Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,644
Kila binadamu hasa sisi wanaume unapokuwa umetulia na kupumzisha akili ndipo mtiririko wa namna ulivyokuwa unaishi, unavyoishi na nini matarajio yako ya baadae huanza kujichora akilini. Mimi ni mmoja wao ambao kila mara nikikaa iwe kwenye starehe au wakati mgumu huwa picha zinaniijia kichwani.
AKILI YA KUZAMIA
Ukweli kabisa nikiwa niko kijijini kwetu ........ kipindi hicho ikiwa ni wilaya ya Geita sikuwaza kuna siku tazamia lkn akili hii ilistawi na kuwa sugu nilipopelekwa Secondary Geita (GESECO). Baada ya kujiunga shuleni hapo ndipo nikagudua hiyo haikuwa shule isipokuwa kambi ya jeshi, sehemu ya mkusanyiko wa wanafunzi waliofukuzwa mashuleni karibu yote ya Mwanza. Geseco na Nyamilama ndizo zilikuwa shule za ovyo kabisa kwa utovu wa nidhamu huku shule ya serikali ya Moringe Geita (baadae ilibadirishwa jina kutokana na kuwepo kwa shule nyingine yenye hilo jina Arusha)
Baadae nilipokuwa fomu two nikiwa bweni niliona mazigira ya kujisomea ni magumu sana hivyo nikamfuata headmaster aitwaye (Shitamanwa) nikarudi day na kuanza kujichanganya night class na wanafunzi wa Moringe kwa masomo zaidi na hapo ndipo nikakutana na rafiki zangu wawili wote wa mjini Mwanza tukisoma pamoja tuition na kuishi nyumba moja vyumba tofauti. Hawa rafiki zangu laiti kama wangekuwa wanatumia madawa ya kulevya basi na mimi ningekuwa mmoja wao kwa namna tulivyoshibana kama tumetokea kwa baba na mama mmoja.
Lakini nilikuja kugundua hawalipi school fees tangu waingie form two (kumbuka zamani tulikuwa tunasoma wakubwa). Nikipowauliza kwa nini katika majina ya wanafunzi ambao hawajalipa Karo ya shule nyie pia mmetajwa je hamuoni kama mtafukuzwa na nawaona hamfanyi starehe yoyote zaidi ya kujisomea? Kwa muda mrefu waliniambia wao hukusanya pesa kama nauli ya kuzamia nje ya nchi lkn wanakuwa busy kusoma endapo huo mpango ukigoma watalipa malimbikizo na kufanya mtihani.
Tangu siku hiyo na mimi nikajumuika katika mawazo hayo na letu likawa moja ila tofauti yangu na wao mimi baba alikuwa akinileta shule anamalizana na mhasibu na inabaki kuachiwa pesa kidogo ya matumizi na chakula. Baada ya mtihani kukaribia tulisomwa wale wote tutakao fanya mtihani lkn jamaa zangu majina yao hayakutajwa!! Tukaanza paper na katika hatua za mwisho waziri wa elimu kipindi hicho Juma Kapuya kupitia ITV akaufuta mtihani nchi nzima na akatangaza wanafunzi wote turudi makwetu hadi tutakapotangaziwa!! Rafiki zangu walifurahi sana kwa kicheko hadi cha kuanguka chini . Tuliporudi kufanya mtihani sikuonana nao ila nilipata taarifa kuwa rafiki yangu mmoja alipata ajali ya kugogwa na gari huko Mwanza hivyo akapooza (baba yake alikuwa mwanajeshi maeneo ya Pasiansi) na nilienda kumuona Bugando. Hali nikiyomkuta nayo sikutamani hata kumuuliza mchakato wa kuzamia isipokuwa nilimuuliza vipi Jaco B yupo hapa Mwanza akanijibu alishazamia Zambia lkn lengo lake ni kufika South Africa na hakuna mawasiliano yoyote. Nilipata division three combination zikiwa hazieleweki na nikapata post ya kwenda ualimu chuo cha ualimu ............. Ukerewe hata hivyo nilikataa kwani sikuipenda hata kidogo kazi ya ualimu.
Kukataa kwenda ualimu kulinifanya kuwa mbali kimaongezi na baba hadi nikakimbilia Zanzibar nikiwa na living na kile cheti cha matokeo ya awali. Baada ya muda mfupi nikapata ajira kwenye hotel ya kitalii .............. (namshukru mungu) na hapo kazini ndipo nikakutana na watu wenye akili za kuzamia walio sugu na mchakato ukapamba moto tukitumia gear za kwenda kusoma nje kwa vyeti vya kufoji na kutongoza wageni (wazungu), marafiki zangu watatu walifanikiwa lkn mimi nikakosa lakini sababu kuu ilikuwa mazigira ya kazi kwani wao walikuwa ni ma waiter na mwingine alikuwa mapokezi. Baadae nikiwa nishamake pesa kutokana na dili za store nilipigiwa simu kuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu mwaka...........wamegoma na kufukuzwa wote hivyo njoo na laki mbili uchukue kazi faster na sikulaza damu nikapanda meli na kurudi nyumbani na kweli nikapata kazi, nikapata mtaji, nikaoa na akili ya kuzamia ikanirudia tena nikiwa nafanya biashara zangu baada ya kupata mtaji kwa mshahara mkubwa wa mgodini pamoja na kiasi nilichoweka pindi nikiwa Zenj. Niliponunua simu ya kisasa baada ya kufahamiana na mama mmoja wa Kisouth ndipo mwanzo wa kuzamia ukaanza tena na kwa kweli yametimia huku nikiwa na familia.
NB: Kwa wazazi, makundi anayokunayo mtoto wako ndiyo mwelekeo wake wa baadae chukua hatua haraka kwani hata hii tabia ya ushoga na madawa ya kulevya chanzo ni makundi ya ujanani.