Kwanini sitaki muungano uvunjike...

Amboni

Member
Nov 27, 2011
6
0
Habari wana JF !

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu muungano hivi karibuni.
wengine wanataka serekali moja,wengine wanataka serikali tatu na wengine wanataka uvunjwe kabisa.

Binafsi sitaki muungano uvunjike kwa sababu zifuatazo:

#1: Baba yangu ni Myeramba na Mama yangu ni Mpemba { Hii ni sababu Binafsi }.

muungano ukivunjika ntahitaji visa kumtembelea bibi yangu.

#2: Huwezi kuwa na nchi kilometa chache kutoka DAR ES SALAAM {sababu za kiusalama }.

Nadhani hii ndio sababu kubwa inayofanya TANGANYIKA kudumisha muungano kwa nguvu zote.

#3: Nataka kuoa binti wa kipemba { Hii ni sababu Binafsi }.

muungano ukivunjika mke wangu atakuwa mgeni hapa nchini.

Hizi ndio sababu zangu, naomba mnisahihishe kama nimekosea lakini msinitukane {Hasa wajomba zangu toka wete }

Shukrani.
 
hapa ulipo unaweza kumuoa mzambia na ukaenda zambia japo hatujaungana kwa hiyo usihofu bila muungano marriage itakuwa palepale
 
hapa ulipo unaweza kumuoa mzambia na ukaenda zambia japo hatujaungana kwa hiyo usihofu bila muungano marriage itakuwa palepale

Naelewa kuwa unaweza kuoa mahali popote pale duniani--
Nisochotaka mimi ni ule usumbufu wa kulipia kibali cha kuishi nchini na mambo mengine kibao,nadhani umenielewa.
 
Naelewa kuwa unaweza kuoa mahali popote pale duniani--
Nisochotaka mimi ni ule usumbufu wa kulipia kibali cha kuishi nchini na mambo mengine kibao,nadhani umenielewa.

Utakwa unasaidi mapato ya nchi za wakwe zako huoni huo ni uzalendo zaidi kuliko bure?? wewe mwanaume vipi
 
Utakwa unasaidi mapato ya nchi za wakwe zako huoni huo ni uzalendo zaidi kuliko bure?? wewe mwanaume vipi
Sasa ntasaidia vipi mapato ya nchi za wakwe zangu ?...mapato yote si yataingia katika serikali ya Tanzania ?
 
Sasa ntasaidia vipi mapato ya nchi za wakwe zangu ?...mapato yote si yataingia katika serikali ya Tanzania ?

Ukiende kutembelea kwa wakwe utatakiwa kulipia viza (mfano pemba) ubalozi wa zenj watapata fedha acha uchoyo mkwe tupe hizo hela za Tanganyika..lol
 
Ni muhimu muungano wa serikali tatu maana kila nchi itakuwa huru kujiendesha kwa mambo yasiyo ya muungano.Maana sasa kuna hisia kila upande kudai inanyonywa na upande mwingine.
 
Habari wana JF ! Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu muungano hivi karibuni. wengine wanataka serekali moja,wengine wanataka serikali tatu na wengine wanataka uvunjwe kabisa. Binafsi sitaki muungano uvunjike kwa sababu zifuatazo: #1: Baba yangu ni Myeramba na Mama yangu ni Mpemba { Hii ni sababu Binafsi }. muungano ukivunjika ntahitaji visa kumtembelea bibi yangu. #2: Huwezi kuwa na nchi kilometa chache kutoka DAR ES SALAAM {sababu za kiusalama }. Nadhani hii ndio sababu kubwa inayofanya TANGANYIKA kudumisha muungano kwa nguvu zote. #3: Nataka kuoa binti wa kipemba { Hii ni sababu Binafsi }. muungano ukivunjika mke wangu atakuwa mgeni hapa nchini. Hizi ndio sababu zangu, naomba mnisahihishe kama nimekosea lakini msinitukane {Hasa wajomba zangu toka wete } Shukrani.
Ndio Ahmad Rashid kakutuma haya...?
 
Ahmadi Rashid anaingiaje hapa ? Nimetoa sababu zangu tatu hapo juu ...jaribu kuzipa changamoto hizo sababu. nje ya hapo utakuwa unataka kuleta malumbano ya CHADEMA na CUF.
 
Watu wa Bara wakitaka kwenda Zanzibar wanasumbuliwa sana, lakini Wazanzibari kuja Bara akaa!
 
Watu wa Bara wakitaka kwenda Zanzibar wanasumbuliwa sana, lakini Wazanzibari kuja Bara akaa!

Lakini nnavyojua mimi ukitaka kwenda Zanzibar unachukua Boat pale Posta au ndege (Kutokea Dar es salaam ).
Usumbufu unaouzungumzia ni upi kati ya huu?

1:Usafiri Mbovu
2:Nauli kubwa
3:Au kama kuna usumbufu mwengine uweke wazi
 
Back
Top Bottom