Kwanini tunakwenda shule? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini tunakwenda shule?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, Jan 30, 2010.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( Kutoka Kwanzajamii.com)

  30 January 2010 3 views No Comment
  Nikiwa Mwanza hivi karibuni nilimwona mtoto huyo aliyelala na kushika tama kila asubuhi niliyokuwa nikifanya jogging. Nilipokwenda nikikimbia, nilimpita akiwa bado hajaamka, na niliporudi kukimbia nilimpita akiwa hajaamka. Kwake ilikuwa ni mapema mno, saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Lakini picha ya mtoto huyo inatukumbusha changamoto za kijamii zinazotukabili. Huko nyuma niliainisha mlango wa kwanza ambao mwanadamu anautumia katika kupata maarifa; Fronesis, ni neno la Kigiriki likiwa na maana ya maarifa yatokanayo na uzoefu.
  Picha ya mtoto huyo wa mitaani inatupelekea kwenda kuufungua mlango wa pili wa maarifa; episteme, ( Epistemolojia) nalo ni neno la Kigiriki likiwa na maana ya maarifa tuyapatao kutokana na elimu ya darasani, shuleni. Na tujiulize basi; kwanini tunakwenda shule?
  Wengi wetu yaelekea hata elimu tuliyoipata kutoka vyuo vikuu imetusaidia tu kupunguza ujinga, si kufuta ujinga. Na kuna wengine, pamoja na kujigamba na digrii zao, bado wanatembea wakiwa wamejifunika ‘ Vilemba Vya Ujinga’. Hata kama ni viongozi, kwao wao uongozi una maana moja kuu; vyeo vyao, U-Bwana Mkubwa, U-Heshimiwa. Hawakuutafuta uongozi ili wasaidie kuwaongoza watu wao kupata nafuu ya maisha. Wamevitafuta vyeo ili nao washiriki ‘ kuwanyanyasa’ watu hao, kwa rushwa zao, kwa matumizi mabaya ya vyeo vyao na maovu mengine, na zaidi linalowasukuma kuwatendea ‘ maovu’ watu wao ni UBINAFSI. Naam. Ubinfasi ndio shina la maovu yote. Mtoto huyo hapo juu pichani na wengine wengi ni majeruhi ya jamii ambayo baadhi ya iliyowapa dhamana za uongozi wanaendekeza ubinafsi. Leo tuna mifano ya wanaojiita ‘ viongozi’ wanapoona fahari kuishi kwenye mahekalu ya thamani ya mabilioni ya shilingi ilihali wananchi hao kwa mamilioni hawana hakika ya mlo mmoja kwa siku. Mtu aliyekwenda shule na hata kujiita msomi anatazamiwa kuwa na ‘ aibu ya kisomi’. Kama mtu huyu anapotenda maovu, na hata akasimama hadharani na kutetea maovu yake, basi, unajiuliza; kwanini tunakwenda shule?
  Born Again Pagan ( BAP) alipata kuandika, kuwa kashfa ya Richmond ni matokeo ya Unyonge wa Mtanzania. Naikubali hoja ya BAP. Hoja hiyo inapata mshiko kutokana na alichopata kusema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere miaka mingi iliyopita.Ni kabla ya wengi wetu hatujazaliwa. Naweza kuendelea kuandika kwa kirefu juu ya tafakari yangu hii, nitakuchosha. Lakini ngoja nihitimishe kwa kuiongezea nguvu hoja ya BAP kwa kuwadokeza alichosema Mwalimu Nyerere, Mei 30, mwaka 1969. Mwalimu aliongea na Walimu na Vijana wa TANU pale ukumbi wa Diamond. Alisema; ” Ukichukua Azimio La Arusha, utaona kuwa sentesi yake ya maana kupita zote ni ile inayosema; ” Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha; na ni unyonge wetu ndio uliotufanya tukaonewa, tukanyonywa, tukapuuzwa. Sasa ni lazima tufanye mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge wetu, ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena”. ( Julius Nyerere, Diamond Jubilee, Mei, 30, 1969). Naendelea kutafakari, nawe tafakari pia!
  CHANZO: kwanzajamii.com
   
 2. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2010
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hili ni swali pana sana.
  Hata hivyo jamii yetu inachukulia kwenda shule kama kama daraja la kupata kazi serikalini na mashirika makubwa yalipayo vema wafanya kazi wake. Kwenda shule siyo tena nyenzo ya kufuta ujinga,bali nyenzo ya kushibibisha matumbo ya wasomi na familia zao,ndiyo maana ni rahisi kwa msomi kulipa ada ya chekechekea milion 1 wakati jirani yake akikosa sh elf 20 ya kulipia ada mtoto wake katika sekondari ya kata. Wasomi ndoyo waliotufiksha hapa,wagawana amali zetu,wametudunisha na kutuuza kwa wageni kwa kutumia vyeti vyao,stashahada zao na shahada zao,hku wa kitupoza Tanzania yenye neema inawezekana.

  Wasomi wetu hawatraki utaalamu wao utumike,wakiona mapato yao hayatoshi kwnye taaluma zao hukimbilia siasa,huko kunaaminika kuweko na mapato makubwa na heshima kubwa.

  KUNA RAHA GANI KUWA TAJIRI KATIKATI YA MASKINI,AU MWELEVU KATIKATI YA YA WAJINGA?.
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ” Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha; na ni unyonge wetu ndio uliotufanya tukaonewa, tukanyonywa, tukapuuzwa. Sasa ni lazima tufanye mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge wetu, ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena”. ( Julius Nyerere, Diamond Jubilee, Mei, 30, 1969).
  .Mmm,maneno mazuri kwelikweli,laiti yangetekelezeka.The truth is haya ni maneno matupu,yasiyotekelezeka.Bado tunaendelea kuonewa na infact hali ni mbaya zaidi kuliko hata pale Nyerere aliposema maneno hayo pale Diamond Jubilee. Tuwanyonge zaidi,tunaonewa zaidi, tunanyonywa zidi na tunapuuzwa zaidi.Hakuna kabisa uwezekano wa hali hii kuwa bora hasa kwa vile tumekubali adui zetu,tena wauaji wetu, wawe ndio mashoga zetu wa kupakua na kula.Mbaya sana.Sikio la kufa hali sikii dawa!Ngoja tujiishie tu,potelea mbali.

  Na kuhusu swali lako la kwanini twende shule,akili timamu niliyo nayo ina niambia kwamba hatukuhitaji kwenda shule.Wapuuzi hawa wali tu-brainwash na hatimaye tukaamini kwamba kwenda shule ndio uungwana, kumbe sababu ilikuwa tupate 'what we wrongly call education' na hatimaye tuwasaidie ku-'advance their foolish agendas against us'.Inasikitisha sana.'We would be better off without this non-sense called education!'

  Sijui kama utanielewa!The conspiracy is too monstrous to be appreciated by a common mind.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwani hujui tunakwenda shule ili tukombe pesa za wajinga walipa kodi? Angalia JK, Chenge ( Mzee vijisenti), RA (ingawa shule yake siijui) Mramba, BWM, Manji teh teh shule dunia bwana mtakoma mwaka huu. Na hawa lazima waendelee kuwaalika mafisadi kutoka katika kila pembe ya dunia kuwasulubisha wa bongo maana mlikuwa mnajifanya kichwa maji sana wakati wa mchonga.
   
Loading...