888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 445
- 554
Jamani hebu tuseme ukweli, lakini kwa utulivu... Hii nchi tuna vyama 19 vya siasa na wengine wanataka kuvifikisha 30! 😳
Nimekuwa nikijiuliza tu, kwanini tusibakize vyama vitatu vya maana—vitatu tu lakini vyenye meno, misuli na ushawishi?
1.Kimoja cha mrengo wa kulia,
2.Kimoja cha mrengo wa kushoto,
3.Kimoja cha katikati (wasiojua wako wapi 😅)
Kisha tukaruhusu wagombea huru – wale wasiofungamana na chama lakini wana nguvu mitaani na moyo wa kizalendo.
📲 Namna ya Kupunguza Vyama sasa:
Hii itafanyika kwa uzalendo na teknolojia. Tunaanzisha mfumo wa kisasa kabisa:
Kila Mtanzania anajisajili kwa kutumia namba ya NIDA na kuchagua chama chake kupitia:
1.Simu (USSD),
2.Kompyuta,
3.Ama stationaries/vituo vya huduma vijijini.
Baada ya usajili:
Tunasema Mfano labda Chama kisichofikisha wanachama 5,000,000 kwa kitaifa na 10,000 kwa angalau mikoa minne kinapewa kadi ya njano...
Kikiwa kimelala hadi muda wa mwisho – kinapewa kadi nyekundu (kimya kimya hakipewi tena ruzuku wala taarifa kwenye TV).
Wanachama wake wanaarifiwa wachague chama kingine ama wawe huru.
💸 Kwanini Hii Inahitajika?
1.Kupunguza gharama ya ruzuku kwa vyama visivyo na mvuto wala sera.
2.Kuhimiza vyama vianze kushindana kwa sera, si kutegemea bendera na nembo za msajili.
3.Kujenga mfumo wa siasa wa kueleweka: wananchi wajue tofauti ya chama A na B, si A na A’ ambayo ni kivuli chake.
4.Kukomesha siasa za "vijisentiko" – chama kinapokea milioni halafu kinafanya mkutano wa wanachama 7, wanne wakiwa ni jamaa wa mwenyekiti. 😂
🤷🏽♂️ Siyo Sera Rasmi, Ni Fikira za Mtaani Tu... Lakini?
Najua wapo watakaosema huu ni udikteta kwa kivuli cha utaratibu. Lakini jamani, kwa mtu anayejali kodi yake na mustakabali wa taifa, si bora udikteta wa hoja kuliko uhuru wa matapishi ya kisiasa?
✍🏽 Tuanzishe Mjadala:
Je, Tanzania ina vyama vingi sana visivyo na mchango?
Je, mfumo wa wanachama kwa NIDA unaweza kusaidia kuchuja pumba kwenye kisiasa?
📌 #VyamaVitatu #SiasaZaMaendeleo #UkweliKwaUcheshi