Kwanini serikali inashindwa kupanga jiji la Dar es Salaam?

kamanyora

JF-Expert Member
May 20, 2013
209
133
nimekuwa nikijiuliza kwa nini serikali inashindwa kupima na kupanga mji? nimetembea na kuona baadhi ya maeneo yakiwa bado hayana idadi kubwa ya watu kiasi kwamba kama wangeamua kuyapima na kuyapanga hayo maeneo kwa sasa ingetumika garama ndogo sana,kwa mfano baadhi ya maeneo kama;
Chanika,Pugu,Kitunda,Kivule,Mbezi ndani ndani,Twahangoma.hizi ni baadhi tu

kwa nini yanaendelea kuachwa watu waendelee kujenga bila mpangilio? faida mojawapo ya kuwapimia watu ardhi ni kuongezeka kwa makusanyo ya kodi,wizara ya ardhi ingeangalia hili kwa umakini.
 
usikute kiongozi mzima wa serikali miaka yote ya kuishi dar hajawahi hata mara kufika maeneo hayo... wanadhani dar ni upanga, kisutu, muhimbili, mnazi mmoja na magogoni huku kwengine ni chaka hayo mawazo ya kufanya mipango miji yatatoka wapi!
 
Kuna baadhi ya mawaziri wanachungulia humu. Watampa habari mwenzao muhusika
 
Back
Top Bottom