Kwanini nashabikia mapinduzi ya UKAWA

Tunaopenda mabadiliko tuendelee kupiga kelele mpaka masikio ya baadhi ya watu yafunguke. Hoja za kutoipa CCM kura ziko wazi kabisa. Lakini inasikitisha kuna watu humu hata ungekesha unajenga hoja hawatakuelewa. Ni kama walevi waliopindukia. Wao ni ushabiki tu. Tukiondoka hapa jamii forum wote tunalala gizani, tunakunywa maji ya visima, tunapeleka wagonjwa kwa waganga wa kienyeji badala ya hopspitali, nk. Lakini tunapoongelea mabadiliko, utawasikia baadhi yetu hasa hawa "Mashabiki" wanaanza kupiga ramli kuhusu UKAWA, eti hawana hakika na sera zao, au viongozi wao, nk. Nchi hii itaendelea kuogelea katika lindi la umasikini kwa muda mrefu sana kama tutaendelea kuwa na kundi kubwa la watu wenye fikra hizi. Ni lazima tufike mahali kama sera za serikali tuliyoipa kura hazifanyi kazi kuondoa matatizo yetu, tuikatae serikali hiyo kwa nguvu ya kura zetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha wale tunaowapa mamlaka kupitia kura zetu wanakuwa na nidhamu na kutekeleza kwa vitendo yale wanayoahidi. La sivyo tutaendelea kuishi kwa matumaini mpaka lini?
 
Ukawa kipindi cha kina Dr Slaa na professor Lipumba ilikuwa inajulikana inaenda wapi na angalau itafanya nini. Sio hii ukawa ya mtoswa ccm

Exactly kiongozi, UKAWA ya Mbowe, Lowassa, Mbatia na Sumaye imekosa mwelekeo. Nilikuwa mfuasi wa itikadi zao hapo mwanzo. Leo hii sioni wanachofanya zaidi ya kutafuta kula...
 
Mpaka sasa sijaona kwanini niipigie kura ukawa??
Ukawa sera yenu ni nini?? Utaambiwa mabaya ya CCM tuuu!!!
Nataka kusikia ukawa mtafanya nini??

Kama hujaona kwann ipigie kura ccm, huwez ona umuhimu wa kuwa na taifa lililo imara katika misingi ya kiuchumi,afya, elimu..etc
 

mapinduzi ya ukawa ni mapinduzi ya kumuondoa Dr. slaa na kumweka Lowassa
 
Ujue Ukawa Mnapata Nguvu Na Kujinasibu Kutokana Maneno Ya Nyerere Ya" Watanzania Wanahtaj Mabadiliko Na Wasipopata Ndan Ya Ccm Watayatafuta Nje Ya Ccm"na Watz wachache walivo connect na matatizo yao wakaamin ukawa ndo solution lakin wakasahau Nyerere Huyohuyo Alisema "mabadiliko Ya Kwel Yatapatikana Ndan Ya Ccm"na Wakat Huo Ndo Sasa...Ukawa Ni Kwel Inataka Kuleta Mabadiliko Lakin Hayatakua Ya Kwel,hata Sis Tumejionea Kama Mtu M1 Anaweza kuja na Kuparanganya Mising Yote Ya Chama Si Zaid Wakichukua Nchi,watakua Wanasimamia Lip Kama Mising Yao Wenyewe Wameshndwa Kuisimamia?
 
Hao ukawa ndo hamna kitu kabisa. Hamna watakacho kifanya zaid ya kuanza kukwapua na kulipa visasi ambavyo havitakuwa na tija yoyote kwa nchi kama nchi.


tatizo hapo si UKAWA bali mtu waliomuweka kupeperusha bendera ya ukawa. ccm A kwa ccm B bora ya ccm A.

Yawezekana mme ni quote kwamba mimi ni kada wa upinzani. Hapana mimi sio kada.

Ila mimi ni raia wa kawaida tu ambaye nimejiridhisha beyond no doubt kwamba raia tunahitaji mabadiliko ya kisiasa na fikra nje ya system msonge ya CCM.

System ambayo kwa miaka 50 imetengeneza bomu la mparanganyiko na maovu katika jamii yenu kitanzania.

System iliyotengeneza viongozi wabinafsi na wala rushwa wa wazi wazi.

System ya viongozi wenye ahadi za uongo kwa jamii yao na kudanyanya waziwazi.

System iliyoleta uduni katika elimu na kufanya watu wawe vipofu wakujua hasa taifa linaelekea wapi.

System iliyoshindwa kutumia potentiality ya utajiri tulionao kama nchi kuwa na sound economic growth.

We unafikir ukiwa mwana ukawa tu ndo unaweza kuona mambo kama haya. Yeyote anaweza kuona kama ukikaa chini na kufikiri kwa dhati hata ukiwa huko CCM.

Ni kwamba waweza baki na chama chako kiwe CCM au whatever Ila unatakiwa kujua kwamba nchi inahitaji mabadiliko na inahitaji watu wenye maono. Over
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…