Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,205
Salaam Wakuu.
Kwanza Natangulia kwa kusema, Natambua kuwa vyombo vya habari ndivyo vyenye Jukumu kubwa sana la kuhabarisha Wananchi juu ya masuala mengi. Vyombo hivi ndivyo hufikisha taarifa ikusuadivyo kufika katika sehemu/hadhira tarajiwa.
Lakini, naomba kuuliza. Kwa nini taarifa kutoka Serikalini haswa Ikulu pamoja na Wizara zake huelekezwa moja kwa moja kwenye Vyombo vya Habari? Naaminisha kuwa, kila barua kutoka IKULU huelekeza taarifa kwa vyombo vya habari badala ya kuelekezwa moja kwa moja kwa Wananchi wote.
"TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI"
Hivyo ndivyo inavyosomeka juu kabisa ya Barua kutoka Ikulu au Wizara za Serikali. Kwa nini Serikali isielekeze Barua zote kwa wananchi kwa Ujumla? Kwa tafsiri halisi, taarifa kwa vyombo vya habari ni taarifa itolewayo mahususi kwa vyombo tajwa. Je, siku vyombo vya habari vikashindwa kufikisha taarifa kwa Wananchi kwa kususa (kupuuzia) au kusahau, Je watoa taarifa Watakuwa na Uhakika gani kuwa taarifa imefika?
Madhalani, huenda hata taarifa yenyewe ikawekwa katika tovuti ya Ikulu au wizara na Mwananchi wa kawaida akafika na kuisoma lakini kuangalia kwenye kichwa tajwa imeelekezwa kwenye Vyombo vya habari, je hata huyo Mwananchi ni Chombo cha Habari ikiwa hana uhusiano wowote na vyombo tajwa?
Cha kushangaza, haielekezi kuwa taarifa husika itangazwe kwa Wananchi.
Kwa nini Serikali isielekeze taarifa zote kwa Wananchi kupitia vyombo vya Habari kama Television, Redio, magazeti, blogs na aina nyinginezo?
Natoa Wito kwa Serikali na taasisi zake ibadilishe zibadilishwe vichwa vya taarifa zao na badala yake zielekezwe moja kwa moja kwa Wananchi wote. Vyombo vya habari vitoe taarifa hiyo kama ambavyo imekua ikivitoa hapo awali.
Matukio ya kuzungumza moja kwa moja na Vyombo hivyo yaani Press conference, ndizo zinafaa kutajwa kama taarifa kwa Vyombo vya habari. Mfano, mtangazaji atasema "Akizungumza na Vyombo vya habari katika Ofisi za Wizara ya Elimu, Mh Joyce Ndalichako amesisitiza kuwa ............ "
Nawasilisha.
Una maoni gani Juu ya hili?