Kwanini tunasifia vyakula vya asili na kuziponda pombe za asili?

Mkuu mbona watu siku hizi tumerudi kwenye pombe za asili, kipindi hiki cha mpito tunapiga chimpumu gizani afu tunaingia bar kuagiza chupa moja inakaa masaa matano. Hali mbaya mzee, hata banana nasikia zinapigwa sana. Sema nani wa kunywa hadharani? Yani uende bar na mtoto mkali afu uagize banana then apige selfie atupie kwenye mitandao yao ile?hahaha.
 
Dengerua,
Kimpumu,
Pingu,
Wanzuki,
Mtukuru,
ulanzi,
Mnazi
.


.
.
.orodha ni ndeefu! Kama vipi ongezea hapoili tuzitambue kwanza aina hizo za pombe.
 
Hata wazipondi pombe za asili zinapendwa sana tatizo lipo Hivi bei za pombe zinatofautisha wanywaji especially mini kwahiyo Kama unabar Nzuri ukiweka chibuku utashangaa watu watakuja na ndala makelele wale wanaokunywa bia watakwazika ila Kwa vijijini mambo ni shwari tu.

Saiv wanapigania pombe za asili ziwe na standard kabisa mfano chibuku and chibuku super ni pombe za asili zenye standard

Mwanza kuna zagamba inastandard kwahiyo kila Mkoa na pombe ya asili iliyopo watahakikisha standards zinapatikana
 
Back
Top Bottom