Kwanini ni vigumu kwa Tanzania kupata wawekezaji wapya katika mazingira ya sasa

Mapato ya Tanzania kwenye sekta ya utalii kwa mwaka ni U$2.9 billion. Mapato ya utalii ya jiji la Paris (siyo France) ni U$89 billion. Bado na wewe unaona una nafasi kubwa kwenye utalii wa Dunia?.

Hivi kujengwa kwa bwawa la umeme au kutojengwa, kuna athari gani kwa mataifa makubwa?

Tusiwe wendawazimu wa kuyahusisha mataifa makubwa kwa hata mambo yetu ya kipuuzi. Kuna watu hata familia zao zikikosa mlo wa jioni, wanatoa sababu ni kwa sababu ya mabeberu. Uwendawazimu mkubwa!

Mataifa makubwa yana shida gani na viwanda vya Tanzania, nchi ambayo haichangii hata 1% ya manunuzi toka nchi za magharibi? Ni argument ya kijinga kabisa kuwa eti ujenzi wa bwawa la umeme la Tanzania unapigwa vita na mataifa makubwa kwa sababu nchi itakuwa na viwanda vingi. Hoja ya mataifa makubwa ilikuwa ni sustainability ya hifadhi ya wanyama - hifadhi ambayo bajeti ya utunzaji wake inayategemea mataifa makubwa.

Umeme ni ingridient ya ujenzi wa vuwanda lakini siyo kisababishi. Tunaweza kuwa na hilo bwawa na wala lisiongeze idadi ya viwanda kama mazingira yaliyopo sasa yataendelea kuwepo kama yalivyo leo.

Nimewahi kushiriki katika kuandaa vigezo vya mazingira ya uwekezaji kwa multinational investing companies. Umeme haupo. Mambo yale ya muhimu kabisa, Tanzania kwa sasa ina rank very low. CONFIDENCE is no. 1. Hakuna investor ambaye ataenda kuwekeza katika nchi ambayo mambo mengi yanategemea kauli ya mtu badala ya sheria
Kwanza nikusahihishe utalii Tanzania mwaka jana uliingizia taifa US$4.5 billion na ni namba 4 kwa Africa. Paris kuna mahali walianzia na sisi ndio hapa tunaanzia. Vivutio tunavyo hutuhitaji wewe au mtu mwingine avitangaze bali ni sisi wenyewe.

Mataifa makubwa hivi sasa shida yao ni kuona wanaendelea kupata mali ghafi kwa bei ya mteremko. Mfano mikataba mibovu ya kuwadhulumu sio Tanzania pekee bali nchi zote za Afrika. Nchi za Afrika kuendelea kuona kwamba hawana uwezo wa kufanya lolote bali kuwategemea wazungu. Yaani Africans kuendelea kuwa second class citizens. Ni haya mataifa makubwa ambayo yanawafanya waafrika kuendelea kuwa masikini kwa kujifanya kwamba tunawategemea wao sana kuliko wao jinsi wanavyotutegemea. Mifano hai ipo mingi sana. Tunanunua bidhaa zao kwa bei ya ghali kuliko wao wanavyonunua bidhaa zetu, mfano Coffee, tea, mazao mbalimbai fruits, fish, maua vyakula mbali mbali matunda etc.

Kuhusu bwawa la mwalimu Nyerere litakapokwisha matumizi ya mkaa yatasahaulika Tanzania, Je ni miti mingapi hukatwa kila mwaka kwa ajili ya mkaa? Hizo mbuga zilikuwepo tangu wakati watemi wetu Mkwawa etc wao hawawezi kuwa waalimu wazuri wa kutufundisha sisi mazingira kwa sababu karibu nusu ya Tanzania ni hifadhi sasa ni mazingara gani ambayo wanaongelea? Vile vile usisahau kwamba East Africa wazungu waliamua tangu zamani wawasaidie zaidi Kenya kuliko nchi nyingine yeyote ie Tanzania kwa sababu ndio waliosababisha nchi za kusini mwa Afrika wawe free kutoka minyororo ya weupe. Wewe unaona upuuzi lakini sisi wenzako tunaona jinsi wanavyotufanyia, inawezekana hufahamu lakini hivi sasa agenda yao kubwa ni JPM whether you like it or not. Hatujaomba pesa za kujenga bwawa na vile vile usisahau wao ndio wachafuzi wakubwa wa mazingara. In actual fact hatutegemei tena pesa za kukinga bakuli maana zipo hapa hapa Tanzania ambazo kila uchwao zinachukuliwa na mafisadi, tutapambana nao tu hadi wazitapike.

BTW hoja zako zimejaa inferiority complex
 
..hakuna kitu foreign investors wanakithamini na kukipa kipaumbele kabla hawajafikia maamuzi ya kuwekeza kama rule of the law and predictable government decisions.
South Africa hawana issues na hayo mambo mawili, lakini soma article hii ifuatayo halafu ujiulize ikiwa kuna watu wana mawazo ya aina hiyo South Africa itakuwaje kwetu?
Wake up ccm! Well; kama ccm hii inaona kina Bashite ni viongozi basi we are doomed as a nation.

Nilitaka kupinga andiko lako hili, hadi niliposoma habari za akina Bashite.

Uwekezaji wetu, matumaini makubwa yapo kwa Wachina. Lakini wachina wenyewe kama tumeanza kuwaweka mahabusu kuwatia adabu, hata wao wataanza kusita.
Ngoja tuemdelee kusikiliza.
 
Mapato ya Tanzania kwenye sekta ya utalii kwa mwaka ni U$2.9 billion. Mapato ya utalii ya jiji la Paris (siyo France) ni U$89 billion. Bado na wewe unaona una nafasi kubwa kwenye utalii wa Dunia?.

Hivi kujengwa kwa bwawa la umeme au kutojengwa, kuna athari gani kwa mataifa makubwa?

Tusiwe wendawazimu wa kuyahusisha mataifa makubwa kwa hata mambo yetu ya kipuuzi. Kuna watu hata familia zao zikikosa mlo wa jioni, wanatoa sababu ni kwa sababu ya mabeberu. Uwendawazimu mkubwa!

Mataifa makubwa yana shida gani na viwanda vya Tanzania, nchi ambayo haichangii hata 1% ya manunuzi toka nchi za magharibi? Ni argument ya kijinga kabisa kuwa eti ujenzi wa bwawa la umeme la Tanzania unapigwa vita na mataifa makubwa kwa sababu nchi itakuwa na viwanda vingi. Hoja ya mataifa makubwa ilikuwa ni sustainability ya hifadhi ya wanyama - hifadhi ambayo bajeti ya utunzaji wake inayategemea mataifa makubwa.

Umeme ni ingridient ya ujenzi wa vuwanda lakini siyo kisababishi. Tunaweza kuwa na hilo bwawa na wala lisiongeze idadi ya viwanda kama mazingira yaliyopo sasa yataendelea kuwepo kama yalivyo leo.

Nimewahi kushiriki katika kuandaa vigezo vya mazingira ya uwekezaji kwa multinational investing companies. Umeme haupo. Mambo yale ya muhimu kabisa, Tanzania kwa sasa ina rank very low. CONFIDENCE is no. 1. Hakuna investor ambaye ataenda kuwekeza katika nchi ambayo mambo mengi yanategemea kauli ya mtu badala ya sheria

These guys! Hawa ni wa kuombewa tu; they are half-baked, clueless and rudderless. Hizi ndizo Mwalimu aliziita hoja za nguvu. Mungu atusaidie sana.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom