Kwanini Tanzania sio Taifa kubwa?

Willy Johnson

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
316
156
Habari wanajf.

Leo nimependa kutoa uzi huu kwa wanajf kwa kutaka kujua au tueleweshane sababu za nchi yetu kushindwa kuwa taifa kubwa kama mataifa mengine yanayosifika duniani.

Pia katika mchango wako nitaomba tuweke pembeni uchama, udini, ukabila, ukanda hii iwe kwa maslai ya nchi yetu. Mchango wako huenda pia ukawa mkombozi wa taifa letu kwa kuwa humu kuna makada wa aina mbalimbali. Naomba niwasilishe kwenu mjadala huu.
 
Kuhusu maendeleo huwezi kuacha kuzungumzia siasa na vyama.

Sababu kubwa ni kwamba tunatawaliwa na chama kinachotoa ahadi hewa.

Viwanda hatuvioni maneno tu huku thamani ya shilingi inashuka.
 
hamna uzalendo
Nimeipata point yako kwaiyo uzalendo kwa maana ile hali ya watanzania kuipenda nchi yao kwa dhati haipo. Pia tukidumisha hii hali inamaanisha hata sisi wenyewe kwa wenyewe tutapendana bila kujali kabila, dini, au chama fulani kwasababu uzalendo hujengwa na watu na watu hujenga taifa. Kwaiyo hata yule anaeshabikia chama fulani hawezi kuwa na watu wengi kama hatakuwa mzalendo maanake yeye atakuwa anaangalia maslai ya chama chake badala kuangalia maslai ya taifa au watanzania wanataka nini?
hamna uzalendo
 
Unazungumzia ukubwa gani ukubwa wa eneo ? ukubwa wa kiuchumi au nguvu za kijeshi ,ukubwa wa kuheshimika mbele ya mataifa mngine weka hoja yako vizuri
 
Unazungumzia ukubwa gani ukubwa wa eneo ? ukubwa wa kiuchumi au nguvu za kijeshi ,ukubwa wa kuheshimika mbele ya mataifa mngine weka hoja yako vizuri
Ukubwa kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa hata kijeshi.
 
Back
Top Bottom