GE2025 Kwanini Polepole unasema haya sasa hivi?

GE2025 Kwanini Polepole unasema haya sasa hivi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

kinjimbi

Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
20
Reaction score
11
Habari wakuu,

Najaribu kuwaza kwa sauti kwa haya mambo yanayoendelea sasa kutoka kwa bwana Polepole sielewi kwa sababu Polepole wewe ulikuwepo utawala wa JPM, kelele za watu kuuawa zilikuwepo, watu wengi walipotea, vyombo vya habari vilidhibitiwa, hatukusikia ukisema chochote. Waliishi kama malaika waliishi, walioshikama mashetani waliishi na kelele zilikuwepo lakini wewe ulikaa kimya kabisa kabisa.

Sasa inakuaje unaanza kueleza haya ya sasa, kuna nini nyuma yako?

Kama uchaguzi watu hata nyinyi mliiba na mkashinda nchi nzima, kitu amabacho hakikuwezekana kwingine isipokua kwenu tu. Na utawala wenu sikusikia ukipiga kelele wala kusema kitu. Sasa kuna nini hapo? Ebu tumble.

Lengo la msingi la kutoa siri za ndani halikua na wewe ulikua humo na hukusema. Au lengo kuu lako ni lipi? Kusema unatetea nchi hapo kutakua na mashaka kidogo kwani hata wewe ulikua kwenye mfumo. Hapa hakuna jipya.

EBU TUELEZE, tulimuamini kigogo kwa sababu hakua upande wetu, alikuwa upande wetu sisi wanyonge. Hebu nawe tupe sababu za kusema sasa na si awali ulipokuwa madarakani chamani.
 
Hasta angesema kesho, ukweli ungekuwa pale pale, wahuni hamko watu wazuri!

Wapumzike Kwa amani JKN, Maalimu Seif, BWM, JPM, na wahanga wote.
 
Hasta angesema kesho, ukweli ungekuwa pale pale, wahuni hamko watu wazuri!

Wapumzike Kwa amani JKN, Maalimu Seif, BWM, JPM, na wahanga wote.
Yeye atueleze kanyimwa nini huko,hata wezi huanza kugombana kwenye mgao na sio kwingine,ATUAMBIE KANYIMWA NINI HUKO NA WENZIE??
 
Kwani unampangia muda gani aongee nini!?... Wewe mbona tangu aanze kutoa speech zake umeibuka leo kumuuliza!?, ulikuwa unasubiri nini!?.., ukielewa swali nililokuuliza kama una akili tayari utapata jibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom