Kwanini Urusi na China hawakumkinga Maduro?

Kwanini Urusi na China hawakumkinga Maduro?

CalvinPower

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
1,675
Reaction score
1,060
Baada ya taarifa kusambaa kuwa rais wa Venezuela alichukuliwa na vikosi vya Marekani, wengi waliuliza swali moja: Urusi na China walikuwa wapi? Kwa nini hawakuingilia kumlinda mshirika wao?
Jibu lake halihusiani na hisia, bali u halisia wa nguvu za dunia.

Kwanza, jiografia huamua nguvu.
Venezuela iko katika ukanda ambao kwa zaidi ya karne moja umekuwa chini ya ushawishi wa kijeshi wa Marekani. Marekani ina vituo vya kijeshi, meli za kivita, na uangalizi wa anga katika Karibiani. Kwa Urusi na China, kuingilia moja kwa moja kungehitaji kupeleka majeshi yao ndani ya Venezuela — hatua ambayo ingekuwa sawa na kutangaza vita dhidi ya Marekani. Hilo si jambo Moscow wala Beijing wako tayari kulifanya.

Pili: Urusi na China hawalindi watu, wanalinda maslahi.
Katika siasa za kimataifa hakuna “urafiki wa milele”.
Kuna mafuta, mikopo, silaha, na ushawishi.
Kiongozi akianguka, wanakaa mezani na anayefuata.
Ndiyo maana wanaweza kumpigia kelele Maduro leo, na kesho wakafanya mazungumzo na serikali mpya bila aibu.

Tatu: Hakuna mkataba wa kumlinda Maduro.
Venezuela si NATO ya Urusi wala China.
Hakuna mkataba unaosema “ukimgusa Maduro tutapigana”.

Nne: Operesheni za kisasa hazitangazwi.
Kama Marekani ilifanya operesheni, ilifanya kwa kasi, kwa siri, na kwa taarifa za ndani.
Urusi na China hawadhibiti jeshi la Venezuela, hawakai kwenye ulinzi wa rais, hawapati alerts za dakika hadi dakika.
Unapofungua TV, kazi tayari imeisha.

Tano: Hatari ilikuwa kubwa kuliko faida.
Kuingilia kungeua wanajeshi wa Marekani.
Kulipiza kisasi kungefuata.
Vikwazo vingelipuka.
Masoko ya dunia yangetikisika.
Hakuna taifa linalohatarisha uchumi na usalama wake kwa mtu mmoja.

Hitimisho ambalo wengi hawataki kulisikia:
Urusi na China hawakumsaliti Maduro.
Waliheshimu uhalisia wa nguvu za dunia.
 
Kwa uhalisia wa siasa za kimataifa, China na Russia HAWAWEZI “kum-rescue” Maduro kirahisi kama watu wanavyodhani.

Kwanza, Maduro akishakuwa chini ya ulinzi wa Marekani, jaribio lolote la kumtoa kwa nguvu lingekuwa sawa na kutangaza vita ya moja kwa moja dhidi ya Marekani. Hilo si jambo ambalo China au Russia wako tayari kulifanya kwa mtu mmoja, hata kama ni mshirika wao.

Pili, China na Russia hupigana vita kwa njia tofauti. China ni nguvu ya kiuchumi na kimfumo, si ya operesheni za kijeshi za kuvamia nchi nyingine mbali na mipaka yake. Russia kwa sasa iko kwenye mzigo mkubwa wa kijeshi na kiuchumi, hivyo haiwezi kufungua uwanja mpya wa vita Karibiani.

Tatu, historia inaonyesha kuwa nchi kubwa hazihatarishi vita ya dunia kwa ajili ya kiongozi mmoja. Wanacholinda ni maslahi yao ya muda mrefu, si watu binafsi. Ndiyo maana hata Saddam na Gaddafi hawakuwahi “kuokolewa” na washirika wao.

Kile China na Russia wanaweza kufanya ni:
  • shinikizo la kidiplomasia kupitia UN
  • vita ya taarifa na propaganda
  • hatua za kiuchumi au kisiasa
  • kuharakisha mipango ya kujiondoa kwenye utegemezi wa dola

Lakini operesheni ya kijeshi ya kumtoa Maduro Marekani? Hilo ni ndoto ya mitandao, si uhalisia wa geopolitics.

Katika siasa za dunia, hakuna “rescue mission” kwa viongozi. Kuna maslahi tu.
 
Ilipangwa hiyo kwa sasa kila mbabe anaangalia maslahi yake na wamekubaliane kamWe hawataingiliana kivita moja kwa moja
 
Kwa ufupi ungetueleza kwamba;USA amewazidi maarifa kwa hatua nyingi mbele.Mwenzao anacheza kotekote ila wao wana mipaka ya kujidaia.Kwisha.
Osama alifuatwa Pakistan na kuadabishwa.Muuza madawa Pablo (kama sikosei)alifuatwa nje ya mipaka ya USA na wengine wengi tu.Nisingeona ajabu hata yule askari wa USA aliyeshikiliwa Tanganyika angefuatwa na kuchukuliwa.
 
Back
Top Bottom