Kwanini uchumi wa nchi haukui?

PendaTz

New Member
Mar 30, 2017
3
1
Nimejiuliza sana kwa nini uchumi haukui, nimegundua hakuna anayepanga na kuweka mikakati bora ili kuikuza, kwa taarifa ya waziri wa fedha aliyoisoma ina mambo mengi ambayo ni nadharia tu.

Hata uchumi ungekua kwa 100%, bado usingeona mabadiliko ya maana. Let alone 7%.
Uchumi wa Tanzania ni 50bn$ ambazo kwa watu milioni 50 ni ndogo mno. Hata ingekua 200bn$ bado ni ndogo sana.

Kwa hiyo, usipende kusikiliza maneno ya walevi, uchumi unakua, ila mpaka uone ukuaji huu, inabidi miaka mingi ipite.
 
Uchumi wa nchi haukui kwa sababu ya sera mbovu, ufisadi, kusaini mikataba ya rasilimali nchini ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania kwa mfano mikataba ya uchimbaji dhahabu ambayo Tanzania inaambulia 5% royalties ambazo ni pesa ndogo sana ukilinganisha na matrilioni ya mapato kwa makampuni ya kigeni nchini. Ubinafsi wa viongozi wa kujilipa mishahara na marupurupu makubwa ukilinganisha na mishahara ya Watanzania walio wengi nchini. Kwa mfano mshahara wa Rais ni zaidi ya milioni 400 kwa mwezi ukilinganisha na mshahara wa kima cha chini ambao ni mdogo sana.

Kwa sababu asilimia kubwa ya Watanzania hawana vipato vikubwa hata purchasing power yao ni ndogo hivyo kuwa na uwezo mdogo sana kuchangia katika pato la Taifa.

Nimejiuliza sana kwa nini uchumi haukui, nimegundua hakuna anayepanga na kuweka mikakati bora ili kuikuza, kwa taarifa ya waziri wa fedha aliyoisoma ina mambo mengi ambayo ni nadharia tu.

PendaTz
 
Back
Top Bottom