kitendaguro kwetu
Member
- Oct 8, 2017
- 28
- 117
Ni mafanikio gani tunayodhani tumepata kwenye sekta ya madini hadi tutake kusifiwa?
Moja ya agenda kubwa ya Taifa na ambayo itaondoa maswali mitaani juu ya rasilimali zetu ni UWAZI KATIKA MIKATABA
Nakumbuka hao tunaowahita wawekezaji, wakati wanakuja kuwekeza tulijifungia nao tukaanguka sahihi na kuja kuutangazia umma kwa mbwembwe kuwa Tanzania sasa inaaminika Duniani ndiyo maana wawekezaji wakubwa wa madini wamejitokeza kuwekeza.
Tukaenda Bungeni tukapaza sauti na kuwakemea kwa nguvu kubwa wale waliotuambia tuanibiwa huku tukiwaita wasaliti na wapotoshaji wakubwa ambao hawana tone la uzalendo ndani yao.
Baada ya muda kupita yale waliokuwa wanayapigia kelele na mkatuaminisha ninyi ni wazalendo mnakuja tena adharani na kukiri kuwa Taifa lilikuwa linaibiwa na wezi wa rasilimali zetu ni hao hao wawekezaji.
Kwa kuwa ajenda yetu kama taifa ni uwazi wa mikataba na umilikishaji wa rasilimali zetu ,wakosoaji wakarudi na kuwapa mbinu za kufuata ili tushinde hii vita kwani vita hii si ya chama kimoja bali ni vita ya kitaifa.Waliposimama kuwakosoa mkawaita tena wasaliti na kwamba hawana uzalendo nao wakaendelea na wanaendelee kukosoa kwa sababu huo ni wajibu wao kukosoa hadi siku ya mwisho.
Baada ya kuona ukosoaji umepamba moto mkawaita tena wawekezeja mkakaa nao kwa miezi mitatu ndani mkijadiliana, naamini wakati mnajadilia mliweka mezani mikataba yenu yote na mkapitia kipengele kwa kipengele na wakati huo hamkuifanya siri miongoni mwenu bali mliweka mambo wazi na mkafikia muafaka kwa baadhi ya mambo ambayo ninyi mliona ndiyo yenye tija kwa taifa.
Nilitegemea pamoja na mazungumzo kukamilika moja ya kitu ambacho mngekuja nacho mbele ya wananchi na kuweka wazi ni taarifa yenye ufafanuzi wa kina wa kila kitu mlichojadili huku mkionyesha kuwa mmeridhiana katika mambo gani, hamkuridhiana katika mambo gani na nini kilichobaki kwa ajili ya muendelezo wa majadiliano...Lakini kilichofanyika ni kutoa summary tu ya kile mnachoamini kuwa kina manufaa kwa jamii na watanzania.
Lile joka lililolitesa taifa kwa muda mrefu ambalo ni uwazi wa namna rasilimali zetu zinavyotumiwa na wawekezaji bado kwenu haikuwa ajenda na hata yale mliyojadiliana hakuna aliyethubuti kuyaweka katika tovuti ya serikali ili kila anayetaka kuhoji au kusoma asome kuona riport nzima inasemaje?
Leo hii wanaopongeza ni wachache na wenye nguvu katika mjadala ni wale wakosoaji, kwanini wakosoaji wamepata nguvu? Ni kwa sababu wale wanaopenda kutoa pongezi hawana document ya kusimamia katika kutetea kile kilichofanywa na serikali.
Lakini pia, Prof.Kabudi hana sababu ya kuongeza au kutoa ufafanuzi mitandaoni pale ambapo taarifa kamili yenye kusheeni facts na isiyo acha maswali itawekwa wazi kwa wananchi wasome , Leo analazimika kutoa ufafanuzi kwasababu taarifa aliyosoma kwa mhe.Rais haipo popote ambapo wananchi wakiwemo wasomi wenzake wakaweza kuipitia.
Natambua yapo mambo ya ndani ambayo serikali kwa kulinda maslahi ya uwekezaji na pia kulinda maslahi mapana kwa Taifa siyo sahihi kuyaweka hadharani lakini kwa yale yaliyosomwa kwa watanzania naamini yanapaswa kuwekwa kwa upana wake katika mitandao na vyombo vya habari tuelewe nia njema ya nchi yetu katika vita.
Hadi sasa hakuna anayejua nafasi ya ACCACIA katika majadiliano yaliyopita, na ndiyo maana maandishi yao kwenye mitandao kwamba hawaafikiani moja kwa moja na kile kilichokubaliwa na serikali na Barick yamepewa ushabiki mkubwa sana Duniani kote na kuharibu yale yote mazuri yaliyojadiliwa kwa miezi mitatu.
Accacia wanapata wapi nguvu ya kupingana hadharani na serikali yetu hasa pale ambapo kampuni mama imetamka mbele ya watanzania kwamba majadiliano yameenda vizuri?Ni wapi tunapoweza kupata ufafanuzi wa kina juu ya nafasi ya accacia katika biashara hii ya madini?Kwanini ufafanuzi juu ya hoja za accacia zisitolewe sasa na serikali?
Ukitafakari utagundua bado serikali haijakubali kuwa wazi katika suala zima LA rasilimali za nchi na ndiyo maana wakosoaji wanapata nguvu kubwa na wana hoja nzito sana masikioni mwetu kuliko serikali.
Mijadala ya rasilimali za nchi Mara nyingi uzimika pale upande mmoja unapotaka kuodhi mjadala husika na kutaka watu waamini nia njema waliyonayo, lakini kwa miongo sasa tumekwama kwa sababu ya kundi LA serikali kumiliki mijadala na kuwaaminisha wananchi kuwa wakosoaji siyo kitu na wala siyo wazalendo ila Mimi naamini serikali isiporuhusu mjadala wa wazi huku ikiweka kila kitu wazi basi wakosoaji siku zote wataibuka washindi.
Njia pekee ya kwenda mbele kama taifa ni kumbeba kila mmoja wetu katika safari ya maendeleo ili siku tukizama asitokee wakusema mlinipuuza.
Bora ukatae kusifiwa kuliko kusifiwa kwa muda mfupi na baadaye kubwezwa na kutukanwa na wale waliokuwa wanakusifia.