Daah acha mkuu binafsi nachukiaga sana silali aniHahaha.
Je huoni raha kwamba usiku unakereka kwa sababu mwili wako unakutumikia na kukusafishia uchafu ?
Kama kweli kazi ya mafua ni kuondoa uchafu,je kuna haja ya kuyazuia mafua wakati kuyaacha kwake yanatusaidia kuondoa uchafu ?Mafua husababisha kichwa kuuma, pua(nasal cavity) kuuma na kuwasha, kukosa hamu ya kula, koo kuwasha, kwa nini uvumilie hali hiyo wakati dawa zipo kuponya ugonjwa huo?
Mwili kikawaida huwa una njianzake pekee za kujilinda dhidi ya vitu mbalimbali(defense mechamism).
Mtu akipaliwa na punje ya wali atakohoa na hakuna anayezuia kwamba usikohoe kwa sababu kukohoa ni njianya mwili kujilinda na baada ya hapo mtu anapata afadhali.
Sasa kwenye mafua, yale mafua ni body fluid ambayo miongoni mwa kazi zake ni kuondoa uchafu kwa kutumia njia ya kujizalisha kwa wingi fluid hiyo na hatimae kuanza kuvuja nje.
Kama hali iko hivyo kwamba mafua yanayotoka kwa mtu ni njia moja wapo ya kusafisha mwil i basi maana yake ni kwamba kuyazuia mafua hayo ni kusema kwamba hautaki uchafu huo utoke ndani ya mwili.
Hiyo ina maana ya kwamba unapotumia dawa ya kuzuia mafua maana yake unatumia dawa ya kuzuia uchafu usitolewe ndani ya mwili.
Je, hii haiwezi kutufanya tuwaze kwamba matumizi ya dawa za kuzuia mafua kwa muda mrefu inaweza kusababisha matatizo makubwa kama kushusha kinga ya mwili?
Maana unapozuia mafua maana yake unazuia ulinzi wa mwili,unapouzuia kwa muda mrefu hatimae utaudhoofisha mfumo wa kinga,na hatimae sasa kifua kitavamiwa kwa kasi hapo baadae na kusababisha COPD yaani matatizo ya kifua sugu?
kitunguu maji ndio suluhisho kata kachumbariHapa nilipo tangu jumapili nina mafua, kichwa kinauma, pua, koo na masikio yanawasha, macho yanauma, nimekosa hamu ya kula, mwili kuuma, nakohoa na kupiga chafya, homa juu ikabidi niende duka la dawa nipate dawa ya mafua. Leo naendelea vizuri najisikia kupona baada ya kunywa dawa