Kwanini upinzani wanaendelea kuwapokea CCM?

Kwanini upinzani wanaendelea kuwapokea CCM?

bobo lee

Senior Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
111
Reaction score
19
Huwa nashangaa ni kwanini sisi Watanzania tunakuwa wepesi wa kusahau.Mimi binafsi kama mdau wa siasa japo si mwanachama wa chama chochote naliona kosa moja wanalolifanya wapinzani nalo ni kufurahia kupokea wanachama kutoka CCM wakati wengi wao ni mamluki.Hivi wapinzani hawajajifunza kutoka kwa watu kama akina Shibuda.
 
Chama hakiwezi kuepuka kuchukua wanachama wa vyama vingine. Chama ni kama daladala, wengine wanatelemka na wengine wanapanda na sio wote wanaoingia ni mamluki kuna wengine wameshakerwa na mfumo wa chama fulani kwa hiyo wanatafuta unafuu chama fulani.
 
Ulitaka wafanye nini wakati wanachama wao wote wametoka ccm twambie nani kwenye vyama vya upinzani hajatoka ccm.
 
Huwa nashangaa ni kwanini sisi Watanzania tunakuwa wepesi wa kusahau.Mimi binafsi kama mdau wa siasa japo si mwanachama wa chama chochote naliona kosa moja wanalolifanya wapinzani nalo ni kufurahia kupokea wanachama kutoka CCM wakati wengi wao ni mamluki.Hivi wapinzani hawajajifunza kutoka kwa watu kama akina Shibuda.
Waulize wapinzani nani ambaye hakutokea ccm asimame ahesabiwe tumuone.
 
Acha uongo mkuu Bobolee kwamba,hauna mapenzi na chama cho chote cha siasa ? NIKUSEMA, "HAUPO KWA MOLA NA KWA SHETANI"!
 
Last edited by a moderator:
Huwa nashangaa ni kwanini sisi Watanzania tunakuwa wepesi wa kusahau.Mimi binafsi kama mdau wa siasa japo si mwanachama wa chama chochote naliona kosa moja wanalolifanya wapinzani nalo ni kufurahia kupokea wanachama kutoka CCM wakati wengi wao ni mamluki.Hivi wapinzani hawajajifunza kutoka kwa watu kama akina Shibuda.

Hivi hapa unaelewa ulichokisema lakini? wewe ni mdau wa siasa halafu si mwanachama wa chama chochote, unadhani watawatoa wapi wanachama wengine ambao kama hawajatoka ccm, wakati ccm imejaza hadi inawakopesha na hata muda mwingine inaamua kuwapunguzia wanachama.
 
Wapo watu wasio wanachama wa chama chochote lakini kumbuka kuwa wanachama ni wananchi.. Huwezi wakataza wananchi kujiunga na harakati wanazo amini zitawakomboa!

Kwamba wengine ni mamluki hilo ni vigumu kulikwepa kwa sababu ni hulka ya binadamu.... ni jukumu la vyama kuweka kanuni na taratibu za kudhibiti tabia na mienendo ya wanachama wake!!
Ingekuwa rahisi kama unavyodhani bora vyama vya siasa vingesajili watoto wadogo mara wanapozaliwa. Lakini si rahisi hivyo... kanuni za siasa zinakataa kata kata!

Hata nyumbani kwako wapo wageni mamluki wanaokutembelea kwa malengo mbali mbali lakini busara ya kawaida ni kuwapokea wote tena kwa heshima, upendo... kuwa au kutokuwa muangalifu na wageni uwapokeao ni jukumu lako mwenyewe!
 
Hakuna upinzani Tanzania ccm wamebadilika tuu na kujiita chadema cut nk
 
Nalisema hili kwa sababu kipindi hiki ni kipindi cha kuelekea kwenye chaguzi vyama visije vikawa kama kokoro la kubebea wazuri na wabaya.Malengo ya wengi wanaojiunga na upinzani muda huu hayaeleweki,inawezekana ni kusaka vyeo baada ya kuvikosa walikotoka,pia inawezekana ni kupeleleza mbinu na mipango ya vyama husika,kufanya ujasiria siasa kwa maslahi.Hisia zangu kutokana na historia zinanipelekea kuamini kwamba wengi wana nia ovu.Furaha yangu ni kuona nguvu za utawala na upinzani ziko sawa kwa maendeleo,uwazi na haki.Binafsi najiita mdau wa siasa kwa sababu naifuatilia japo nayaona mapungufu mengi sana kwenye vyama ambayo hayarekebishiki kwa sasa labda hapo baadae hivyo sipendi kuumiza kichwa,kwa sasa ni muumini wa dini na sio hiki kinachoitwa sihasa.
 
Back
Top Bottom