Ila inakera sana. Bora mtu kutokuoa. Kama wewe hujaoa, mpe exam mkeo ya kuwazoea dada zako.
kwahiyo umethibitisha kwamba mawifi sio wakorofi ila mkeo ndio mkorofi sio?? je hatak kukaa nao kwenye nyumba moja ama hatak kushirikiana nao?? ama ana maneno ya uchonganish na umbea??Samahani kwa kutumia neno hilo la "mjinga". Ila nilimaanisha mke anayeendekeza ugomvi pasipo na sababu. Mazingira niliyochukulia ni yale yenye "all people are ignorant under a corporate veil" Kwamba hujawahi kujua kama wifi zako ni wakorofi, ila wewe unaanzisha kuwachukia tu wifi zako bila kuangalia mazingira yao.
Hapo naelewa concern
yako, ila mi nilichotaka kuongelea je pakiwa na wifi zako wadogo (form
one au hawajaanza shule) au wengine wapo wapo tu, na wao hawana ugomvi
(chukulia wale ambao hawajakulia mijini--yaani siyo wambea mbea). Je
chuki ya nini kwa watu ambao hawajakuchokoza?
Bold na Blue, hizo point nazikubali. Ila sasa kwa nini hata mwanamke ambaye ni msomi anashindwa kuelewa jinsi ya kuishi na watu ambao hawajaenda shule, tena ambao ni humble to the ground? Ila ulivyosema pande mbili ni kweli ila nadhani pia mke kama msaidizi wa mume she need to be bold and speak out of anywrong doing za wifi, wakati mwingine mke anaweza kausha, haswa wifi wanapoboronga anasubiria waharibu zaidi halafu anakuja kusema eti siku nyingi alikuwa anafanya hivyo, then unamuuliza why hukusema, anabaki kimya, je huyu utamuhesabu ni mke??Mkuu Kama alivyosema Kaunga hii kitu ni ya pande mbili. Na mara nyingi huanzishwa na dada wa kaka kwa kutaka mkeo aishi kutokana na matakwa yao wao. na wakati mwingine huanzishwa na Mkeo asipokuwa na uelewa wa kutosha kwa namna ya kuishi na jamii ya watu wengine tofauti na familia alioizoea.
Mkuu kwa habari ya hii mambo huwa ni ngumu sana kuamua au kusuluhisha usipojitahidi kuwa ''independent'' nikimaanisha usichue maneno ya upande mmoja na kuyafanyia kazi, jipe muda, chunguza na atakayekuwa ameenda kinyume na mwingine umuonye mbele ya wengine kwa HAKI, Kama ni dada zako unawakemea kwa haki na kama ni mkeo unamkemea kwa haki, hapo utaanza kujenga uhusiano na heshima kwa kila mmoja.
Mwisho jitahidi sana kuwa na msimamo wako kama Mwanaume na kama kichwa cha nyumba yako, '
Maneno ya hekima yanasema katika kitabu cha mwanzo kuwa ''Mtu mume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na Mkewe nao watakuwa mwili mmoja'' so kuna matatizo mengine inaweza pia kuwa wewe mwanaume ni chanzo pasipo kujua. ''nani alikuambia wanawake wanapendana kiasi hicho hata waishi pamoja kwa uelewano? ni wachache sana kaka wa namna hiyo''
Sasa hapo shida ni uwazi wa wanandoa. Nadhani kama hakuna dhamira ya kuwa wawazi kwa wanafamilia nalo ni tatizo.Tena hao ndio wabaya maana wanaendeshwa kwa remote! Ana shida anampigia mama yake mkoa,mama anampigia mumeo amsaidie mtoto wewe huna habari! Mwe!
Bold na Blue, hizo point nazikubali. Ila sasa kwa nini hata mwanamke ambaye ni msomi anashindwa kuelewa jinsi ya kuishi na watu ambao hawajaenda shule, tena ambao ni humble to the ground? Ila ulivyosema pande mbili ni kweli ila nadhani pia mke kama msaidizi wa mume she need to be bold and speak out of anywrong doing za wifi, wakati mwingine mke anaweza kausha, haswa wifi wanapoboronga anasubiria waharibu zaidi halafu anakuja kusema eti siku nyingi alikuwa anafanya hivyo, then unamuuliza why hukusema, anabaki kimya, je huyu utamuhesabu ni mke??
Wadau ni suala ambalo
mie limenisumbua kidogo. Kwa nini wake huwa hawaelewani na wifi zao? Je
ni ujinga wa wake? au? Yaani wakati mwingine unaweza kuta mke ni msomi
anashindwa kuelewana na wifi zake ambao either ni wadogo au wakubwa
hawajaenda shule, why? mwenye experience.
nashukuru Mungu mie na mawifi zangu tunapatana sana, hata mama mkwe pia tunaelewana.
Wanaume mnashindwa kuelewa nafasi yenu kwenye ndoa wewe ni kichwa unatakiwa kutawala kwa akili sio kwa upendeleo kama mkeo hapatani na dada yako oongea na mkeo kwa upendo nini unataka na atakuelewa ila ukitaka kujifanya unampotezea akikulalamikia ndo unawasha moto pili punguza kuongelea mabaya ya ndugu zako kwa mkeo hiyo inampa nafasi ya kuwachukia ndugu zakoneggirl, nimekuelewa. Ila sasa chanzo cha chuki ndiyo mi nashindwa kuelewa. Mimi kama mwanaume unaweza kukuta nawapenda sana wadogo za mke wangu, wawe wa kike au mkiume. Ila kwa wanawake hii inakuwa tabu. Mfano, kama mke akijua unawasaidia wadogo zako haswa wa kike roho inamuuma sana, tena anakuwa anaona eti hatuwezi wasaidia wote, anakuwa na ile roho mbaya ile mbaya ya kutu kabisa. Sasa mi kinachonitatiza, kwa nini wawe vile?