zimezindikwa kinomanoma!!!ukijichanganya tu,usipokufa utakuwa chizi!!!..ebu nenda pale GNBUSH kaibe uone!!!,,,,nakumbuka kuna shamba la pale KASAMWA,ni shamba la mipera,lipo kando ya barabara kutoka geita kuelekea sengerema,unaambiwa kuna story alinisumulia abiria mwenzangu tulipofika eneo hilo{tulikuwa tukielekea mwanza kupitia BUSISI,,,,jamaa aliniambia"unaona hili shamba,ukiingia ukachuma mapera na ukala hapohapo haina shida,ila ukibeba na kutaka kuondoka nayo,nyoka anakugonga,,{sijui ni kwli au vipi lakini ndivo nilivoambiwa]
 
Usukumani

Kuna falsafa nyingi usukumani mfn unaruhusiwa kuingia shamba ukala zako Ila usiondoke na VITU..

NB.
WAKATI MWINGINE UKICHUMA MAZAO AU TUNDA BILA KUOMBA MWENYE NAYO UNAWEZA KUNGAN'GANIA KWENYE MTI PIA UKICHUMA MAZAO AU TUNDA BILA KUOMBA UNAKUA UMECHUMA ROHO YAKO.
Hii si kweli matunda kwa wasukuma siyo kitu cha kunyimana.
 
Mwalusembe Mkuranga.
Mwalusembe, wizi, uchawi, umalaya, umbeya vyote vyao.

Kile kijiji sijui kimelaaniwa na nani ?

Nimewahi kukaa hapo 2015-2017 nilikuwa nalima matikiti maji kijiji cha Kikoo picha linaanza ile kufikisha watu wangu wa kazi wote wakaugua macho kila siku wanatoa machozi tu, usiku ndani vurugu haziishi. Ikabidi niwahamishie shambani huko huko hapo mwalusembe siyo.
 
Wasukuma asili yao ni waungwana sana na waaminifu
Tunaenda na cash hela ndefu wakati ule tunakusanya mazao wiki nzima na tunawapa hela siku tunafika watuwekee
Hakuna kuiba wala nini
Wana utu na ukifika unashiba kwanza Salaam baadae
Ila wengi wamejichanganya na makabila mengine wamebadilika sana
Ila ndani ndani huko mbona hata mifugo tunawekeza kwao?
Kweli wanaungwana sana japo wapo wenye tabia za hovyo lakini wengi ni watu wema tu
 
Back
Top Bottom