Kwanini tunahitaji Umoja?

Kwanini tunahitaji Umoja?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
Katika historia ya vita mbalimbali zilizowahi kupiganwa Duniani, basi kila vita kati ya hizo walioshindwa sababu mojawapo iliyowakosesha ushindi ni kukosa umoja. Hata timu ya mpira ikikosa umoja baina ya wachezaji uwanjani basi haiwezi kufanikiwa.kupata ushindi.

Vilevile hata familia isiyo na umoja ni vigumu sana kujengeka na kuwa familia imara na iliyo bora ndio maana hata vitabu vya dini vinahimiza upendo ili kuchochea umoja.

Kwanini umoja ni muhimu katika maisha ya mwanadamu?

Jibu rahisi umoja ndio uleta nguvu katika kulifanya jambo lolote liwezekane hata kama lilikuwa gumu.

Ile simulizi ya sisimizi wamtoa nyoka pangoni inasadifu umuhimu wa umoja katika maisha ya kila Siku. Jamii yenye umoja inaweza kukubaliana kuwa na mazingira safi na kuyashinda magonjwa.

Jamii inaweza kukubaliana kuwa na ulinzi na kuwashinda maadui wanao izunguka.

Wahehe wa Mtwa Mkwawa miaka iliyopita walimpiga mjerumani na jeuri yake yote ya kivita sio kwamba walikua na silaha bora hapana ni nguvu ya umoja. Umoja unaifanya jamii iaminike, iogopwe na kuaminika.

Je, nani asiyeguswa na ile vita ya Vietnam na Marekani miaka ya 1950's? Marekani alichakazwa vibaya mpaka kuwaza kurudi nyumbani hii yote ilikuwa mbinu ya umoja wa Wavietnam katika kumpiga adui licha ya uchanga wa nchi yao.

Simulizi ya umoja inagusa kila kona ya maisha hata kiimanj, unaweza kujiuliza ni mbinu gani ilitumika kuijenga himaya ya Roma? Jibu fupi ni uimara na umoja wa Jeshi la Warumi katika kuijenga jamii yao hadi ikawa kubwa zaidi duniani.

"Umoja ni nguvu," kauli pekee inayowapa nguvu wanafunzi kukataa uonevu wa waalimu mashuleni juu ya haki zao kwani wanagoma kwa pamoja haki hupatikana. Hakuna lenye haki lisilo wezekana mbele ya umoja wa jamii au watu.

"Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu," kauli hii inatosha kutamatisha juu ya mahubiri haya juu ya umuhimu wa umoja.

Peter Mwaihola


1671078005946.jpg
 
Wale tunaotaka katiba mpya, tuliochoshwa na manyanyaso tokea polisi, takukuru, uhamiaji, tra, Sumatra, nk.

Wale wanafunzi wa law school, wenye kutaka mikutano ya siasa na wote msumbukao na dhuluma mbalimbali za wachache, kuna wito wenu huku.
 
Back
Top Bottom