Kwanini mapema hivi serikali ya awamu ya tano haya yanatokea?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kuna kitu najaribu kujiuliza hapa kutokana ambavyo mamilioni ya watanzania walikua na matarajio makubwa sana kwa serikali ya awamu ya tano! Binafsi sikutegenea kukutana na haya mapema namna hii, tulitegemea kua tutakutana na viwango vya hali ya juu vya watendaji wa serikali ya awamu hii tofauti na awamu zote zilizopita kwa maana ya kwamba kiongozi mkuu akiwa kama kiranja wa watendaji hao na mambo yataenda sawia kabisa na tukabadili the whole history of our nation.

Nisiwe na wingi wa maneno lakini katika haya naomba niseme tu na mwenzangu tujadili kwa kina kwa maslahi mapana ya taifa. Nitajikita zaidi kwa watendaji wa serikali hasa mawazrizi ambao ndio viongozi wa maamuzi ya mwisho katika kupanga mambo mengi na makubwa yahusuyo taifa kwa ujumla.

UTENDAJI WA MAWAZIRI

Ni juzi hapa tangu wateuliwe mawaziri na Mh Rais tumeshuhudia vituko vingi sana kwa mambo ya msingi yaliyohitaji utulivu mkubwa kwa maslahi ya taifa.

1.WIZARA YA AJIRA, KAZI, WALEMAVU NA VIJANA.

Tumeshuhudia tu juzi hapa waziri Jenista Muhagama akifanya uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF lakini baada ya masaa manne tu akatengeua utezi wake, Yaani hapa mtu unaweza kufikiri mpaka kichwa kinauma! Inamaana mtu unafanya tu uteuzi wa mtu kwa taasisi kubwa kama ile bila hata kua na taarifa kamili za utendaji wake na Uhalali wake katika nafasi ile kweli? Yaani kwakua mtu umependa Rangi,sura au ukaribu mlionao ndio ukaona anafaa kweli? Haya ni maajabu ya mwaka 2016!

Ambapo juzi juzi waziri mwenzake amelalamikiwa kumfukuza kazi mtu akiwa mezani bila hata kufanyia uchunguzi hata angalao wa masaa kadhaa ili afanye maamuzi lakini yeye kwa hisia zake pale pale anamwambia mtu acha kazi! Ni katiba ya bara lipi iliyotumika hapa? Kuna utaratibu wa kumwachisha mtu kazi ukiwa ni pamoja na kumwandikia barua na sio mezani.

Juu ya huyu mama Mh Rais kwa kuzingatia maamuzi aliyokwisha yafanya mpaka sasa apime kama viatu vya uwaziri vinamfaa.

2.NISHATI NA MADINI

Ni juzi tu Mh waziri mkuu wakati anajiandaa kwenda kufanya ziara ya ghafla kwenye mita za kupimia mafuta Bandarini lakini kufika akakuta kuna watumishi wametumiwa ujumbe kwa njia ya simu ili wajiandae kwa kuweka sawa mazingira, inasemekana kua huo ujumbe ulitumwa na moja wa mawaziri ndani ya wizara hiyo! Kwa maana hiyo hao watendaji walijiandaa kumdanganya waziri na umma kwa ujumla ili kuficha ukweli.

Kwakweli huyu waziri aliyetuma huo ujumbe naye alinwangusha sana Mh Rais naye anapaswa àjipime kwa nafsi yake kama ataweza kuendana na kasi ya Mh Rais.

3.WIZARA YA TAMISEMI
Udhaifu wa hapa hata Mtoto mdogo anaufahamu, haihitaji degree au cheti kuufahamu.

Inawezekana vipi mpaka leo miezi 4 hatuna Meya wa jiji la DSM? Jiji kubwa kuliko yote na kongwe nchini, na liko katika rank ya majiji maarufu na makongwe Afrika.Wziri yupo, maamuzi hakuna, tunataka kulipeleka taifa katika uchumi wa kati huku mambo madogo kama haya yanatushinda. Huyu waziri ni vipi ameshindwa kuliamua hili jambo jambo dogo kama hili ambalo liko wazi? Je makubwa atawaweza?

Naye anatakiwa ajitathmini kwa utendaji wake kama dhamana aliyonayo kwa umma inamtosha.

Kwakweli haya yasipoangaliwa kwa umakini tutashuhudia mambo mengi kabla hata ya kufika nusu ya awamu ya tano.
 
Kwa hilo la UMEYA wa DSM litakuwa na mkono wa wakubwa(wenye chama chao). Rejea jeuri ama matusi ya Masaburi kwa waheshimiwa madiwani wa Dar kuwa wanafikiri kwa kutumia kiungo "bandia"
 
Back
Top Bottom