Kwanini si vyema kubeza juhudi za mtu

Kwanini si vyema kubeza juhudi za mtu

Shareef Conscious

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
522
Reaction score
343
Kuna tabia imekuwepo kwa miongo kadhaa, pengine hata karne sasa

Nasema karne, japo ki umri ndio kwanza nipo theluthi moja ya karne
Ila nafahamu Tabia za mwanadamu hazibadiliki ingawa mazingira pekee ndio hubadilika

Juhudi chanya ndizo nilizokusudia hapa

Mnamo mwaka 2001 huko malawi, mvulana 1 ktk kijiji 1 akiwa na miaka 14 aliweza kutengeneza kinuu upepo(Windmill) na kufanikiwa kuvuna nishati kupitia Upepo,alijifunza kwa kujisomea ktk maktaba
William kamkwamba akageuka shujaa ktk kijiji chao,miaka kadhaa mbele kisa chake kikasambaa duniani kote
Akapata ufadhili kutoka kwa wahisani na kurejea shule,kwakua aliishia njiani kutokana na changamoto za kifedha(Wazazi wake kutomudu gharama za masomo), japo anakiri watu walimuona kituko/asiyejitambua wakati akifanyia kazi mradi wake

Miaka 14 iliyopita nchini Siera leon,kelvin Doe alitengeneza kituo kidogo cha redio(Radio transmitter, mixer&microphone receiver)
Alitengeneza pia battery kubwa km chanzo cha umeme
Ni mhandisi aliyejifunza mwenyewe
Tukio hili liliwasisimua sana watu, habari yake ilipofika ktk vyombo vikubwa vya habari, alialikwa marekani ktk chuo cha MIT kutoa Lecture, akawa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kualikwa km "VISITING PRACTITIONER"
Na sasa anamiliki kampuni yke ya utengenezaji wa vifaa vya umeme

Hapa nyumbani, kwa siku za hv karibuni
Mwandishi/mtengeneza maudhui/Mchoraji vibonzo Masoud kipanya alifanya uzinduzi wa gari aina ya "KP A72"
Gari isiyotumia mafuta
Ina tembea umbali wa Km60-80 ikichajiwa
Katumia kipindi cha miezi 21 kuikamilisha
Ni mbadala mkubwa wa Mafuta, hasa ktk kipindi hiki ambapo mafuta yamepanda sana bei
Muda wote anafanya mradi huu, hakuweka wazi kabisa(Alifanya siri isipokua kwa watu wake wa karibu)

Naamini Alihofia kubezwa
Kukatishwa tamaa n.k
Walau yeye alikua na msingi wa fedha kidogo kufanikisha ndoto yake

Kuna juhudi nyingi za watu zilizobezwa na kubakia ktk MAKARATASI

Tukibadili Mindset zetu na kuwa sababu ya kuwajengea watoto wetu/ndugu/rafiki/jamaa uthubutu wa kufanikisha miradi yao badala ya kuwabeza tutapiga hatua kubwa sana
Muda mwingi si msaada wa KIPESA

Waweza kua sababu ya kumkutanisha na watu wenye uwezo wa kufanikisha jambo husika, badala ya kumbeza na kumrudisha nyuma zaidi
 
Point, ila pesa mda mwingine ni muhimu kama resource hamna
 
Back
Top Bottom