Nadhani hili ndio wazo muhimu kuliko yote hususan kwenye maisha ya sasa ambapo watu wanawapangia watu maisha (mfano watoto wao) wanadhani labda sababu wao wanafurahi kwa wanachofanya au wanashida kwa walichokosa na wenyewe watafurahi, au kusikitika kama wao kwa kupata wanachopata au walichokosa; Mfano wewe ni Mwanasheria una Firm kubwa unamuandaa mtoto wako awe CEO; wakati yeye anapenda kuimba....Mkuu huwa mnawaza nini
MAda nzuri sana na mimi nitaganda hapa kufanya mjadala wa kina ili nipate elimu zaidi katika huu uzi.Swali sio kwamba Kwanini watu wanaishi nauliza kwanini wewe Unaishi ?
Dhumuni la swali ni kujaribu kueleweshana huenda watu tumesahau kwamba Binadamu tupo tofauti chema kwako ni kibaya kwa mwingine...; Ila mwisho wa siku kila mtu anahitaji Kusudi (Purpose); kitu kinachomsukuma kuamka asubuhi na kufanya anachofanya..., Iwe ni kumridhisha mwenza, kuhudumia familia, kutoa elimu, kutoa Tiba, Kutetea wenye shida, Kula Bata n.k.
Kama kila mtu ana kusudi (purpose) inayomfanya kufurahia maisha, kama Jamii hatuoni kwamba tunapotoka tunapodhani watu tunaishi ili kupata Pesa ?; Yaani mtu hapendi kujichanganya na watu tunamwambia awe daktari sababu inalipa au mwanasiasa Je huyu atafurahia maisha wakati anachofanya sio kusudi lake ?
Iweje Msanii / Muimbaji aseme kazi ya Usanii hailipi wakati hata asingelipwa angeweza kuifanya Bure ?!!!
Binafsi nadhani maisha ni simple sana watu ndio wanaya-complicate kwa kutaka kuishi kwa jicho la Jamii linavyokuona na sio wewe binafsi unataka nini au kutokujua ni nini tunataka, na kudhani the Grass is Greener on the Other Side - Hivyo kusahau kuishi bali kutumia muda wetu hapa duniani tuki-chase an ILLUSION....
Kusudi: Ni Sababu ya kitu kufanyika..., kwa muktadha wa hii mada Kusudi ni sababu inayokupelekea wewe kufanya kitu fulani..., Ukiondoa mahitaji muhimu ambayo mtu unahitaji ili uweze kuishi (basic needs), sababu bila hayo huwezi hata kuwaza kufanya mengine..., jaribu kufanya mambo ambayo yanafurahisha moyo wako na si vinginevyo.... (tofauti ya hapo utakuwa mtumwa wa maisha)...Je kwa kuanzia tu mkuu,najuaje kusudi langu mimi ?
Ukiishi lazima ufe, tungekuwa tunaishi ili tufe kuna shortcut tungechukuwa ya kukatisha maisha sasa hivi na sio baadae... na nadhani tungepewa uamuzi na kama tungekuwa hatuzeeki / Kuchoka ni wachache sana wangechagua Kifo (Hence dunia ingekuwa imeshafurika)Tunaishi ili tufe...
Kama tunsishi ili tufe basi nature isingeruhusu tuzaliwe.Tunaishi ili tufe...
Naam ukizingatia Nature inafuata Law of the Fishes...; (Matsya Nyaya is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish. It is described as the fundamental law of nature explained by the proverb of the big fish devouring the smaller fish, hence strong devour the weak)...Kama tunsishi ili tufe basi nature isingeruhusu tuzaliwe.
Kwa sababu kama lengo la kuzaliwa ni ili tufe maana yake ilikuwa lengo la kuzaliwa tumelifikia hata kabla ya kuzaliwa kwa maana kila mtu kabla hajazaliwa anakuwa kafa yaani hayupo duniani.
So hata mimi nadhani lengo sio kufa bali kufa ni hatua ya mwisho ya hapa Duniani baada ya kufanya tuliyofanya hapa Duniani.
Ni sawa na mimba tu,lengo sio kuzaliwa kwa mimba bali lengo ni mimba izaliwe na iishi hapa Duniani.
Naam ukizingatia Nature inafuata Law of the Fishes...; (Matsya Nyaya is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish. It is described as the fundamental law of nature explained by the proverb of the big fish devouring the smaller fish, hence strong devour the weak)...
Kwahio kwa upande wa nature wanyama wanaazaana wenyewe kwa kupenda ile furaha na kuzaana na hata mimea kuwepo kwa me na ke kunapelekea propagation (na wao binafsi aim yao ni kuzaana na wawe wengi na kizazi zao kisipotee) ila kwa jicho la nature specie moja ni chakula ya specie kingine (sisi tunakufa ili tuwe mbolea na chakula cha mimea, ili tule mimea ili tukifa tuwe chakula cha mimea) Imekuwa hivyo sababu hio ndio sustainable way inayofanya dunia iwe stable....
Lakini individually sidhani kama Swala anaweza kukuelewa ukimwambia yupo pale ili Simba aweze kupata mlo (yeye Binafsi yupo pale ili aweze kuishi as long as possible na kula majani) Na kundi la Swala lipo pale ili liweze kuzaana na kizazi chao kisipotee....;
Haya mambo ukiyszungumza kwa watu ambao hawafikirishi bongo zao bila shaka watakuona unazingua na unavuta bangi tu,ni mambo yanahitaji ubongo uliotuliaUnachozungumza uko sahihi sana kwa wenye uelewa,kuna mahala nilishawahi kuwaeleza watu kidogo kuhusu jinsi gani nature ina operate,wengi wao waliishia kusema mi nimeanza kula bangi!
Nadhani hilo ndio swali..., Sio kwanini tunaishi bali kwanini unaishi... na hiyo ndio theme ya Mada ukizingatia sababu yako wewe binafsi huenda sio sababu yangu hivyo kukupangia nakosea ukizingatia hio sababu yako ndio inakupa motivation ya kufanya unachofanya...Kila mtu ana sababu yake ya kuishi , hata kama akili yako haijui ,tambua wewe unajua. ,
Jitafute utajua sababu yako ni nini !!!!!
HakikaNadhani hilo ndio swali..., Sio kwanini tunaishi bali kwanini unaishi... na hiyo ndio theme ya Mada ukizingatia sababu yako wewe binafsi huenda sio sababu yangu hivyo kukupangia nakosea ukizingatia hio sababu yako ndio inakupa motivation ya kufanya unachofanya...
INGAWA inawezekana wewe sababu yako ni kufika Mlimani au Kwenye Bonde na unadhani huko ndipo unapokwenda ila kumbe ile njia unayopitia kwa sasa haikupeleki kwenye Bonde wala mlima bali kwenye Mto..., thus unajikuta maisha yako yote unakimbiza kitu ambacho hakipo au siku ukifika unapata frustrations sababu ulichodhani sicho....
Nimechakata Jibu lako kwenye Grey Matter na Logically lina-make sense kwa mtizamo wa kwamba tunaishi ili baadae tufe (sio nife....); Kwa mtizamo wa Ecosystem....Tunaishi ili tufe...