Kwanini MORUWASA wasiongeze uzalishaji maji kwa kuchimba visima virefu maeneo ya Kihonda??

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
697
WanajF,

Mimi nakereka sana kuona miji ambayo iankua kwa kasi kama Morogoro bado mamlaka husika hawajiongezi na kupeleka huduma za jamii kama maji kwa haraka kabla maeneo mengi hayajawa over-populated. Mfano ni eneo la Kihonda na kuelekea kata ya Lukobe na maeneo jirani. Katika kata hii hakuna maji ya bomba, lakini uwezekano wa kutumia maji ya chini ya ardhi upo kwani maeneo haya kwa tafiti chache zilizofanyika inaonekana maji yapo.

Je, sijui ni kwanini MORUWASA hawajiongezi na kuchimba visima walau katika kila umbali wa km 1 kuna kwa na kisima kirefu. Nchi kama Thailand, India, Bangladeshi, n.k. wametumia njia hii.

Nawauliza management ya MORUWASA hili wazo mnalo kichwani au mnasubiri mpaka JPM ndo awaeleze na hili??? Kwanini Mkurugenzi usiwajibike??

Binafsi ni mtaalamu wa utafiti wa maji ya chini ya ardhi (groundwater hydrologist), kama hamna wataalamu basi mseme ili tuwasaidie.
 
angalau umetumia ubunifu kutafuta ajira... shout out! ila kiukweli kihonda panakera sana jamani... yaani utadhani tupo Darfur!
 
Aisee umesema point sana

Nimekaa hapo kihondo Kilimanjaro tangu 2009 ni ka mtaa kanakoanzaa kukua kwa kwa kasi na wahamiaji wengi

Lakini kuna shida ya maji sanaaa

Wakati mwingine wiki nzima hamna maji maisha gani hayo daaah

Morogoro ni mji mzuri sana kijiografia but uhaba Wa maji unaufanya uonekane kama mji Wa ovyo sana

Hao jamaa moruwasa kwanza nasikia wanaafanya biashara ya kuuza maji mitaani na magari badala kuwapa watu maji kwenye mabomba

So sad
 
Wahusika wa MORUWASA mbona hamjibu kitu?? Hata waziri wa maji jitokeze useme ni kwanini hili tatizo/wazo hamuoni ni la msingi?
 
MORUWASA kwa kweli wamechemsha kabisa katika usambazaji maji hususani katika miji mipya na inayokuwa kwa kasi kama vile Tubuyu, Tungi, Mkundi.

Kimsingi wanajisahau sana kufanya bunifu mbalimbali za kupeleka maji katika mji tajwa wa mleta uzi na hio mingine niliyotaja.

Hivyo naunga wazo la mleta Uzi.
 
MORUWASA wameshindwa kutreat vizuri hata hayo kidogo tu wanayoproduce kutoka Mindu. Nadhani income generation capacity yao ni ndogo sana na wanahitaji external support. Wangeweza kujiongeza kidogo huenda wangepata loans kutoka AfDB and the like..
 
Ni ubaradhuri na ubazazi tu wa watumishi wa MORUWASA, pale wanauza msamvu wana kisima kikubwa wanauza maji kwenye ma bowser litre 1000 kwa sh. 940 ila majumbani wanaenda kuuza sh. 15,000 kwa litre na wanaofanya hiyo biashara asilimia kubwa ni wafanyakazi wa Moruwasa. Afu kule juu mlimani kuna jamaa ana maji mengi sana na ni safi na salama ila hawampi kibali cha kusambaza maji hadi kihonda.
 
Mh. Rais Magufuli tunaomba watu wa MORUWASA washughulikiwe kwani wanafanya biashara ya kuuza maji ndo maana hawajali uboreshaji wa miundo mbinu ya maji.
 
Mlima lukobe wenyewe una maji ya kutosha sema morogoro sio kama sehemu nyingine watu walio kwenye nafasi ya kutoa maamuzi si wazawa,naomba mnielewe hata viongozi wa kuchaguliwa ngazi za kata wengi si wazawa wa pale tofauti na mikoa mingine kiasi ule uzalendo unakosekana.
 
WanajF,

Mimi nakereka sana kuona miji ambayo iankua kwa kasi kama Morogoro bado mamlaka husika hawajiongezi na kupeleka huduma za jamii kama maji kwa haraka kabla maeneo mengi hayajawa over-populated. Mfano ni eneo la Kihonda na kuelekea kata ya Lukobe na maeneo jirani. Katika kata hii hakuna maji ya bomba, lakini uwezekano wa kutumia maji ya chini ya ardhi upo kwani maeneo haya kwa tafiti chache zilizofanyika inaonekana maji yapo.

Je, sijui ni kwanini MORUWASA hawajiongezi na kuchimba visima walau katika kila umbali wa km 1 kuna kwa na kisima kirefu. Nchi kama Thailand, India, Bangladeshi, n.k. wametumia njia hii.

Nawauliza management ya MORUWASA hili wazo mnalo kichwani au mnasubiri mpaka JPM ndo awaeleze na hili??? Kwanini Mkurugenzi usiwajibike??

Binafsi ni mtaalamu wa utafiti wa maji ya chini ya ardhi (groundwater hydrologist), kama hamna wataalamu basi mseme ili tuwasaidie.
Hawana mpango wa maendeleo wamejigeuza TRA wanakusanya mapato tu tena kwa miundombinu ya zamani kabla ya kuanzishwa mamlaka. Haiwezekani zaidi ya nusu ya eneo la manispaa halina miundombinu ya maji na wao wapo tu.
 
Napendekeza hiyo shughuli ya kukusanya mapato wanyang'anywe ili wabaki na shughuli ya kuweka miundombinu tu.mbona Dar imewezekana kwanini Morogoro ishindikane?. Watu wanateseka wao wapo tu tena wanafanya biashara ya kuuza maji na malori yao.
 
Mlima lukobe wenyewe una maji ya kutosha sema morogoro sio kama sehemu nyingine watu walio kwenye nafasi ya kutoa maamuzi si wazawa,naomba mnielewe hata viongozi wa kuchaguliwa ngazi za kata wengi si wazawa wa pale tofauti na mikoa mingine kiasi ule uzalendo unakosekana.
Shida ya maji haina mzawa au asiye mzawa wote ni binadamu wanahitaji maji na pia wakaazi wa Lukobe,Kihonda, Mkundi wazawa ni kama hakuna wengi wanaojiita wazawa wako Kiegeya tena 0.01%

Back
Top Bottom