Kocha Mwambusi: Kitendo alichokifanya Ntibazonkiza ni furaha ya kufunga goli

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga SC Juma Mwambusi, amesema kwamba kitendo alichokifanya mchezaji wake Saido Ntibazonkiza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania VPL, dhidi ya Gwambina FC ni kutokana na furaha ya kufunga goli kwasababu hakufunga katika mechi mbili zilizopita.

"Ntibazonkiza alikuwa anafurahia kupata goli kwasababu mechi mbili zimempita alitoka bila kufunga goli". Amesema Mwambusi.

Katika ushindi wa Yanga SC wa mabao 3-1 mchezaji Saido Ntibazonkiza aliingia akitokea benchi na kufunga goli la tatu kwa Yanga.

Baada ya kufunga tu akaonyesha ishara ya kuomba atolewe uwanjani, akatoka akaenda zake.

Wachezaji na benchi la ufundi likiongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi pamoja na kujaribu kumrudisha uwanjani lakini alikataa.

Je unadhani nini kimemsibu mchezaji huyu..?!
 
Back
Top Bottom