Kwanini mitandao ya mikopo yanakiuka makubaliano?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Nina hoja ya msingi kuhusu jinsi baadhi ya mitandao ya mikopo ya simu inavyokiuka makubaliano ya ulipaji. Kwa mfano ukikopa tarehe 15 mwezi huu, makubaliano yanaonyesha kwamba malipo yanapaswa kufanyika tarehe 21. Hata hivyo kabla ya tarehe hiyo kufika, tayari wateja wanaanza kupigiwa simu, kutumiwa ujumbe wa vitisho, na kukumbushwa kwa njia ya matusi na kejeli.

Swali langu ni,. Kama tumekubaliana tarehe ya mwisho ya kulipa ni tarehe 21, kwa nini wanachukua hatua kabla ya muda huo kufika? Hii ni kinyume na makubaliano ya kimkataba.

Ni kweli Watanzania wengi tunakumbwa na changamoto za kifedha na tunategemea mikopo hii kwa matumizi ya dharura lakini haimaanishi kwamba watoaji wa mikopo watunyanyase au kuvunja sheria na makubaliano waliyojiwekea wenyewe.

Naomba Serikali kupitia mamlaka husika kama TCRA, BOT au mamlaka ya kulinda watumiaji wa huduma za kifedha ifuatilie mwenendo huu wa kampuni zinazotoa mikopo kwa njia ya simu hasa zile zinazoenda kinyume na makubaliano ya ulipaji.

Ninaomba wanajamii wenye uzoefu kama huu wachangie labda maoni yetu yatafika huko juu.

Kiranga[/USER], DR Mambo Jambo,
 
Watanzania bana tuliumbiwa kulalamika sana yaani. We unaacha fursa inakupita unaishia kulalamika tu. Kama una uhakika muda bado, hujakiuka mkataba, wamekukashifu na kukutukana kwa maandishi ya meseji, ofisi zao unazijua, kopi ya mkataba unayo kwanini usiruke chap .mahakamani tu ukadai milioni 349 za kukashifiwa?

Ukidai 349m, mahakamani ikachezesha ikaamuru ulipwe 150m ukatoa hapo 30m za wakili una hasara gani kupata 120m for just kutukanwa tu ambako hata hakuumi kiviiile na hata watu hawajasikia kwanza
 
Sheikh hawanaga ofisi hao wakopeshaji. Hata ukiwaambia nielekezeni ofisi zenu nije niwalipe wanakataa kukuonesha wanakwambia lipa kwenye simu mumo humo.
 
Je, Na wewe walishawahi kukudai kabla ya mda wa makubaliano?
 
Walishawahi, mkopo wa siku 7 wanaanza kutuma meseji na kupiga simu siku ya 5.
Niliwalipa kidogo kwanza ila usumbufu ulivyozidi simu na jumbe kutoka namba tofauti nikasema siwalipi, mkitaka nionesheni ofisi nije niwalipe hapo hapo.
 
Hawakutuma ujumbe kwa baadhi ya jamaa zako?
 
Nina hoja ya msingi kuhusu jinsi baadhi ya mitandao ya mikopo ya simu inavyokiuka makubaliano ya ulipaji. Kwa mfano ukikopa tarehe 15 mwezi huu, makubaliano yanaonyesha kwamba malipo yanapaswa kufanyika tarehe 21. Hata hivyo kabla ya tarehe hiyo kufika, tayari wateja wanaanza kupigiwa simu, kutumiwa ujumbe wa vitisho, na kukumbushwa kwa njia ya matusi na kejeli.

Swali langu ni,. Kama tumekubaliana tarehe ya mwisho ya kulipa ni tarehe 21, kwa nini wanachukua hatua kabla ya muda huo kufika? Hii ni kinyume na makubaliano ya kimkataba.

Ni kweli Watanzania wengi tunakumbwa na changamoto za kifedha na tunategemea mikopo hii kwa matumizi ya dharura lakini haimaanishi kwamba watoaji wa mikopo watunyanyase au kuvunja sheria na makubaliano waliyojiwekea wenyewe.

Naomba Serikali kupitia mamlaka husika kama TCRA, BOT au mamlaka ya kulinda watumiaji wa huduma za kifedha ifuatilie mwenendo huu wa kampuni zinazotoa mikopo kwa njia ya simu hasa zile zinazoenda kinyume na makubaliano ya ulipaji.

Ninaomba wanajamii wenye uzoefu kama huu wachangie labda maoni yetu yatafika huko juu.

Kiranga[/USER], DR Mambo Jambo,
Kwani Bado Ipo Si nilisikia Ilifungiwa
 
Back
Top Bottom