Kwanini si Kiswahili&English huko BBA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini si Kiswahili&English huko BBA??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rweye, May 27, 2012.

 1. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Ninashindwa kushangaa pindi napoona bigbrother ikiendeshwa huku ikikiuka misingi ya uafrika wake

  Hebu wanajamvi tueleweshane,kama AU ambayo ni platform ya masuala ya Afrika inaweza kudhubutu kuruhusu lugha ya kiswahili kutumiwa kwanini BBA nayo isiwe platform na ikaweza kuruhusu baadhi ya local languages kama kiswahili zikatumika ili kuupromote uafrika wetu?kwanini 90%BBA inapromote umagharibi badala ya uafrika angali ipo kwa ajiri ya Afrika?

  Ama ndo yaleyale weusi kuendelea kujidhalilisha kwa kukumbatia ya wenzetu huku ya kwetu yakizidi kukwama

  Tujadili jamani.
   
 2. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,130
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280


  Mbona unaenda mbali mkuu? We angalia hapa Bongo watangazaji wetu mapaparazzi wanaona ujiko kuongea broken English redioni kupoteza muda wakati 99.9% ya wasikilizaji wao hawajuwi English. Sasa nani mpumbavu hapa? Ukisikia ukoloni mamboleo ndo hivi kaka. Uzezeta mwingine twajitakia wenyewe sie waafrika. Mtu anaitwa Joseph Fimbo yeye atajibatiza na kujiita Joseph Michael (jina la baba yake) ili ajifananishe na mmarekani mweusi. Kwa mtazamo wangu, nafikiri waafrika wanakasumba ya identity!
   
Loading...