SoC03 Kwanini mtu huyu haguswi?

Stories of Change - 2023 Competition

King Muchachu

Member
Jun 8, 2023
6
7
Kuna majukumu mengi ambayo napaswa kuyatekeleza katika nchi yangu, mengine ni kwa mujibu wa sheria na mengine ni yakutumia busara lakini yote ni kwasababu ya kuwasaidia wananchi wangu, kikundi au jamii niliyo apa kuitumikia kwa mujibu wa sheria lakini sifanyi hivyo na siwajibishwi, muda mwingine nawaza huenda wananiogopa au wanaogopa kunikwaza au labda hakuna sheria inayoweza kutumika kuniwajibisha au walio apa kwaajili ya kuilinda sheria hawafanyi hivyo bado sina majibu.

Wananchi wangu hutumia siku tisini na tisa {99} kulalamika lakini mimi huja siku ya miamoja {100}kuwaambia kuwa nimesikia malalamiko yao na nitayafanyia kazi, ikionekana kuna wananchi wanahoji sana nawachukua nawapa uongozi pia nawafundisha kuwa kama mimi nazidi kuongeza tatizo kwenye jamii yangu matatizo hubaki palepale au kuongezeka zaidi wananchi huanza kulalamika tena, hapa huwa natambua kuwa wananchi wanatamani kuniwajibisha lakini hawajui pakuanzia pia hawajui utaratibu wa kufuata hawana uhakika kama wanacho kilalamikia nihaki yao kisheria au kikatiba hakuna mtu wa kuwafafanulia, hiyo kwangu nifuraha kubwa kutumia ujinga na matatizo yao kujinufaisha.

Muda mwingine natamani kuwafundisha namna ya kudai haki zao bila kuvunja sheria lakini nakwepa kuwajibika juu yao wakati mwingine nikifanya hivyo naweza kuchukiwa na bosi wangu mwenye tabia kama yangu na kazi nitaikosa, natamani ninufaike pasipo kuvuja jasho, laiti kama wangalijua wanaweza kuanzia kwa viongozi wa chini kabisa wa serikali kueleza matatizo yao ambapo itakuwa rahisi kufuatilia na kujua tatizo lipo wapi au mtu anaekwamisha ninani wangefanya hivyo lakini wao huja mitandaoni kwanza kabla ya kukutana na viongozi wa chini kabisa kiserikali hivyo naweza kuwajibu kirahisi tuu kwamba sikuona wala kusikia malalamiko yao au nikawapa majina mabaya walio chapisha habari mtandaoni na kuwapuuza, lakini wakifuata utaratibu nitashindwa kuwaambia kuwa sikuona wala kusikia malalmiko yao sababu kutakuwa na ushahidi hivyo nitachukua machache niyafanyie kazi, mengine yatasubiri, kwanza hakuna wa kuniuliza.

Wananchi wengi hawajui sheria muhimu zinazo walinda hivyo nirahisi kwangu kutumia muhimili mmoja katika serikali kwaajili ya kuwatisha, naweza kuwatafutia jina baya tuu kisha nikawashtaki, hapa wataniogopa na wataambiana wenyewe kuwa mimi sichezewi. Wataniogopa wataishia kulalamika chinichini lakini hakuna wakunifuata sijui ninani atawakomboa sababu hata elimu tunazo wapa kuanzia mashuleni bado hazigusi maeneo muhimu yanayo amua maisha yao, pengine ingefanyika hivyo kungekuwa na uelewa wa kutosha na ningetekeleza majukumu yangu kwa weledi nisiwajibishwe.

Pia nilicho gundua kwa wananchi wangu nikuwa hawana maelezo ya kutosha kuhusu bajeti zinazotengwa na serikali kwaajili yao hata vijana ambao ndio wenye nguvu na tegemezi bado hawajui kama wanaweza kuunda vikundi vya watu kumi wakapewa mkopo na serikali wakajikwamua kiuchumi na jambo hili sipendi lizungumziwe mahali popote ili wasije kuelewa wakaniuliza zilipo fedha hizo, wale wachache wanao elewa hawapati fedha hizo kama hawako upande wangu.

Nilicho gundua sheria ni msumeno lakini kuna muda inachagua wa kumkata mbona mimi siguswi? Na nikiharibu sana najua nitahamishwa, hiyo ndo adhabu yangu kubwa na hainipunguzii chochote
Kwanza nakumbuka sikuwa tayari kuwatumikia wananchi ilitokea fursa tuu(conection) mjomba akaniita niende nikapeleka vyeti, baadae ajira ikatangazwa tukaenda wengi kwenye usahili, nakumbuka wapo wengi waliokuwa na uwezo mzuri wa kujieleza zaidi yangu lakini hawakufua dafu tayari nafasi hiyo ilikuwa yangu kwani mapema sana nilisha peleka vyeti na hivyo tulikuwa tukikamilisha ratiba tuu, Hapa nilijua kuwa hata mifumo yetu ya ajira bado sio rafiki kwa wenye uwezo mzuri kazini na pia sio rafiki kwa maskini yaani kiufupi inaangalia “unamjua nani” na sio “unajua nini”,

Muda mwingine nawaza mfumo wa ajira uwe na namba maalumu za utambulisho badala ya majina kama ilivyo zoeleka ambapo baada ya mtu kuomba ajira na kukamilisha vigezo vyote basi mfumo utatengeneza namba ambayo hata mwombaji hawezi kuifahamu, taarifa zitakazo onekana ziwe umri, jinsia na mwaka wa kuhitimu pamoja na chuo alichohitimu pekee, na baada ya kupangiwa kituo cha kazi taarifa zake ziwe katika hali ya kusubiri (pending) akiripoti kazini nakuonyesha nakala zote zinazotakiwa mwajiri wake athibitishe ndipo taratibu nyingine ziendelee, kuwepo na muda maalumu wa kukamilisha zoezi hilo. Nafikiri wangefanya hivyo huenda nisinge kuwa hapa badala yake kiti hichi kingekaliwa na mtu mwenye nia na kiu ya kusaidia wananchi.

Ningependa kupendekeza kuwepo na mifumo ya siri ya serikali kwaajili ya kutoa taarifa na mifumo hiyo iweze kufikiwa na wananchi na kuona kero mbalimbali za viongozi walio na tabia kama yangu lakini bila kumtambua aliye toa taarifa hiyo, uchunguzi ufanywe na kama ikibainika kiongozi hawajibiki sheria zichukuliwe badala ya kuhamishwa kituo au eneo la kazi, mfumo huo unaweza kuwa na sekta mbalimbali mfano Afya, uchumi, maji,mazingira na pomoja na sekta nyingine ambapo mwananchi atachagua kero yake inaenda sehemu gani haswa.Wananchi warudishiwe nguvu ya kuwawajibisha viongozi wao.

Wananchi waelimishwe ipasavyo juu ya mambo muhimu kwenye jamii, watambue haki zao ikiwezekana wafundishwe baadhi ya haki za msingi wakati wa masomo mashuleni au katika vikao na viongozi wao.
Tuweke mifumo kisheria ambayo ndiyo itakayo tumika kumuongoza kiongozi na si kiongozi kuongoza kwa hisani au ilani ya chama chake pekee, na ikiwezekana sheria hizo ziwe wazi na kwa lugha ya Kiswahili ili ziweze kueleweka na watu wote.
Nimeyaweka haya bayana sababu nakaribia kustaafu na nisingependa mambo haya yajirudie katika kipindi kijacho natamani sikumoja pawepo na usawa kwenye sheria na pia maeneo ya kazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom