Takwimu sahihi zinatakiwa, inawezekana ni kuwa ndiyo trend ya ripoti za habari Tanzania kuhusu vifo vya kutokana na mauaji kutokana na ukatili wa kijinsia, ushirikina, tamaa ya urithi, tamaa ya mali ndiyo vinabebwa na vyombo vya media na kufuatiliwa sana.
Pia teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA kupamba moto hivyo taarifa zaidi ambazo hazikuweza kuenea nchi nzima kwa kasi sasa ni rahisi habari hizo kufika maeneo ya mbali na kulipotokea tukio, tofauti labda zamani tukio likiishia habari zake maeneo ya jirani hivvyo kuokuwa habari ya kitaifa ikaishia kuwa habari za mtaa / kijiji ( local news).
Utashangaa kuwa ripoti sahihi za polisi takwimu za maeneo yanayoongoza kwa mauaji ni maeneo yasidhaniwa maana huko huonekana ni shamba na hakuna taarifa zake nyingi ktk media, blogs, vlogs, FB, X n.k :
1 Dec 2020 — Kitengo cha takwimu cha Jeshi la Polisi kinajukumu la kupokea taarifa na ripoti : mchanganuo wa makosa mbalimbali:
2.5.1 Mauaji na Sababu Zake
Makosa ya mauaji hutokana na sababu mbalimbali zikiwemo watu kujichukulia sheria mkononi na visasi. Idadi kubwa ya mauaji ilijitokeza kwenye matukio yaliyohusisha wizi wa kawaida, ujambazi, ugomvi majumbani, imani za kishirikina, wivu/ugoni, visasi na ugomvi vilabuni. Idadi ya matukio ya watu kuuawa ilijitokeza kwa wingi katika mikoa ya Kagera (163), Tabora (152), Dodoma (119), Kigoma (111) na Mwanza (103). (Jedwali Na. 2.13) .
2.2.1 Makosa Dhidi ya Binadamu
Kundi hili linahusisha makosa ya mauaji, kubaka, kulawiti, wizi wa watoto, kutupa watoto, kunajisi na
usafirishaji haramu wa binadamu. Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2020 jumla ya makosa
11,001 yaliripotiwa ikilinganishwa na makosa 12,223 kwa mwaka 2019. Huu ni upungufu wa makosa
1,222 sawa na asilimia 10.0. Makosa yenye ongezeko kubwa la idadi ni Kunajisi (23), Kutupa watoto
(5) na Usafirishaji haramu binadamu (1). Aidha, makosa yaliyopungua sana kiidadi ni Kubaka (574),
Mauaji (394) na Kulawiti (278) (Jedwali Na. 2.4).......
Source
www.nbs.go.tz/ kitengo cha takwimu jeshi la Polisi
MAKALA MAALUM:
Ezekiel Kamwaga
Mchambuzi
23 Februari 2021
Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Idara ya Taifa ya Takwimu (NBS), zilizotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, zinaonyesha kwamba kwa wastani, Watanzania tisa kati ya kila 1000 hufariki dunia kila mwaka hapa nchini.
Kama tutachukulia kwamba Tanzania ina watu milioni 60 sasa, maana yake mwaka huu ilikadiriwa watu 540,000 watapoteza maisha kwa sababu mbalimbali. Hizi ni takwimu rasmi za serikali.
Lakini, shirika la ujasusi la Marekani, linaeleza kwamba kiwango hicho cha vifo (crude death rate) kinafikia watu saba kwa kila watu 1,000. Kwa sababu hiyo, Tanzania wanakufa watu wachache kwa mwaka kulinganisha na marekani kwa sababu kwa wao, kiwango ni wastani wa watu nane kwa kila wananchi 1000.
Kuna uwiano usio sawa baina ya mkoa na mkoa au mijini na vijijini. Mkoa wa Njombe, kwa mfano, kiwango ni watu 13.5 kwa kila watu 1000. Kwa maana hiyo, kama Njombe ingekuwa ni nchi yenye idadi sawa na ya Tanzania, watu 810,000 wangekuwa wanakufa kila mwaka katika taifa hilo.
Walatini wana msemo maarufu; Mors certa, incerta vita. Kwa tafsiri ya Kiswahili maneno hayo yana maana " kifo ni lazima, kuishi ni bahati". Msemo huu mara nyingi humaanisha kwamba katika maisha ya binadamu, jambo la uhakika zaidi kuliko yote mengine ni kwamba kuna siku mwanadamu ataondoka duniani.
Hata hivyo, wakati vifo vinapotokea kwa watu wengi - maarufu na wasio maarufu na tena katika kipindi kifupi na kwa mfululizo, hilo haliwezi kuwa jambo la kawaida. Na wakati vifo hivyo vinapotokea katika wakati dunia inakumbana na tatizo lililotangazwa na shirika la afya duniani (WHO kuwa ni janga; maswali yanakuwa mengi zaidi.
Ndiyo hali inayoikumba nchi ya Tanzania kwa sasa.
Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja kuanzia Machi mwaka jana hadi Februari mwaka huu, kumekuwa na taarifa nyingi za vifo vya watu mashuhuri na wasio mashuhuri. Hata hivyo, vifo vya watu mashuhuri vimetikisa zaidi kwa sababu wengi wao maisha yao yanawagusa watu wengi. Wengine, maisha yao yanagusa nchi kabisa.
Hili ndilo jambo lililosababisha baadhi ya magazeti yanayochapwa kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kuandika taarifa zinazoeleza mshtuko uliopo baada ya vifo hivyo. Ni mshtuko kwa sababu kinachotokea sasa hakijawahi kuonekana katika historia ya nchi tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 60 iliyopita.
Source : BBC Swahili