Kibundi wa getto
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 455
- 877
Mwaka 2012 nilikua nabet sana, nilikuwa naweka 500 mpaka 1000 kwa siku. Nilikua nabet kipindi cha likizo, kipindi nipo advance, ela ya tution mchikichini kwa mgote ndio nilikua naipunguza ili nibet.
Likizo ya kuingia kidato cha sita, nilikuja na upepo mkali sana. Nilikua nakula 50000 mpaka 100000 kwa siku. Nilibet mpaka rafiki zangu wakahisi natumia ndumba. Uwezi amini mpaka ligi inaisha Kwa Man city kubeba kombe ule msimu nilikua na million 7 benki
Nilishindwa kurudi Shule ili niendelee na masomo Kwa ajili ya kubet, sababu kila nikisema naenda kubet ya mwisho nilikua nakula tu, yani nilinogewa na ushindi mpaka nikaona Shule sio dili tena.
Siku man city anamfunga QPR ndio nilisema sasa basi, sibeti tena ngoja nifanye biashara sababu nilikula million 2 cash, mimi nilikua naweka laki mpaka Laki 5 kwa mkeka mmoja ndio sababu nilikua nashinda ela nyingi.
MAAJABU YA ELA YA KUBET
Nilianza biashara zangu kwa kufungua CD library, play station games, saluni ya kiume na mgahawa wa chakula sababu nilikua na million 9 cash.
Niliajiri vijana, hasa marafiki katika kila idara.Biashara ilikua nzuri mwanzoni lakini tatizo lilikua nidhamu ya fedha kwangu na kwa marafiki
Tatizo la nidhamu ya pesa lilisababishwa na kipindi nabet nilikua natumia pesa bila mahesabu, hata ndugu na jamaa nilikua nawagawia ela mpaka wakawa wanahisi nauza madawa ya kulevya.
Waliendelea kutumia vibaya ela za biashara bila mpangilio na kusababisha biashara kuyumba. Niliumia sana na nikaona bora nirudi kubet tena japo nilikua nimeshastafu kubet
Nilirudi kwa fujo na Niliishia kuliwa, yani sikuwai kula tena mpaka ilifikia hatua hata ela ya kula sina.Niliuza kila kitu mpaka nguo ili nikabet lakini wapi.
Ilibidi nitafute kazi ya kufanya, nikawa namenya viazi kwenye mabanda ya chipsi.
Kwa ufupi, nilipoteza kila kitu. Yani mpaka akili ya utaftaji.
Yote kwa yote, nilirudi kupiga buku japo nilirudia sasaivi nshamaliza chuo na nina kazi.
KITU CHA KUJIFUNZA
Kubet sio mchezo mzuri, unaweza kula ata billion moja lakini hautoridhika. Bado utatamani kuendelea kubet tu ili uwe tajiri, na mwisho wake utaliwa chote ulichoshinda nakubaki kujifariji ipo siku nitakula tena.