Kwanini ni vigumu kwa Tanzania kupata wawekezaji wapya katika mazingira ya sasa

Kwanza nikusahihishe utalii Tanzania mwaka jana uliingizia taifa US$4.5 billion na ni namba 4 kwa Africa. Paris kuna mahali walianzia na sisi ndio hapa tunaanzia. Vivutio tunavyo hutuhitaji wewe au mtu mwingine avitangaze bali ni sisi wenyewe.

Mataifa makubwa hivi sasa shida yao ni kuona wanaendelea kupata mali ghafi kwa bei ya mteremko. Mfano mikataba mibovu ya kuwadhulumu sio Tanzania pekee bali nchi zote za Afrika. Nchi za Afrika kuendelea kuona kwamba hawana uwezo wa kufanya lolote bali kuwategemea wazungu. Yaani Africans kuendelea kuwa second class citizens. Ni haya mataifa makubwa ambayo yanawafanya waafrika kuendelea kuwa masikini kwa kujifanya kwamba tunawategemea wao sana kuliko wao jinsi wanavyotutegemea. Mifano hai ipo mingi sana. Tunanunua bidhaa zao kwa bei ya ghali kuliko wao wanavyonunua bidhaa zetu, mfano Coffee, tea, mazao mbalimbai fruits, fish, maua vyakula mbali mbali matunda etc.

Kuhusu bwawa la mwalimu Nyerere litakapokwisha matumizi ya mkaa yatasahaulika Tanzania, Je ni miti mingapi hukatwa kila mwaka kwa ajili ya mkaa? Hizo mbuga zilikuwepo tangu wakati watemi wetu Mkwawa etc wao hawawezi kuwa waalimu wazuri wa kutufundisha sisi mazingira kwa sababu karibu nusu ya Tanzania ni hifadhi sasa ni mazingara gani ambayo wanaongelea? Vile vile usisahau kwamba East Africa wazungu waliamua tangu zamani wawasaidie zaidi Kenya kuliko nchi nyingine yeyote ie Tanzania kwa sababu ndio waliosababisha nchi za kusini mwa Afrika wawe free kutoka minyororo ya weupe. Wewe unaona upuuzi lakini sisi wenzako tunaona jinsi wanavyotufanyia, inawezekana hufahamu lakini hivi sasa agenda yao kubwa ni JPM whether you like it or not. Hatujaomba pesa za kujenga bwawa na vile vile usisahau wao ndio wachafuzi wakubwa wa mazingara. In actual fact hatutegemei tena pesa za kukinga bakuli maana zipo hapa hapa Tanzania ambazo kila uchwao zinachukuliwa na mafisadi, tutapambana nao tu hadi wazitapike.

BTW hoja zako zimejaa inferiority complex
 
Nilitaka kupinga andiko lako hili, hadi niliposoma habari za akina Bashite.

Uwekezaji wetu, matumaini makubwa yapo kwa Wachina. Lakini wachina wenyewe kama tumeanza kuwaweka mahabusu kuwatia adabu, hata wao wataanza kusita.
Ngoja tuemdelee kusikiliza.
 

These guys! Hawa ni wa kuombewa tu; they are half-baked, clueless and rudderless. Hizi ndizo Mwalimu aliziita hoja za nguvu. Mungu atusaidie sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…