Habari zenu wanajf?
Kwanza kabisa nitoe pongezi zangu kwa shirika letu la nyumba NHC. Tangu menejimenti mpya ya akina Mchechu na wenzake ianze kufanya kazi; tumeona mabadiliko makubwa katika utendaji wa shirika hilo, kitu ambacho hakijawahi tokea tangu kuanzishwa kwake.
Kitu kinachnitatiza ni kuona NHC ikiwekeza katika miradi mingi sehemu mbalimbali nchini; lakini sijasikia mradi wowote katika jiji la Mbeya. Kuna tatizo gani kisiasa, kiuchumi au kijamii linalosababisha Mbeya kuachwa katika maendeleo hayo??
Mwenye maoni, majibu au ushauri anakaribishwa.
Karibuni!