Nadhani kwa namna yake Mungu anatupenda watanzania sana ukilinganisha na mataifa mengi duniani!
tukishindwa kushukuru kwa haya tuliyonayo sidhani kama hata makubwa kama Mlima Kilimanjaro tutaweza kushukuru!
kabla hatujamfikia Magufuli naomba tusafiri hatua kwa hatua tuone jinsi tulivyopewa Baraka, kwanini huyu naye pia ametoka kwa Allah/Bwana etc
Kambarage:
Huyu kiumbe aliishi miaka iliyotakiwa kuwe na umoja wa kitaifa, kati ya viongozi wote waliowahi kutawala nchi hii, huyu hakuwahi kuwa na kwao. huyu alihamia Magomeni kisha Magogoni na alipofika msasani akawa yupo nyumbani. kama angekuwa japo ana ubinafsi kidogo, taswira ya taifa hili isingekuwa hii ya leo! Huyu aliishi katika Dunia yenye matabaka Makubwa ya kibapari na kijamaa, lkn kitu hatari ilikuwa ni mafungamano ya kisiasa, ila kwa eledi wa kambarage na ujuaji wake wa siasa akatufanya tubaki kutofungamana na upande wowote.
Mungu alimchagua mtu ambaye hakuwa mkabila wala mdini! mtu anayeijua siasa mno na hiyo ilikuwa hazina kuu kwetu, wengi kati ya viongozi wenziwe wa mataifa jirani walijitajirisha na hawakufika mbali
Mwinyi:
Wakati dunia inapata muelekeo mpya wa kiuchumi na kidemokrasia, Mungu akamleta Mwinyi, issue za biashara huria na uhuru wa kisiasa (demokrasia) vikakutana na mtu asiye na vikwazo, mambo yaliyoleta mitafuruku katika nchi nyingi Africa, kwetu hayakukutana na ukinzani wowote, tuliambiwa rukhsa, kila kitu. hatukumwaga damu kama nchi nyingi katika kulazimisha serikali iridhie kubadili mfumo wa kisiasa! laity Mungu angemuacha Kambarage labda mtihani huu angefeli. Huu haukuwa wakati mgumu sana kisiasa kwa kuwa soviet walikuwa wanaanguka na Marekani alishaanza kutawala, so issues za siasa hazikuwa kubwa sana bali uchumi. Ila Mungu ni mwema, alimpumzisha Kambarage baada ya kumaliza kazi ya umoja wa kitaifa na kuruhusu Mwinyi atupitishe ktk mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.
Mkapa:
Aliingia wakati dunia iko moja, wote tunapelekwa na Marekani na washirika wake wa Magharibi, issue za utandawa na soko huria lililoshamili. Mkapa akaja kuendeleza uchumi huria aliouanzisha Mwinyi, kwa bahati na raisi wa Marekani Clinton na Bush ambao walikuwa strong nyakati hizo na kwa jeuri yao walikutana na raisi anayejua mengi, mwepesi kujieleza, anajiamini na anaweza kupanga mambo yake. huyu alifufua uchumi kwa weledi wa hali ya juu!
Kikwete:
huyu kwanza alitaka kuja wakati si wake Mungu akazuia, ila muda aliofika ulikuwa muafaka kwetu. Ni wakati ambapo Tanzania ilikuwa huru ku-trade na yeyote, na kwa mapenzi Yake Mungu, taifa kubwa la Marekani likapata pacha wake. watu waliohuru na wenye kupenda maendeleo ktk sekta zote, uchumi, biashara, michezo, elimu, siasa etc. wakati huo ulituendea vema maana mkuu wetu alikuwa ana-match na viongozi wengi duniani. shida kuu ya tawala hizi 2 za mkapa na Kikwete utegemezi wetu toka nje ulizidi kukua, kiasi kwamba hata chaguzi za marekani tulikuwa tukizifuatilia maana sera za raisi wao zinaathiri mustakabali wetu. ila huu ulikuwa ni wakati mzuri wa kujenga mahusiano na kuvuna kupitia miradi mbalimbali iliyoanzishwa duniani. Mungu alitupenda kwa mara nyingine, akatupatia raisi aliyefanana na mazingira ya dunia!
Now, Magufuli:
Huyu bwana hata njia alizopitia Mungu anajua, miaka 2 iliyopita, hakuwa hata na idea kuwa anaweza akarejea kuwa waziri (ubunge hakuwa na shida), ila hakuwa na ndoto za uraisi. Mungu amemleta tena kwetu kwa mara nyingine mtu anayefanana na wakati uliopo! Duniani kwa sasa ongezeko la viongozi wenye mkondo wa kulia, wanaojali utaifa wao na kukataa ushirikiano na mataifa mengine, maraisi wanaotumia msuli kusukuma agenda za kitaifa au za kimataifa. uzuri wa Magufuli alimtangulia raisi wa Marekani (Trump) hivyo sera zetu za nje, tayari zilishakuwa sio tegemezi, yale mambo miradi au shughuli zinazotegemea ufadhili wa wamarekani tulishaanza kuzikosa maana sheria ngumu kwa wafadhili/wahisani iliwafanya wengine wapunguze activities, wakimbie au waendelee bila ya kutupa masharti magumu. lakini huyu bwana pia amekuja kutunyoosha pale tulipokuwa tunazembea maeneo kama uzalishaji, uwajibikaji na ufisadi. katika dunia hii yenye kuongezwa ugumu na kina Trump kama tungekuwa tunafuja pesa na rasilimali kama zamani nadhani nchi ingeshasimama kutoa huduma
Mungu amerejea tena kwetu kwa mara ya Tano na Kutupa raisi anayefanana na ulimwengu. kama tusingekuwa na raisi wa aina ya Magufuli, nadhani leo nasi tungekuwa tunalia kuwa tutakosa msaada, A au B. Tuendelee kumshukuru Mungu ya yote.
Note: tumezungumzia yale makubwa na yaliyokuwa ya msingi ktk hizo tawala, wote watano wanamapungufu kadhaa lkn hayo hayakuwa sehemu ya uzi huu!
TUSIACHE KUSEMA MANENO HAYA KILA SIKU:
MUNGU IBARIKI TANZANIA (hii ni dua/maombi)
MUNGU IBARIKI AFRIKA (hii ni sadaka kwa wenzetu nasisi wenyewe)