Kwanini tunazalilishana kiasi hiki?.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Wanajamvi nilikua naangalia TBC habari,na taarifa ya mwisho alionyeshwa kijana mmoja kwa jina JUMA MUSA ni mlemavu wa macho (kipofu) lakina alibahatika kufaulu na kuanza kudato cha kwanza (sikupata vyema ni mkoa gani na amechaguliwe shule gani) lakini hakuweza kuendelea na shule kutokana na wazazi wake kukosa uwezo wa kumsomesha.

chakushangaza ni kuwa hakukatatama ya kutafuta msaada.alìpita ofisi mbalimbali za serikali mpaka kwa mkuu wa mkoa na hata wa wilaya lakini msaada alioupata ni kupewa barua inayomruhusu kuwa ombaomba na kumwambia aende kuomba makanisani na msikitini

tunaenda wapi jamani? Walishindwa nini kumwezesha mlemavu huyu kuendelea na masomo? viongozi hawa wanamsaada gani kwetu kama wanashindwa na jamboa dogo kiasi hiki.

kweli tunasafari ndefu
 
Kumpa kibali cha kuwa omba omba ndiyo msaada wao mkubwa sana
 
Hawa jamaa mi huwa si waelewi wana upumbavu wa aina gani vichwani mwao, kuna mkoa nilienda kila mlemavu ana barua ya ombaomba kutoka kwa RC, DC, RAS au DAC, hata kama anasoma shule ya kata ya elfu 20 ambayo haifikii hata bajeti ya chai ya RC kwa siku moja anayetumia zaidi ya laki mbili za walipa kodi kunywa chai na wapambe wake wilayani. Ufedhuli mtupu huu.
 
Huu ni ubaguzi wa hali ya juu sana. Yaani kumpa barua ya kum-declare ombaomba ndicho walichoweza kumsadia? Huu mtindo wa kuwapa walemavu barua za kuwa ombaomba inabidi utokomezwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom