Wakati kuna pesa kubwa zaidi zimeibiwa?
Au mshasahau zile TRILIONI 3 za JWTZ? Mbona hakuna anayeuliza au kupiga kelele kuhusu wizi wa SYMBION, BOMBA LA GESI MTWARA, UPANUZI WA BANDARI etc?
Au ndio double standards?
Nchi hii haina collective responsibility na sidhani kama kuna mtu atawajibishwa au atawajibika so lets stop hii charade ya kitoto wakati tunajua mkuu wa nchi hawezi na hananubavu wa kumwadhibisha mtu wakato.kabakisha kiezi 12 aende kupumzika na kufuga ngombe zake kule Yamousskuro
Kwa hiyo wewe unaridhika vigogo wachache walioko madarakani, kujichotea shilingi bilioni 321?!
Wewe utakuwa hujitambui, kwani hujui kuwa kuna connection, kati ya wewe kulipa bei ya umeme ya 'kuruka' kwa bei ya shilingi 323 kwa uniti na wizi huo?
Kwani hujasikia kuwa kwenye ripoti hiyo imeelezwa kuwa, pesa hiyo iliyoibwa ni ya umma, tofauti na tulivyokuwa tunajulishwa na kina Pinda, Lukuvi, Muhongo na Lukuvi?
Imelezwa pia kuwa hizo bilioni 321, zilizochotwa na hao watu wachache, zilipaswa kurejeshwa TANESCO, kwa kuwa ilikuwa overpayment ya capacity charges.
Kwa hiyo hapo pia hujabaini kuwa huyo singa singa wa IPTL na swaiba wake Rugemalira ( mgawaji pesa kama njugu) kutokana na kuwatoza viwango vya juu vya bei ya umeme TANESCO, ndiko kulikosababisha nasi tutozwe bei ya umeme ya kuruka?
Wewe uliyeleta hii post, unaweza kuwa one of beneficiaries wa kuingiziwa kwenye akaunti yako, yale mabilioni yaliyokuwa yanagawiwa kiholela na Rugemalira.
Kitu kimoja mtambue nyiye vigogo ambao mmezoea kuifanya TZ kuwa shamba la bibi kuwa na sisi watanzania tunawaeleza kuwa, mmetuibia kiasi cha kutosha, mmetutesa kiasi cha kutosha, na unyonge wetu ndiyo uliotufanya nyiye watawala wetu mtuibie mnavyotaka, sasa tushasema IMETOSHA!