Kwanini usile tena mkate mweupe kuanzia leo?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,850
34,300
KWA NINI USILE TENA MKATE MWEUPE KUANZIA LEO.jpg

Mkate ndiyo chakula kikuu cha kila siku cha familia nyingi duniani, hasa sehemu za mijini na ndiyo chakula kinachotumika na watu wa rika zote, wakubwa kwa wadogo, lakini ni wangapi tunajua kuwa mkate mweupe, ambao ndiyo chaguo namba moja la familia nyingi, ni hatari kwa afya zetu?

Kuna msemo maarufu wa Kiingereza kuhusu mkate mweupe usemao:
The Whiter the Bread, the Quicker You are Dead!
kwa tafsiri isiyo rasmi, msemo huu unamaanisha kuwa ‘kadiri unavyopenda kula mkate mweupe, ndivyo utakavyokufa haraka!’ Amini, usiamini, mkate mweupe siyo mzuri kwa afya yako!

Inawezekana kabisa habari hii isikufurahishe, lakini kama kweli unataka kuboresha afya yako, unapambana na suala la kupunguza unene, unataka kujiepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (Type II), ugonjwa wa moyo au saratani ya tumbo, basi huna budi ya kuachana na mkate mweupe.
Kama tulivyosisitiza kila mara katika makala zetu nyingi za nyuma kuwa vyakula vyote vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa vina hasara zaidi kiafya kuliko faida, mkate mweupe nao ni miongoni mwa vyakula hivyo.

KWA NINI USILE MKATE MWEUPE?
Kama ujuavyo, mkate unatengenezwa kutokana na ngano na mkate mweupe unatokana na unga wa ngano iliyokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu vya asili ambavyo huwa muhimu katika uimarishaji wa mfumo wa usagaji na umeng’enyaji chakula tumboni (Digestive system and metabolism).
Ili unga uwe mweupe, ngano baada ya kukobolewa husafishwa kwa mashine maalumu kwa kutumia kemikali na joto kali, kitendo ambacho huondoa kabisa virutubisho vinavyoweza kuwemo kwenye nafaka na hivyo kuiacha punje ya ngano ikiwa nyeupe na kubaki makapi.
Makapi hayo, baadaye husagwa na kuwa unga safi na mweupe ambao hutayarishwa kabla ya kutengenezwa mkate kwa kupitia hatua mbalimbali, ikiwemo hatua ya kuwekewa hamira ili uumuke, kuongezewa sukari pamoja na chumvi ili kuongeza ladha.

MADHARA YANAYOWEZA KUKUPATA KWA KULA MKATE MWEUPE

Madhara ya kwanza unayoweza kuyapata kwa kupenda sana kula mkate mweupe ni ugonjwa wa kisukari. Utafiti unaonesha kuwa mkate au chakula chochote kilichotengenezwa kutokana na unga mweupe kina kiasi kingi cha wanga ambao husababisha kuongezeka sukari mwilini.

Madhara mengine yatokanayo na mkate mweupe ni kuongezeka kwa lehemu (bad LDL cholesterol) kwenye damu, hali ambayo inaweza kusababisha presha au magonjwa ya moyo yatokanayo na kusinyaa au kuziba kwa mishipa ya damu.

Madhara hayajaishia hapo, mengine yanayoweza kukupata ni tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu. Mkate mweupe huchangia kuvuruga mfumo wa umeng’enyaji wa chakula tumboni (metabolism). Mwili unapokuwa hauna virutubisho vya kutosha, usagaji na uondoaji wa sumu mwilini huwa wa shida na uchafu unaporundikana tumboni kwa muda mrefu bila kutoka, husababisha kansa ya tumbo!

ULE NINI BADALA YA MKATE?

Kuna aina nyingine ya mkate ambayo ndiyo unayopaswa kula, mkate huo ni BROWN BREAD au MKATE MWEUSI kama unavyojulikana na wengine. Mkate huu hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa hivyo kuwa na virutubisho vyake asilia vinavyohitajika mwilini na kuwa na faida zitakazokuepusha na kupatwa na madhara yaliyotajwa hapo juu. Mkate huu hauna sukari wala chumvi, hivyo kuwa bora zaidi kwa afya yako. Kama kweli unajijali, utaacha kula mkate mweupe na kuanza kula huu mweusi leo!
 
Asante kwa somo dr. Majuzi hapa nilijipongeza sana, nilipick mkate late kidogo nikakuta wa brown umeisha nikachukua mweupe. Nilishindwa kula ule mkate hadi ukaharibika.

Ukizoea brown bread huwezi kula mweupe tena manake unagundua utamu wake.
Hongera mimi ukiisha Mkate wa Brown niko teyari kuchemsha viazi na mayai ya kuchemsha nile asubuhi tena hiyo. Siwezi kuuchukuwa mkate mweupe unanifunga nisapate kwenda haja kubwa.
 
Mkuu MM,

Hili ni somo zuri sana.

Mimi nilikuwa ni mpenzi wa mkate tangu mdogo na si unakumbuka mkate wa siha kutoka pale National Milling, pamoja na TanBond?

Lakini baadae hasa nilipohamia ughaibuni nikaja kugundua kwamba mkate mweusi ndio wenye manufaa sana na hasa ule wenye mbegumbegu na nakshi za nafaka asili ya ngano.

Ni mkate ambao ukiula hata bila siagi unakuwa mtamu tu na baada ya muda unaanza kufanya kazi tumboni.

Mkate mweupe unatumia nguvu nyingi kuchota vitamins, maji na madini mengine katika kujisaga na baadae kuhifadhi mafuta na magando mengine kwenye hifadhi ndani ya utumbo bila kutoa chochote na ndio vitambi na matumbo au "waistline" huanzia hapo.

Kwa kifupi ukiacha mikate, sukari, vyakula vya kutengenezwa na maziwa na ukajaribu yai la kuchemsha, boga viazi vitamu na juisi ya kukamua mwenyewe na chai isiyo sukari, basi unaweza kuepuka matatizo mengi likiwemo la uzito na vitambi au tumbo.
 
Ahsanta Dr. MM.

Kwa kuongezea tu kama anataka kupika home made bread basi tumieni unga wa atta. Kwa maandazi na mikate aina yote. Si lazima hadi tununue brown loaves au slices supermarkets.

Tena chapati za atta tamu ajabu.

Kwa wapenzi wa biscuits au salt crackers zipo za brown pia ambazo ni very tasty.

Say no to white bread, say no to white flour.
 
View attachment 319242

Mkate ndiyo chakula kikuu cha kila siku cha familia nyingi duniani, hasa sehemu za mijini na ndiyo chakula kinachotumika na watu wa rika zote, wakubwa kwa wadogo, lakini ni wangapi tunajua kuwa mkate mweupe, ambao ndiyo chaguo namba moja la familia nyingi, ni hatari kwa afya zetu?

Kuna msemo maarufu wa Kiingereza kuhusu mkate mweupe usemao:
The Whiter the Bread, the Quicker You are Dead!
kwa tafsiri isiyo rasmi, msemo huu unamaanisha kuwa ‘kadiri unavyopenda kula mkate mweupe, ndivyo utakavyokufa haraka!’ Amini, usiamini, mkate mweupe siyo mzuri kwa afya yako!

Inawezekana kabisa habari hii isikufurahishe, lakini kama kweli unataka kuboresha afya yako, unapambana na suala la kupunguza unene, unataka kujiepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (Type II), ugonjwa wa moyo au saratani ya tumbo, basi huna budi ya kuachana na mkate mweupe.
Kama tulivyosisitiza kila mara katika makala zetu nyingi za nyuma kuwa vyakula vyote vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa vina hasara zaidi kiafya kuliko faida, mkate mweupe nao ni miongoni mwa vyakula hivyo.

KWA NINI USILE MKATE MWEUPE?
Kama ujuavyo, mkate unatengenezwa kutokana na ngano na mkate mweupe unatokana na unga wa ngano iliyokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu vya asili ambavyo huwa muhimu katika uimarishaji wa mfumo wa usagaji na umeng’enyaji chakula tumboni (Digestive system and metabolism).
Ili unga uwe mweupe, ngano baada ya kukobolewa husafishwa kwa mashine maalumu kwa kutumia kemikali na joto kali, kitendo ambacho huondoa kabisa virutubisho vinavyoweza kuwemo kwenye nafaka na hivyo kuiacha punje ya ngano ikiwa nyeupe na kubaki makapi.
Makapi hayo, baadaye husagwa na kuwa unga safi na mweupe ambao hutayarishwa kabla ya kutengenezwa mkate kwa kupitia hatua mbalimbali, ikiwemo hatua ya kuwekewa hamira ili uumuke, kuongezewa sukari pamoja na chumvi ili kuongeza ladha.

MADHARA YANAYOWEZA KUKUPATA KWA KULA MKATE MWEUPE

Madhara ya kwanza unayoweza kuyapata kwa kupenda sana kula mkate mweupe ni ugonjwa wa kisukari. Utafiti unaonesha kuwa mkate au chakula chochote kilichotengenezwa kutokana na unga mweupe kina kiasi kingi cha wanga ambao husababisha kuongezeka sukari mwilini.

Madhara mengine yatokanayo na mkate mweupe ni kuongezeka kwa lehemu (bad LDL cholesterol) kwenye damu, hali ambayo inaweza kusababisha presha au magonjwa ya moyo yatokanayo na kusinyaa au kuziba kwa mishipa ya damu.

Madhara hayajaishia hapo, mengine yanayoweza kukupata ni tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu. Mkate mweupe huchangia kuvuruga mfumo wa umeng’enyaji wa chakula tumboni (metabolism). Mwili unapokuwa hauna virutubisho vya kutosha, usagaji na uondoaji wa sumu mwilini huwa wa shida na uchafu unaporundikana tumboni kwa muda mrefu bila kutoka, husababisha kansa ya tumbo!

ULE NINI BADALA YA MKATE?

Kuna aina nyingine ya mkate ambayo ndiyo unayopaswa kula, mkate huo ni BROWN BREAD au MKATE MWEUSI kama unavyojulikana na wengine. Mkate huu hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa hivyo kuwa na virutubisho vyake asilia vinavyohitajika mwilini na kuwa na faida zitakazokuepusha na kupatwa na madhara yaliyotajwa hapo juu. Mkate huu hauna sukari wala chumvi, hivyo kuwa bora zaidi kwa afya yako. Kama kweli unajijali, utaacha kula mkate mweupe na kuanza kula huu mweusi leo!
 
Ahsante sana dr mzizi mkavu.
Maana hii kitu natumiaga sana ila kuanzia leo nasema sasa basi tena.
 
Vitumbuwa vyeupe kula tu hakuan shidabibie inaonyesha ndio ugonjwa wako? nitaweka Thread ya faida na hasara ya kula vitumbuwa.:D

Dr. MM vipi kuhusu chapati, maandazi na bagia (nadhani wanatengeneza kwa dengu) ukizingatia na suala la kupunguza unene maana hata chapati zenyewe tushazoea mbili ila ndiyo hivyo za ngano nyeupe
 
Hongera mimi ukiisha Mkate wa Brown niko teyari kuchemsha viazi na mayai ya kuchemsha nile asubuhi tena hiyo. Siwezi kuuchukuwa mkate mweupe unanifunga nisapate kwenda haja kubwa.
Mkuu viazi havina wanga? Na je vipi kuhusu vyakula kama wali, chapati, maandazi, tambi, makande etc si pia vina wanga? Ugali najua nitapika dona but hivyo hapo juu tunafanyaje?
 
Yeah ,sababu nyingine ya kutokula mkate mweupe ni hii.
 
Attachments

  • IMG-20160127-WA0006.jpg
    IMG-20160127-WA0006.jpg
    28.1 KB · Views: 428
Sijui ndio maana nimeanza kuota kitambi. Katika siku 7 za wiki angalau siku 5 nakula angalau slice 2 za mkate.....duh! Ofisi yetu inatoa chai asubuhi kutakua na vitafunwa vingine lakini mkate lazima uwepo. Ntachange....

Na je docta MM vipi kuhusu mkate mweupe mixer margarine kama vile tanbond, blueband etc
 
Nakumbuka wakati tunasoma Tosamaganga Sekondari tulikua tunaenda kununua maandazi yaliyotengenezwa kwa ngano isiyo kobolewa pale kwenye convent ya masista wa kanisa katoliki. I really miss those days......since then sijawahi kula andazi lisilokobolewa.
 
View attachment 319242

Mkate ndiyo chakula kikuu cha kila siku cha familia nyingi duniani, hasa sehemu za mijini na ndiyo chakula kinachotumika na watu wa rika zote, wakubwa kwa wadogo, lakini ni wangapi tunajua kuwa mkate mweupe, ambao ndiyo chaguo namba moja la familia nyingi, ni hatari kwa afya zetu?

Kuna msemo maarufu wa Kiingereza kuhusu mkate mweupe usemao:
The Whiter the Bread, the Quicker You are Dead!
kwa tafsiri isiyo rasmi, msemo huu unamaanisha kuwa ‘kadiri unavyopenda kula mkate mweupe, ndivyo utakavyokufa haraka!’ Amini, usiamini, mkate mweupe siyo mzuri kwa afya yako!

Inawezekana kabisa habari hii isikufurahishe, lakini kama kweli unataka kuboresha afya yako, unapambana na suala la kupunguza unene, unataka kujiepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (Type II), ugonjwa wa moyo au saratani ya tumbo, basi huna budi ya kuachana na mkate mweupe.
Kama tulivyosisitiza kila mara katika makala zetu nyingi za nyuma kuwa vyakula vyote vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa vina hasara zaidi kiafya kuliko faida, mkate mweupe nao ni miongoni mwa vyakula hivyo.

KWA NINI USILE MKATE MWEUPE?
Kama ujuavyo, mkate unatengenezwa kutokana na ngano na mkate mweupe unatokana na unga wa ngano iliyokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake muhimu vya asili ambavyo huwa muhimu katika uimarishaji wa mfumo wa usagaji na umeng’enyaji chakula tumboni (Digestive system and metabolism).
Ili unga uwe mweupe, ngano baada ya kukobolewa husafishwa kwa mashine maalumu kwa kutumia kemikali na joto kali, kitendo ambacho huondoa kabisa virutubisho vinavyoweza kuwemo kwenye nafaka na hivyo kuiacha punje ya ngano ikiwa nyeupe na kubaki makapi.
Makapi hayo, baadaye husagwa na kuwa unga safi na mweupe ambao hutayarishwa kabla ya kutengenezwa mkate kwa kupitia hatua mbalimbali, ikiwemo hatua ya kuwekewa hamira ili uumuke, kuongezewa sukari pamoja na chumvi ili kuongeza ladha.

MADHARA YANAYOWEZA KUKUPATA KWA KULA MKATE MWEUPE

Madhara ya kwanza unayoweza kuyapata kwa kupenda sana kula mkate mweupe ni ugonjwa wa kisukari. Utafiti unaonesha kuwa mkate au chakula chochote kilichotengenezwa kutokana na unga mweupe kina kiasi kingi cha wanga ambao husababisha kuongezeka sukari mwilini.

Madhara mengine yatokanayo na mkate mweupe ni kuongezeka kwa lehemu (bad LDL cholesterol) kwenye damu, hali ambayo inaweza kusababisha presha au magonjwa ya moyo yatokanayo na kusinyaa au kuziba kwa mishipa ya damu.

Madhara hayajaishia hapo, mengine yanayoweza kukupata ni tatizo la ukosefu wa choo kwa muda mrefu. Mkate mweupe huchangia kuvuruga mfumo wa umeng’enyaji wa chakula tumboni (metabolism). Mwili unapokuwa hauna virutubisho vya kutosha, usagaji na uondoaji wa sumu mwilini huwa wa shida na uchafu unaporundikana tumboni kwa muda mrefu bila kutoka, husababisha kansa ya tumbo!

ULE NINI BADALA YA MKATE?

Kuna aina nyingine ya mkate ambayo ndiyo unayopaswa kula, mkate huo ni BROWN BREAD au MKATE MWEUSI kama unavyojulikana na wengine. Mkate huu hutengenezwa kutokana na ngano isiyokobolewa hivyo kuwa na virutubisho vyake asilia vinavyohitajika mwilini na kuwa na faida zitakazokuepusha na kupatwa na madhara yaliyotajwa hapo juu. Mkate huu hauna sukari wala chumvi, hivyo kuwa bora zaidi kwa afya yako. Kama kweli unajijali, utaacha kula mkate mweupe na kuanza kula huu mweusi leo!
Unaweza ukatuonyesha ngano iliyokobolewa na isiyokobolewa unga wake
 
Asante kaka mkubwa;
Tatizo huku kwetu wapo waoka mikate wanaweka rangi ya brown
badala ya kutumia ngao isiyokobolewa
 
Back
Top Bottom