Kwanini unapaswa kununua bond au Hati fungani ya NMB?

Copy1

Member
Feb 10, 2016
96
143
Uwekezaji katika Bond au Hati fungani ni aina ya uwekezaji ambao imekuwepo kwa muda mrefu sana katika nchi mbalimbali,

Hata hivyo hapa nchini kwetu dhana hii ya uwekezaji bado inaonekana kwa ni ngeni miongoni mwa watu wengi

Bondi au Hati fungani ni nini?

Ni uwekezaji ambapo mwekezaji anaikopesha serikali au kampuni, na serikali hiyo au kampuni inaahidi kumlipa mwekezaji huyo baada ya hatifungani hiyo kukomaa,

Kwa kawaida faida inayoambatana na uwekezaji katika bond hugawiwa kila baada ya miezi 6.

Benki ya NMB ambayo ndiyo the most profitable bank, na ndiyo benki iliyo sambaa zaidi nchini Tanzania kwa sasa imetangaza uuzaji wa hatifungani yake, ambapo imeanza kuuzwa kutoka tarehe 10 May na itauzwa hadi tarehe 8 June 2016, kupitia madalali 10 wa soko la Hisa la Dar es salaam Mfano Arch Financials & Investments Advisory Limited wanaopatikana katika jengo la NIC life house lililopo mtaa wa sokoine posta jijini Dar es salaam, (Tel:+25522732922396,Mob: 0784952814) au Kupitia Tawi lolote la NMB lililo karibu nawe

Kwa Kiasi kidogo tu cha uwekezaji cha shillingi laki tano (500,000) unapata faida ya asilimia 13% kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu ambapo faida hii inakuwa inalipwa mara mbili kwa mwaka, bila kusahau kuwa bondi itakapo komaa "mature" NMB itakulipa pesa yako yote uliyokuwa umewekeza awali

Hati fungani hii ya NMB walengwa wakuu ni wawekezaji wadogo na wakati, japo hata wakubwa hawajazuiwa na ndiyo maana kiwango cha chini cha uwekezaji ni Tsh 500,000/= Tu na kuendelea, tofauti na Bondi nyingine za makampuni zilizo wahi tokea hapa Tanzania

Chukulia kama umewekeza Shillingi 1,000,000 kwa riba ya 13% kwa mwaka, hivi ndivo itakavyokuwa

1.Interest=Principal*Rate* Time

=1,000,000*13/100*1year

=Shillingi 130,000

2.Lakini interest hii inalipwa mara mbili kwa mwaka hivyo malipo ya mkupuo wa kwanza yatakuwa ni TZS130,000/2 =TZS 65,000/=

3.Kila mkupuo wa malipo unatozwa kodi ya zuio ya 10%

=65,000-(65000*10%)

=65,000-6,500

=TZS 58,500

Hivyo kufikia Disemba 2016(baada ya miezi 6) utapokea Shillingi 58,500

4.Baada ya miaka 3, uwekezaji wako katika hatifungani hii utakuwa umekuingizia Shillingi 351,000 (58,500*6) kutoka katika uwekezaji wako wa Shillingi 1000,000. Shullingi 1M yako itakwa imekuwa hadi kufikia shillingi 1,351,000 pasipo wewe kufanya chochote, umeingiza pesa hizi ukiwa umekaa tu nyumbani au upo kwenye shughuli zako nyingine.

Isitoshe endapo utapata dharura, kabla miaka mitatu haija isha,na ukahitaji hizi pesa zako bado una nafasi ya kupata pesa zako ulizo wekeza , ambapo utaweza ku uza hatifungani hii katika soko la Hisa la Dar es salaam, kupitia madalali wake

==========
NYONGEZA:
==========

Hati fungani za NMB zimekuja kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini ile wenye kuweka hela (saving) kiasi na hawaitumii mpaka muda waliojipangia au dharula inapotokea.

Hizi za NMB zimegawanywa katika 500,000/- kwa bond, ni watu wengi sana wenye kipato cha wastani huwa wanakuwa na balance ya namna hii au zaidi kwenye acc tena inakuwepo kwa zaidi ya mwaka inakatwa tu monthly charges nk, badala ya kuongezeka inapungua.

Hii 500,000 haiwezi kununua fixed deposit (FDR) kwa sababu mara nyingi FDR zinakuwa na min limit ya zaidi hata mili 5 na kuendelea, na rate zake ni 12-16. Ili upate rate ya 15 au 16 ni lazima uweke hela nyingi kuanzia hata mil 100. Kwa mil 10 unaishia kupata 12 au 13, so kama unaweza kupata 13% kwa sh 500,000 ni faida sana.

Hati fungani za serikali ni kwa wenye hela nyingi zaidi, maana unakuta moja inauzwa kwa sh mil 500 na kuendelea na ni kwa miaka 5 au zaidi, rate zake mara nyingi ni 14-16.5%. Hizi sisi hatuwezi.

Kuna watu wanasema kuliko kupata hiyo faida ya 130,000 kwa mwaka akiweka mil 1 ni bora akafanyie biashara gani apate faida zaidi, sasa watu hawa hawa unakuta anaongea hivyo ana hela benki ambazo zipo tu na hata hizo biashara hawafanyi na hela inakatwa charges.

Pole pole watu wakielimishwa wataelewa. Uzuri hii ukiwa na dharula inauzika haraka, na kwenye kuuza utapata faida ila siyo kama ambayo ungepata ukisubiri muda uishe, kuna gharama ya kutoa hati mapema itaathiri faida ila hela yako yote utaipata.
 
Nimehamasika sana!!!
Hati fungani ni fursa nzuri ya kukua kiuchumi ambayo utapata wasaa wa kuwekeza pesa yako inayoanzia 500,000 kwa miaka mitatu kwa riba ya 13% kwa mwaka ambayo utakua unalipwa kila baada ya miezi sita sita..
kwa mfano ukiwekeza 1m then utapata 130,000 kila mwaka kwa kpnd cha miaka 3 s0 utakua unalipwa 65,000 kila baada ya miezi 6 kwa miaka mitatu then mwezi wa mwisho wa mwaka wa tatu utalipwa principle yako plus 65,000 ya mwisho..
Nmb karibu yako
 
Miaka mitatu unatengeneza laki Tatu. si bora hiyo hela nile minenepe. Hii business ni nzuri kwa watu wenye hela nyingi ukiweka milioni 50 faida yake unaiona sasa uweke mil 1 kwenye miaka mitatu upate laki tatu c utani huo? hata muuza vitumbua anatengeneza zaidi ya laki tatu kwa mwaka na mtaji wake wa elf hamsini.
 
Unajua maaana ya Passive Income???

Muuza vitumbua ametengeneza zaid ya laki tatu ndiyo is it passive income??
 
Ila sasa uzuri wa hii kitu ni kwamba, NMB watasababisha watu waliokuwa na savings au fixed deposit kwenye mabenki kuhamisha fedha zao kwenda kwenye bond market, nakumbuka walianza Exim bank sema hawakuitangaza sana. NMB wakiitangaza sana watapata watu, kwa hiyo yale mabenki yanajidai dai kama CRDB and the like yataumbuka tu lazima, lazima na wenyewe either wa raise deposit rate au nao wa issue debt.
Hapo ndo wateja tutaanza kuwa wafalme vizuri na kuwa na choice, hata serikali itaongeza mapato kupitia withholding tax, sio zaman walikuwa wamesinzia sinzia tu.
 
Ila sasa uzuri wa hii kitu ni kwamba, NMB watasababisha watu waliokuwa na savings au fixed deposit kwenye mabenki kuhamisha fedha zao kwenda kwenye bond market, nakumbuka walianza Exim bank sema hawakuitangaza sana. NMB wakiitangaza sana watapata watu, kwa hiyo yale mabenki yanajidai dai kama CRDB and the like yataumbuka tu lazima, lazima na wenyewe either wa raise deposit rate au nao wa issue debt.
Hapo ndo wateja tutaanza kuwa wafalme vizuri na kuwa na choice, hata serikali itaongeza mapato kupitia withholding tax, sio zaman walikuwa wamesinzia sinzia tu.

Watanzania bado hatuna mwamko wa haya mambo ya hati fungani na mambo ya financial market kwa ujumla.

Kama wangekuwa wanajua mbona kila mara serikali inauza hati fungani zake na watu hawaendi kununua?

Iweje hii ya NMB watu wakanunue na sio za serikali ambazo ni salama zaidi?

Watakao nunua hizi za NMB ni walewale wanaonunua kila siku, hasa hayo mabenki.
 
Ni kawaida kabisa kila mtu kuweka pesa ya akiba benki, mfano: mtu anaweka milioni 2 kwa kudunduliza kisha anasema hazigusi mpaka pale atakapo pata dharura au kuna kitu anahitaji kufanya siku zijazo, anachoshindwa tambua kuwa katika akaunti ya akiba ile pesa haitojizalisha zaidi ya kupungua, ila kama akiiweka kama hati fungani hata kama faida ni ndogo ila faida imepatikana bila jasho na bila ya shaka ya kupata hasara na uzuri zaidi katika hati fungani ukihitaji pesa yako hata kabla ya muda unaweza iuza hiyo hati fungani ukachukua pesa yako ukaenda

hati fungani ni nzuri ila kila biashara ina malengo, unaweza ukawa na milioni 1 au milioni 500, suala ni hiyo pesa inayokuja kama faida waitumiaje?

usifanye biashara upate utajiri, fanya biashara upate faida ya uhakika yenye uhakika na uwekeze zaidi utajiri ni matokeo ya kuwekeza muda mrefu kwenye biashara.
 
Tatizo la watanzania wanataka wakiweka mil.1 wapate faida 100% ndani ya mwaka mmoja... Easy money.
 
Hii iko poa xna subir niongeze juhudu za kutafuta kias kikubwa cha pesa ili nije kuwekeza atifungani hii 200 aitoshi itanipa faida ndogo
 
Hii inafaa wanaoweka pesa bank hawana cha kuzifanyia lakini si sisi waganga mjaaa...faida ni ndogo sana nikilinganisha nifanya biashara ya uchuuzi nitapata kubwa kuliko hiyo..
 
duh hapana bora nikopeshe jamaa zangu hilo million moja nilikopeshe kila laki moja ije na 2% ya riba yaani 20000tsh per month
 
Back
Top Bottom