Kwanini taasisi za kidini zisilipe kodi?

Maziku-Winston Smith

JF-Expert Member
May 17, 2015
296
167
Kwa nini makanisa, misikiti pamoja na taasisi nyingine za kidini huwa hazilipi kodi?

Mbona taasisi nyingine kama vilabu vya mpira na taasisi zisizo za kiserikali zinalipa kodi
 
Nilikuwa nimesahau kidogo . Swali linafaa kuwa hivi; Kwa nini taasisi za kidini Kama vile makanisa na misikiti n.k huwa hazilipi kodi?
 
Kabla hujaandika thread juu ya jambo fulani jifunze kutafuta uelewa wa jambo husika (kodi ), pili fanya utafiti hii itakusaidia kujenga hoja halafu uje uulize. Tatu usipende kufikiri kwa kutegemea mawazo ya wengine maana umeleta swali ambalo kama ungetumia muda wako kufikiri ungejijibu. Unajua maana ya kodi, aina, dhumuni na inakuwaje mpaka mtu analipa kodi? Nenda katafute maana uje huku utueleze kwanini hao ukiowataja hawalipi kodi. Kwa uelewa wako mdogo unafikiri ni Makanisa pekee ndio hawalipi kodi! Sio kila kitu cha kuuliza jf rafiki, hizi assignment za chuo zikitegemea jf zitaua ubunifu na uwezo wa kufikiri na impact yake itaonekana baada ya kumaliza chuo. Tafakari na chukua hatua.
 
Kwa nini makanisa, misikiti pamoja na taasisi nyingine za kidini huwa hazilipi kodi?

Mbona taasisi nyingine kama vilabu vya mpira na taasisi zisizo za kiserikali zinalipa kodi

Ni kwa sababu kazi zao ni kuhudumia jamii ambayo ndiyo kazi ya kodi tunazolipa, hivyo kama wakilipa watakuwa kama wanafanya kazi mara mbili, na ndiyo maana ni lazima wathibitishe kwa yale yote wanayosamehewa kodi ni kwa ajili ya jamii, na siyo wao tu hata wewe kama ukianzisha mradi ambao unaweza kuthibitisha kwamba lengo lako ni kuhudmia jamii hautalipa kodi pia!
 
Kabla hujaandika thread juu ya jambo fulani jifunze kutafuta uelewa wa jambo husika (kodi ), pili fanya utafiti hii itakusaidia kujenga hoja halafu uje uulize. Tatu usipende kufikiri kwa kutegemea mawazo ya wengine maana umeleta swali ambalo kama ungetumia muda wako kufikiri ungejijibu. Unajua maana ya kodi, aina, dhumuni na inakuwaje mpaka mtu analipa kodi? Nenda katafute maana uje huku utueleze kwanini hao ukiowataja hawalipi kodi. Kwa uelewa wako mdogo unafikiri ni Makanisa pekee ndio hawalipi kodi! Sio kila kitu cha kuuliza jf rafiki, hizi assignment za chuo zikitegemea jf zitaua ubunifu na uwezo wa kufikiri na impact yake itaonekana baada ya kumaliza chuo. Tafakari na chukua hatua.
Nimeuliza hivi kwa sababu taasisi nyingi za kidini siku hizi zimevamiwa na matapeli ambao wamezigeuza kuwa kama biashara ambazo zimewawezesha kujilimbikizia kiasi kikubwa cha pesa
 
Back
Top Bottom