website biashara inayotoa huduma hapa Tanzania kuwa na lugha ya kingereza nikupoteza hela tu, ndio maana website nyingi na vingereza vyao huwa zipo ilimradi kampuni ionekane ina website.
Website ni chombo cha kuvutia wateja, sasa kama hauzungumzi lugha yao utawakosa hao wateja.
Unapoandika kingereza maana yake umelenga watu ambao hawajui kiswahili, sasa jiulize Tanzania ni wangapi ambao hawajui kiswahili?
maoni yangu Tovuti zinazotoa huduma hapa Tanzania ziwe kwa lugha ya Kiswahili alafu unatengeneza tovuti mfanano ya pili kwa lugha ya kingereza(kama ukipenda).
Pili, kama mleta mada alivyo sema kublog ni muhimu ilikuelimisha wateja, na kwa lugha ya kiswahili ndio inafaa zaidi kwasababu unauhakika asilimia kubwa atakaye soma anafahamu lugha.
Wageni wenyewe ambao hawajui kiswahili wanapambana sana kujifunza kiswahili, mimi naona hakuna haja ya kuandika kingereza kama biashara yako inatoa huduma hapa Tanzania.