Kwanini taarifa za uwepo wa mamilioni ya manispaa ya kukopesha wanawake na vijana zilifichwa ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,782
239,459
Kabla ya viongozi wapya wa jiji la DSM ( UKAWA ) kutwaa madaraka , taarifa za kuwepo pesa nyingi zinazotengwa kila mwaka na manispaa zetu ili kukopesha wanawake na vijana zilikuwa siri .

Taarifa hii imebainika baada ya wakazi wa manispaa ya Ilala ( kata ya Tabata ) kupigwa na butwaa baada ya kupata taarifa kutoka kwa diwani wao uwapo wa zaidi ya sh milioni 650 zinazotolewa kila mwaka na manispaa ili kuwakopesha akina mama na vijana .

swali langu kwa viongozi wa ccm walioondolewa madarakani baada ya nguvu ya umma kufanya kazi yake octoba 25 , ni nani aliyekuwa anakopeshwa hela hizi kwa miaka yote tangu zianze kuidhinishwa ? na kwanini yeye akopeshwe kwa siri ? na je amelipa marejesho kama inayotakiwa ?

kama kuna mwenye taarifa zaidi na hela hizi juu ya wananchi kukopeshwa au kufahamu uwepo wake , na kama kweli manispaa ziliweka wazi uwepo wa mamilioni haya ajitokeze .

Shukurani sana kwa viongozi wa UKAWA kwa kututoa matongotongo ,

Nakala imfikie Mh Jerry Silaa , Meya mstaafu wa Ilala .
 
Sio jiji la Dar es Salaam tu bali kwenye Halmashauri zote za Wilaya zilizopo chini ya uongozi wa CCM. Muone jinsi chama hiki kinavyofisidi nchi na mtu akikikosoa tu anaambiwa anavuruga amani ya nchi!
 
Sio jiji la Dar es Salaam tu bali kwenye Halmashauri zote za Wilaya zilizopo chini ya uongozi wa CCM. Muone jinsi chama hiki kinavyofisidi nchi na mtu akikikosoa tu anaambiwa anavuruga amani ya nchi!
ashukuriwe Mungu kwa wema wake wa kuileta UKAWA .
 
hii nchi imeoza kuliko unavyodhani .
mkuu hapa naona ndio mwanzo je wakianza kupitia ile kitu iliyosababisha wabunge wa dar wakatukanwa kwa kuambiwa kwamba wanafikiri kwa kutumia sijui nini vile,
nisimalizie nisije kuambiwa nimetukana mimi.

hapo ndio patamu sijui itakuwaje?
 
kila kitu kitafahamika tu .
 
Taarifa zote zitakazohusu nafuu zote za wananchi zinazotolewa na manispaa zitawekwa hadharani .
 
Mkuu pesa zilikuwa haziliwi kumbuka hiyo ni % fulani tu ya mapato hivyo tulikuwa tunapeleka kufanya shughuli nyingine za maendeleo kwa manufaa ya wananchi hao hao.
 
Mkuu pesa zilikuwa haziliwi kumbuka hiyo ni % fulani tu ya mapato hivyo tulikuwa tunapeleka kufanya shughuli nyingine za maendeleo kwa manufaa ya wananchi hao hao.
kama kuna ushahidi wowote hapa ni bora ukituwekea kama uthibitisho wa andiko lako .
 
Aisee kuna mwaka fulani wakati tumemaliza chuo tulijikoki vijana kama 11 hivi tuakaenda halmashauri ya Ilala kuomba pesa za kilimo, tuliyoyaambulia huko ni siri yetu tu.

Tulikuwa na ardhi kama hekari 70 hivi huko Rufiji maeneo ya Chumbi na kila kitu tuliishia kuzunguka maofisini tu, mwisho wa siku tulipohoji hoji tukaishia kuchimbwa mkwara mzito na "wakubwa"siwezi sahau
 
poleni sana .
 
Back
Top Bottom