Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,617
Leo naomba niweke sawa hili kwanini sikuwa Daktari licha ya kwamba nilipata nafasi kutoka kwa rafiki wa karibu wa mjomba na mwishowe nikawa nafanya Utanesco.
Katika uzi wa Safari ya Dar es Salaam nimeelezea nilivyoenda Dar na kufikia kwa mjomba ila mjomba alianza kunichukia kwa sababu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi wake ambaye nilimkuta pale kwake. Kabla sijapata kazi nilianza mahusiano na yule mfanyakazi wa ndani na mjomba akagundua. Kwa vile nilipewa chumba cha nje nilipoanza mahusiano na yule mfanyakazi wa ndani nilimtaka aishi na mimi kama mke na mme pale kwa mjomba na ikawa hivyo.
Mjomba alikuwa anaacha pesa ya kula mchana na usiku nikawa nachukua ile pesa nafanya matumizi mimi na mke wangu, tukanunua jiko letu na mkaa na taratibu tukawa tunajibana muda mwingine hatuli tunanunua chakula cha kutosha tunaweka ndani kwetu, kwa vile mjomba alikuwa akila usiku tu hivyo tuliweza kujibana sana na zile pesa alizokuwa anaacha na tukajikuta tuna akiba kubwa ya chakula na mkaa wa kupikia.
Baada ya muda nikamkataza mke wangu asiwe anafanya kazi mle ndani kwa mjomba na kama atafanya basi mimi ndiye nitampa ruhusa hiyo, mjomba alianza kumuuliza kwanini nyumba siku hizi ni chafu na hufanyi usafi mke wangu alimwambia mjomba kuwa nimekatazwa na mme wangu kufanya kazi humu. Mjomba ni mkali sana aliuliza kwa sauti una mme hapa? Nikaona atampiga mke wangu nikaenda na kumwambia mjomba usije ukajaribu kumgusa huyu mwanamke ambaye naishi naye katika mazingira magumu usiyoyajua, tunajibana sana ili kutengeneza maisha yetu usijaribu chochote kibaya kwake.
Nilikuwa sina kazi wakati huo, basi mjomba akaja mle ndani akakuta tumenunua jiko la mkaa na vyakula mle ndani akagombeza sana ila akasema kwa vile umeoa mfanyakazi wangu basi ondoka naye hapa kwangu sitaki kuwaona kuanzia leo na akatoa vile vitu tulivyonunua nje na kubana mlango kwa kufuli.
Nilikaa nje na mke wangu nisijue cha kufanya ila nilienda kuomba mjomba msamaha na akanifungulia nikalala na mke wangu, zimepita siku kadhaa mjomba alileta mfanyakazi mwingine pale ambaye alikuwa anafanya kazi za ndani na yule mke wangu akaachishwa kazi hata zile pesa za kula akawa hapewi tena, tukaishi kwa tabu sana pale kula ikawa ni kitendawili sana. Siku moja usiku nilienda kwa mjomba nikamwambia mjomba naomba mrudishe mke wangu kazini tunapata maisha magumu kwa sasa ila mjomba alikataa na pasipo mimi kujua akamtorosha mke wangu na akamrudisha kwao. Niliumia kiasi chake ndipo nikaingia kwenye mgogoro kati yangu na yeye.
Sasa ile nafasi ya Udaktari niliyopata akanibania nisiwe daktari alisema nimeonesha sana dharau kwake kwa kuoa nikiwa kwake tena mfanyakazi wake wa ndani. Hivyo akadai nikiwa na kazi nzuri naweza kumdharau sana na hii ikawa sababu ya kutoniunganisha na udaktari hata baada ya nafasi kupatikana.
Hata yule daktari aliyepata nafasi kumbe aliambiwa na mjomba mambo yangu ndiyo maana na yeye akaamua kuniacha asinishike mkono ili nipate kazi ila baada ya kuanza Utanesco na kupata ajali iliyopelekea nirudi kijijini niliondoka na kinyongo dhidi ya mjomba kwani aliniharibia maisha hasa mke wangu akamfukuza kazi, na mimi akaninyima nafasi ya Udaktari.
Baada ya kuanza kilimo na kunufaika alikuja nyumbani na tukapatanishwa kwa sasa tunaongea vizuri ila sio kama zamani na kila mmoja maisha yake yanaenda kwa jasho la nguvu zake.
Sababu kubwa ni hiyo, kwanini sikuwa Daktari licha ya kupata nafasi hiyo.
Sent using Jamii Forums mobile app