Kwanini Mkuu wa Mkoa anaambatana na mkuu wa Maaskari?

El nino jr

Member
Aug 7, 2014
66
24
Habari wanaJF,

Kwanini anapokuwepo Mkuu wa Mkoa au Wilaya utakuta kuna askari polisi kadhaa, askari magereza kadhaa na pia utakuta na mwanajeshi mmoja au wawili tena hao pia maskari wenye vyeo tu?

Sasa hapa huwa ndio nashindwa kuelewa.Mwenye kufahamu naomba anijuze.
 
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa / wilaya huwa inajumuisha wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani au wilayani ndo sababu panakuwepo mwanajeshi,askari magereza ,polisi,uhamiaji...
 
hbr wana jf,kuna kitu ningependa kufahamu jambo hili.kwann anapokuwepo mkuu wa mkoa au wilaya utakuta kuna askari polisi kadhaa askari magereza labda wawili na pia utakuta na mwanajeshi pia mmoja au wawili tena hao pia maskari
wenye vyeo tuu.sasa hapa huwa ndo nashindwa kuelewa.mwenye kufahamu naomba anijuze


Ndani ya Wilaya hao wote wapo chini yake na wana ofisi ofisini kwake.
 
hahahahahahahahhahahah....ndugu yangu weeeeee....nyamaza watakuja hapa kina Lizaboni watakutafuna...usiguse MIUNGU wao
 
Wanasiasa wanawasumbua wana ulinzi na usalama kwa mambo yasiyo na tija wakati mwingine...! Ila hawana jinsi inabidi waandamane nao tu! Hasa hawa wa Dar wapenda media ndio wanatusumbua sana na matamko yao yasiyo n kichwa wala miguu.....wakiwa mikoa ya pembeni wenzao wanafanya kimy kimya! Mwingine amevamia hospitali usiku kw kushtukiza kumbe alikuwa na waandishi wa habari wakichukua video!kama bongo movie hivi
 
Habari wanaJF,

Kwanini anapokuwepo Mkuu wa Mkoa au Wilaya utakuta kuna askari polisi kadhaa, askari magereza kadhaa na pia utakuta na mwanajeshi mmoja au wawili tena hao pia maskari wenye vyeo tu?

Sasa hapa huwa ndio nashindwa kuelewa.Mwenye kufahamu naomba anijuze.

Umeuliza swali zuri, sina ufahamu sana wa suala Zima...lakini ninachofahamu Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Mkuu wa Ilaya ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya...Nafahamu pia kuwa kila mkoa una ofisa wa Jeshi (JWTZ) ambaye ni mshauri wa mgambo wa mkoa...ila sina hakika kama ofisa huyu naye ni mjumbe wa Kamati ya ulinzi ya mkoa, ingawa akili na uzoefu wangu unanituma niamini kuwa ofisa huyu naye ni mjumbe wa kamati ya ulinzi ya mkoa...Utakuta pia kila ofisi ya mkoa kuna maafisa wa magereza na polisi kwa utaratibu, wanaohusika na mkoa huo vivyo hivyo na wilaya...sasa ni wazi tu kwamba maafisa hao wa vyombo vya dola ni wazi wanaweza wakaambatana na mkuu wa mkoa au wilaya...Jibu langu linaweza kuwa siyo sahihi sana lakini nadhani kwa kiwango Fulani naweza kuwa nimesaidia...Bila shaka wenyewe wanaweza wakaja hapa wakatupa jibu sahihi zaidi.
 
Mshauri wa Mgambo (mwanajeshi) ni mjumbe wa Kwmati ya Ulinzi ya Mkoa/Wilaya. Wajumbe wengine maaskari ni Afisa Usalama wa Taifa wa Mkoa/Wilaya, Mkuu wa gereza lililopo Wilayani/mkuu wa magereza wa mkoa na Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa/Wilaya. Hawa wote, Mkuu wa Mkoa/Wilaya anapokuwa na ziara lazima awe nao karibu. Kabla hajatoa maagizo yoyote lazima akubaliane na hawa askari kwanza.
 
Back
Top Bottom