Kwanini ukipika mchele unajaza sufuria?

MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
5,727
6,610
Wadau amani iwe kwenu,

Kama kichwa kinavyosema hapo juu naomba kujua ni expansion ya namna gani inafanyika pindi ukipika mchele?

Unaweza ukaweka mchele robo sufuria lakini baada ya kuiva unakuta sufuria imejaa? Je, ni nini kinafanyika?

Mnaweza kuona ni swali la ajabu kuwahi kutokea ndani ya viunga vya JF lakini nimejiuliza sana leo bila mafanikio

Hili limekuja wakati nikiwa nakula wali leo, sasa nikajaribu kulinganisha punje ya wali ulioiva na ya mchele ambao bado haujapikwa, Cha kushangaza punje zote zinalingana ukubwa, kama kujaa kwa sufuria ni kutokana na expansions ya mchele, nilikuwa natarajia nione punje ya wali ikiwa kubwa kama ya maharage lakini sivyo, punje ya wali na ya mchele zote zinafanana kwa ukubwa.

Je, hii inatokana na nini?

Jamani uwezo wangu wa kufikiri uliishia hapo, naombeni mnijibu kwa ustaarabu.

NB. Mimi sio mzawa wa Koromije, vyeti ninavyo Ila hili limenishinda.....
 
Kuna kitu kinaitwa MICROPORES, kwa hiyo inanyonya maji na kutanuka.
 
Hii hutokana na maji kufyonzwa na Michele, ukiangalia mchele kabla haujaiva ni mwembamba ukiiva unakuwa mnene, kwa sababu ya maji uliyotumia kupikia, maji hunywea na kuufanya mchele kunenepa, kumbuka unakuwa na michele mingi na yote hufyonza maji hatimaye hunenepa na kujaza chombo ulichopikia na kuita wali sasa. Mchele hata utie maji pekee bila kuupika na uache kwa muda fulani utakuta umeongezeka na maji yamekauka kwenye chombo.
 
Ubarikiwe mkuu, macho basi yalinidanganya maana nilivyolinganisha nikaona yote inafanana ndio maana nkaona kimbilio ni hapa JF
 
ni kwasbb unatia maji kwenye wali unafikiri yale maji yanaendaga wap ndo huvimbisha
kingine ni makande nayo unapika kikombe yanatoka sahani 3
 
Back
Top Bottom