Kwanini ni muhimu sana kutenda haki

James88

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Posts
1,700
Reaction score
1,765
Watu wengi sana wamekuwa wakituhusia kuhusiana na swala la kutenda haki. Wazazi, Viongozi wa kidini, Viongozi wa kiserikali na makundi mengine mengi... Lakini swali ni Je ni kwanini ni muhimu kuyenda haki?

Kuna Usemi mmoja wa kizungu unasema "what goes around comes back around", maana halisi ya usemi huu ni kwamba Yale unayoyafanya kina siku yatakuka kukurudia. Kama unafanya mabaya basi mabaya yatakurudia na kama unafanha mema basi pia mema yatakurudia. Sasa basi hebu tuangalie cases kadhaa ambazo zinaonesha ni kwanini ni muhimu kutenda haki.

1. Fikiria wewe ni Mhadhiri wa chuo kikuu(Chuo cha udaktari especially surgiary), Kuna mwanafunzi wako unafahamu fika kwamba kuna mambo fulani kuhusu taaluma yake hayawezi kabisa yet anakuhonga halafu unampitisha kwamba amefaulu. Miaka inaenda unakuja kupata mgonjwa ambaye anatakiwa kufanyiwa surgiary na daktari wa kumfanyia surgiary ndiyo yuleee ambaye ulimpitisha kwa rushwa. Finally ndugu yako anafariki kwa sababu ya uzembe ambao ulisababishwa na tamaa zako.


2. Fikiria tena kwamba wewe ni daktari katika kitengo cha kupima ukimwi. Kuna mtu ni muathirika let say ni mwanamke anakuja anakuhonga na anakuambia kwamba atakuja kupima na mtu wake hivyo katika kutoa majibu itabidi usemw kwamba yuko salama. Finally wanakuja kupima na unasema wote wako salama. Miaka inapita, one day mmoja kati ya wale wawili waliokuja kupima hasi yule ambaye hakuwa na maambukizi anakuja kutembea na mwanao. Now ukimwi unaingia rasmi nyumbani kwako lakini chanzo hasa itakuwa ni wewe mwenyewe.

Hiyo ni mifano michache sana ambayo inaonesha ni kwa kiasi gani ni muhimu kutenda haki. Watu wengi tunashindwa kujifunza lakini ukweli ni kwamba mambo mengi yapo indirect sana. Ubaya ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanafikiria in a short term.

Ngoja tuendelee kujifunza. Lakini siku zote tenda haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…