Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,292
Siyo makusudio yangu kumpigia mtu debe, lakini kwa jinsi ninavyoona hali ya mkoa wa Dar es salaam inavyokwenda kuna uwezekano mkubwa Ndugu Makonda akaelemewa na hili Jiji, na kama hatakuwa makini kusoma hali ya upepo na kubadirika basi bila shaka mabadiriko ya mkuu wa mkoa hayaepukiki. Nasema haya kwa kuzingatia haya yafuatayo:
1. Dar es salaam ni jiji kubwa na ni kioo cha nchi
Hili jiji ni kimbilio la wananchi wakiamini kuwa ni mji wa maziwa na asali, wakiamini kuwa pesa zipo Dar es salaam, Inahitajika mipango endelevu na umakini wa hali ya juu sana kudeal na hili jiji, Hili jiji halihitaji KUENDESHWA KWA MATUKIO au KUTAFUTA UJIKO KWA MAMLAKA ZA UTEUZI, Ukiwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salam unatakiwa uwe na Mipango kabambe, Lakini uwe ni kiongozi mwenye weledi mkubwa kwelikweli kufanikisha mipango yako, ukikosa ajenda basi hili jiji litakushinda.
2: Dar es salaam ni JIji lenye watu wengi wenye weledi
Watu wengi wa Dar es salaam wana elimu ya angalau kidato cha nne kuliko mkoa mwingine wowote, Watu wanajua haki zao, ni vigumu kuwapeleka peleka kwa amri na matamko yasiyozingatia sheria, wanaweza wakakustahi lakini muda wa sanduku la kura ukifika wanaweza kukutaa (mfaano mzuri ni uchaguzi wa mwaka 2015)
3: Dar es salaam ni kitovu cha harakati za mabadiriko
Harakati za uhuru ziliongozwa na Dar, Harakati za Mabadiriko ya Kisiasa miaka ya 1990 zilifanyika Dar, Makao makuu ya vyama vya siasa yapo Dar, Dar ina potential ya kuongoza mabadiriko chanya au hasi kwa nchi nzima, ni mji ambao ni very strong lakini very delicate.
4: Dar ni power Engine ya uchumi wa nchi
Kwa jinsi hili jiji lilivyo, linachangia zaidi ya asilimia 70 ya pato lote la nchi, hyhivyo basi hili ni jiji la kuhandle kwa care sana.
Je ni uongozi gani Unalifaa jiji la Dar es salaam
1. Uongozi wenye kufikiria kutatua matatizo ya Wanachi na siyo kuyahamisha
Kwa mfano kiongozi anayesema hataki mashoga katika mkoa wake wa Dar es salaam, je Tatizo ni Watu waitwao mashoga au Tabia za kishoga?, na Je ukiwafukuza katika mkoa wako wa Dar es salaam ndo utakuwa umetatua tatizo la ushoga nchini?, Je unapoamuru viongozi wa serikali za mitaa wawasake wote wasio na shughuli, je wakishawasaka then what, je kwa kufanya hivyo umetatua tatizo la ajira?
2: Uongozi wenye kutoa taswira ya Utamaduni wa mtanzania
Tulishakubaliana kama taifa kwamba hili ni taifa la kuvumiliana kwa tofauti zetu za kisiasa, maoni na kwamba tutapingana bila kupigana,Hili jiji linahitaji aina ya Mkuu wa wa Mkoa ambaye wananchi na Wageni ambao balozi zao zimejaa tele hapa wakiona jinsi jiji linavyoendeshwa wanasema naam hili ni jiji kuu la Tanzania, watu wanataka waone Utawala wa sheria katika jiji, wanataka waone haki za watu zikiheshimiwa, Watu wanataka waone uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza katika jiji kuu la Tanzania, Kiongozi wa mkoa mwenye kuwatia ndani wapinzani wa kisiasa, kiongozi mwenye kuzuia mikutano ya kisiasa katika Jiji kuu kama hili la Dar es salam huyo hataliweza.
KWA NINI JIJI LINAMUHITAJI MTU AINA YA POLEPOLE
1. Polepole Ana kipawa cha uongozi
Ana nguvu za ushawishi, na uwezo wa kuongoza bila kuhitaji kutumia Ma amri na mabavu, Ukiona kiongozi anategema operesheni za kipolisi na kutishia tishia kila mara kuwaweka ndani huyo ni kiongozi muflisi, nimefuatilia uongozi wa Polepole kwa muda mfupi aliokaa pale mkoani mara kama mkuu wa wilaya, yeye hakuingia katika mtego wa kutishiatishia kuwatia ndani watu, bali alitumia huo muda kuisoma jamii ya pale na wala hakuingia katika mtego wa kutoa matamko ya ajabuajabu
2. PolePole ana uwezo wa kuelezea mipango yake vyema na kujibu hoja kinzani
mara nyingi viongozi ambao hata kama wako sahihi lakini hawewezi kujenga hoja, au viongozi wenye kutaka kufanya kazi ili kumfurahisha bosi badala ya umma mara nyingi hujikuta wanaongoza katika mazingira ya kushindwa kwa sabbu wako out of phase na wateja wao yaani wananchi. Naamini Polepole kwa uwezo wake wa hoja ana uwezo wa kujenga mazingira rafiki sana kwa Vyama vya kisiasa kufanya shughuli zao mkoani Dar bila kulazimika kutumia mabomu ya machozi, maji ya washawasha n.k
3. PolePole ana Exposure na amefanya shughuli kwa maslahi ya vijana kwa muda mrefu
Tatizo kubwa la Jiji la Dar ni Ajira, badala ya kiongozi anayetaka kuhamisha tatizo la ombaomba waende mikoa mingine, Au kuwaska vijana majumbani mwao, Angalau Polepole amefanya shughuli hizi za kuwatafutia fursa vijana kwa muda mrefu, anajua nini maana ya ukosefu wa Ajira, anajua ABC ya tatizo hili. Mimi naamini huyu kijana akiwa mkuu wa Mkoa Anaweza kulisaidia JIji la Dar kuwa na hadhi ya Jiji kisawasawa