Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1977 mpaka mwaka 1980 halafu akateuliwa tena kushika wadhifa huo mwaka 1983 mpaka 1984 alipofariki dunia.
Wakati wa awamu ya kwanza ya uongozi wake Hayati Sokoine alifanya kazi ya uwaziri mkuu kwa weledi wa hali ya juu haswa wakati wa vita vya kagera mwaka 1978-1979 dhidi ya uvamizi majeshi ya Uganda Sokoine akiwa Wazir Mkuu alisimamia vita hivyo akishirikiana na mkuu wa majeshi wa wakati huo General David Musuguri mpaka Tanzania ikashinda vita hivyo.
Baada ya kuondolewa kama Waziri Mkuu Sokoine alienda kusoma Yugoslavia kwa muda wa miaka mitatu mpaka mwakan1983 aliporejea nchini na kuteuliwa tena kuwa waziri mkuu watu wengi wanaamini Sokoine alienda Yugoslavia kupigwa msasa kisiasa ili aje kuwa mrithi wa Mwalimu Nyerere kwani nchi ya Yugoslavia ilikuwa inafuata sera za kijamaa kama Tanzania.
Edward Sokoine alipochukua wadhifaa huo mwaka 1983 alikutana na changamoto kubwa ya kupambana na wafanyabiashara wakati huo walikuwa wakiitwa walanguzi kwani serikali ilikuwa ikitoa chakula na mahitaji muhimu kwa bei nafuu kwa wananchi lakini hawa wafanyabiashara walikuwa wakinunua bidhaa hizo na kuzificha ili baadaye waziuze kwa bei kubwa wafanyabiashara wengi walikamatwa na wengine walikimbia nchi, pili Edward Sokoine alisimamia kurudisha nidhamu kwa wafanyakazi wa umma na mawaziri hakuwa na mzaha katika utenda wa serikali kwa wakati huo.
Mabadiliko ya kiuchumi Edwars Sokoine alipunguza kodi kwa wanaoagiza magari aina ya pick-up na tractor ili wakulima wapate urahisi katika kazi zao, Sokoine ndiyo aliruhusu magari ya Dala Dala ya watu binafsi kuanza kufanya kazi katika jiji la Dar, neno dala dala lilitokana na dola ya kimarekani kwani wakati huo dola moja ilikuwa ni sh tano na nauli ya kusafiri jijini Dar ilikuwa ni sh tano. Mwezi wa nne mwaka 1984 ilikuwa siku ya masikitiko na simanzi makubwa kwa watanzania kwani Edward Sokoine aliyekuwa tegemeo ama nguzo kubwa sana kwa serikali ya awamu ya kwanza alifariki kwa ajali ya gari huko Morogoro.
Rais Magufuli ndio kiongozi pekee ambaye naona ambaye ameamua kuvaa viatu vya Marehemu Sokoine haswa kwa utendaji wake wa kazi pamoja na changamoto nyingi anazokutana nazo. Kweli kama Mwalimu angekuwa hai leo angeguswa sana na utendaji wa Rais Magufuli.