Kwanini ndege inapotua taa za ndani huzimwa?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
7,121
10,233
Wale wahudumu husema wanafanya vile kwa mujibu wa sheria za kimataifa, je hiyo sheria ilinuia nini kutaka taa zizimwe ndani wakati pilot yupo kwenye cockpit na si kwamba taa zinamwumiza asione mbele kama nyadikwa nikiwa kwenye lendrova langu.Asante kwa majibu
 
Mkuu ndege gani hiyo walizima taa za ndani? Au kitu cha bibi sumbawanga?kawaida taa za ndani huwekwa dimmed then floor light zinakuwa real glowing kwa ajili ya kuinyeshea milango iLipo incase of emergency
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wale wahudumu husema wanafanya vile kwa mujibu wa sheria za kimataifa, je hiyo sheria ilinuia nini kutaka taa zizimwe ndani wakati pilot yupo kwenye cockpit na si kwamba taa zinamwumiza asione mbele kama nyadikwa nikiwa kwenye lendrova langu.Asante kwa majibu
Ndege gani hiyo? Hii ndo nasikia kwako
 
Kama ni kwa Pilot,hilo ni la kawaida. kule kuna navigation instruments ambazo huwa zinamsaidia kuruka na kutua,kumbuka Ndege inaporuka Rubani haangalii nje kama dereva wa gari anatumia hizo Instrumente ambazo huwa zina rangi tofauti na kila rangi huwa na sababu zake.
images
 
Wale wahudumu husema wanafanya vile kwa mujibu wa sheria za kimataifa, je hiyo sheria ilinuia nini kutaka taa zizimwe ndani wakati pilot yupo kwenye cockpit na si kwamba taa zinamwumiza asione mbele kama nyadikwa nikiwa kwenye lendrova langu.Asante kwa majibu

mkuu swali lako zuri na majibu yake ni kama ifuatavyo:
Kuna sababu kuu mbili zinazopelekea taa kuzimwa wakati wa kuruka na kutua kwa ndege,nazo ni kama ifuatavyo:

1.sababu ya kwanza ni kuwa,taa huzimwa na kuachwa zile zilizoko chini zinazoonyesha milango ya kutokea kwa njia ya kawaoda na ile ya dharura ili kuyawezesha macho yako kuzoea ugiza na mwanga hafifu wa zile taa za chini.hii ni tahadhari kuwa endapo itatokea dharura wakati huo wa kutua au kuruka basi iwe ni rahisi kwako kuziona zile taa na kuzifuata kwa kawa ajili ya uelekeo wa kutoka nje.

2.ndege inaporuka au kutua huwa inatumia umeme mwingi,hivyo basi rubani huzima taa hizo ili kupunguza matumizi ya umeme na kuhifadhi umeme mwingi zaidi ili kusudi kama inatiokea dharua mfano injini moja ikazingua basi awe na umeme wa kutosha kukikontroo chombo na kukishusha salama

natumai nimeeleweka
 
umeeleweka mkuu thanks kwa majibu mwanana
 
Kama ni kwa Pilot,hilo ni la kawaida. kule kuna navigation instruments ambazo huwa zinamsaidia kuruka na kutua,kumbuka Ndege inaporuka Rubani haangalii nje kama dereva wa gari anatumia hizo Instrumente ambazo huwa zina rangi tofauti na kila rangi huwa na sababu zake.
images
Mkuu kwa hii pichani ndio windscreen ya rubani au anatumia hii na kioo cha mbele
 
Lakini pia ajali nyingi za ndege hutokea wakati wa kuruka na kutua hivyo kuzima taa kutasaidia abiria kuona milango ya dharula vizuri zaidi kama alivyosema mkuu hapo juu.
 
Kwa nn pia huambiwa kufungua blinds za madirisha wakati wa ndege kutua.?
 
Mkuu kwa hii pichani ndio windscreen ya rubani au anatumia hii na kioo cha mbele
Hiyo ni sehemu tu ya Front cockpit ndani ya ndege,Ila ninavyofahamu Rubani hana ulazima wa kuangalia kioo cha mbele katika Flights zake,anapoangalia hapo anapata maelezo yote yanayohusu route yake kama yupo mita fulani kutoka usawa wa bahari,speed anayoruka,hata matairi yanapotoka hapo anaona na maelezo mengi yanayohitajika.
 
sheria ililenga nini asa? technical reason? security reason. hapo ndio mtoa mada anataka kujua?
For security reasons mkuu... At least tangazo lao ndo huwa linasema hivyo!!! "For security reasons, the aviation rules demand the switching of lights during taking off and landing"
 
Umenikumbusha mbali na hiyo picha.Si nilipanda siku moja Dar -Moro (ndege) vile vya watu kumi! Mnaingia kama mnaingia kwenye toyota mark II nikapewa karibu na siti ya dereva (rubani)! Nilishangaa kweli siku hiyo ila lakini, Wee ! Eheee! Yaani kilikuwa kizungumkuti na ile ndege, ilipokuwa ikipita, pishana na hata kawingu kadogo mnarushwa utadhani dalala inapita barabara ya Kutoka dalaja la Nyerere kuelekea Kigamboni ndani! Yaani kama unaroho ndogo ndege zile usipande. Yaani tena pale mbele unajiona kama upo kwenye 'Ungo' uliorushwa mawinguni. Ni wakati huo nilibahatika kuona kwa karibu namna ndege ndogo iendeshwavyo.
====
Sisi bwana hatukuzimiwa taa, tena tulitua pale Kihonda mida ya saa 12:30 jioni.
 
Kwa sababu za kiusalama zaidi... Kupunguzwa mwanga taa za ndani ya ndege au kuzimwa hutokea kipindi hali ya hewa inapokuwa mbaya... Kwa maana ya kukiwa na ukungu mkali, giza kali nje ya ndege...

Ki usalama itakusaidia wewe uliyendani kuona taa za kuongozea ndege au zilizo kwenye lami ya njia za ndege vizuri endapo kutakuwa na tatizo au dharura...

Ni kama gari unapoliendesha usiku huku ukiwa umewasha taa za ndani, inakupa ugumu kuona vizuri nje na unaweza pata ajali...

Cc: mahondaw
 
Umenikumbusha mbali na hiyo picha.Si nilipanda siku moja Dar -Moro (ndege) vile vya watu kumi! Mnaingia kama mnaingia kwenye toyota mark II nikapewa karibu na siti ya dereva (rubani)! Nilishangaa kweli siku hiyo ila lakini, Wee ! Eheee! Yaani kilikuwa kizungumkuti na ile ndege, ilipokuwa ikipita, pishana na hata kawingu kadogo mnarushwa utadhani dalala inapita barabara ya Kutoka dalaja la Nyerere kuelekea Kigamboni ndani! Yaani kama unaroho ndogo ndege zile usipande. Yaani tena pale mbele unajiona kama upo kwenye 'Ungo' uliorushwa mawinguni. Ni wakati huo nilibahatika kuona kwa karibu namna ndege ndogo iendeshwavyo.
====
Sisi bwana hatukuzimiwa taa, tena tulitua pale Kihonda mida ya saa 12:30 jioni.
, eti kama ungo
 
Hiyo ni sehemu tu ya Front cockpit ndani ya ndege,Ila ninavyofahamu Rubani hana ulazima wa kuangalia kioo cha mbele katika Flights zake,anapoangalia hapo anapata maelezo yote yanayohusu route yake kama yupo mita fulani kutoka usawa wa bahari,speed anayoruka,hata matairi yanapotoka hapo anaona na maelezo mengi yanayohitajika.

Utajua umuhimu wa vioo vya mbele vya rubani ukitazama hii video clip hasa kati ya 0:25 na 0:40.

Back
Top Bottom