comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Rais Dr John pombe Magufuli ilipoingia madarakani iliweka vipaumbele vya kuboresha uchumi kama vile kupunguza na kufuta kodi zenye kero kwa watanzania, kutoa elimu bure, kuboresha miundombinu, kuboresha maslahi ya wafanyakazi nidhamu, kuangalia upya mikataba tata kuboresha huduma za afya, maji na kilimo, lakini ghafla kwa muda wa miaka miwili sasa imekua ikishambulia watumishi wa umma kwa kila sababu sijui sababu hasa imeamua kubadili gia angani,vilevile na kusahau vipaumbele vyenye tija kubwa Mfano mikataba ya ardhi, madini na gesi?