Kwanini Lipumba anautaka tena uenyekiti wa CUF, alisahau nini?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,761
239,430
Kama chama cha CUF bado kinaamini katika umoja wa UKAWA , huyu ambaye aliyatelekeza makubaliano ya UKAWA ya kumsimamisha mgombea mmoja , katika kipindi muhimu kama kile , leo anataka kurudi ili iweje ?

Bila shaka ana lengo la kuvuruga kabisa UKAWA ndani na nje ya bunge , asipewe nafasi hiyo, ushahidi wa usaliti wa Lipumba ukiwemo ushahidi wa picha za Kigali , Rwanda alikoenda kula maisha baada ya kusaliti , umejaa hapa Jf. Maalim Seif , Juma Duni na Taslima mkiruhusu hili litokee dunia itawashangaa !

Ombi kwa Moderators msiunganishe uzi huu tafadhari .
 
swali la kujiuliza ni kwamba

JE ATAKUWA TAYARI KUFANYA KAZI NA MTU ALIYESABABISHA ASEME NAFSI IMEMSUTA HIVYO ANA STEP DOWN?
"siasa hazina adui wa milele" eti inasemakana ndiyo maana hata leo mhe.zitto anashirikiana na walewale waliomwita msaliti.............................ni muda tuu utaongea

pili,CUF ya sasa sioni atayeweza kuvaa viatu vya huyu jamaa,mchumi wa kimataifa,kwa cuf bado hajatokea sijui lakin hayo ni maono yangu.............
 
"siasa hazina adui wa milele" eti inasemakana ndiyo maana hata leo mhe.zitto anashirikiana na walewale waliomwita msaliti.............................ni muda tuu utaongea

pili,CUF ya sasa sioni atayeweza kuvaa viatu vya huyu jamaa,mchumi wa kimataifa,kwa cuf bado hajatokea sijui lakin hayo ni maono yangu.............
Alifanya nini kuimarisha CUFkatika uongozi wake ? Ikumbukwe pia kwamba upo ushahidi kwamba aliwahi kukiri msikitini kariakoo kumsaidia kikwete 2010 kwenye uchaguzi mkuu , wakati huo yeye akiwa mgombea wa CUF, ushahidi wa video upo hapahapa jf .
 
"siasa hazina adui wa milele" eti inasemakana ndiyo maana hata leo mhe.zitto anashirikiana na walewale waliomwita msaliti.............................ni muda tuu utaongea

pili,CUF ya sasa sioni atayeweza kuvaa viatu vya huyu jamaa,mchumi wa kimataifa,kwa cuf bado hajatokea sijui lakin hayo ni maono yangu.............
Kwenda kupiga porojo misikitini ati waislamu tujipange sawasawa ndio unamuona huyu Profesa Pumba zinamtosha!? Labda kama humjui vizuri mtu huyu.
 
Nani amekwambia Lipumba hana imani na UKAWA? Hujui kuwa Lipumba alikuwa mmoja wa waasisi wa UKAWA na Lowassa ndo kadandia gari barabarani? Au kipindikile ulikuwa mdogo sana?
 
Apewe nafasi nyingine endapo akitubu na kukubali kwenda na mfumo.
Siasa tamu jamani ikishaingia kwenye damu ukikaa pembeni kidogo.
Nisawa na mamba kutoka kwenye maji lazima atarudi tu.
 
Alifanya nini kuimarisha cuf katika uongozi wake ? Ikumbukwe pia kwamba upo ushahidi kwamba aliwahi kukiri msikitini kariakoo kumsaidia kikwete 2010 kwenye uchaguzi mkuu , wakati huo yeye akiwa mgombea wa cuf , ushahidi wa video upo hapahapa jf .
Aliwahi kuja korogwe manundu uwanja Wa shule ya mazoezi alisika akiwaambia wananchi wasimpe mgombea yeyote zaidi ya Kikwete km watashindwa kumpa yeye kura
 
CUF tangu kuondoka Lipumba upande huu wa Mainland imepwaya sana. Na yeye hakuacha chama watu wali react tu .alikua na msimamo anao uamini kuhusu lowasa. Hakupenda kula matapishi yake , hio iko wazi na CUF walimuelewa ndio maana hata wao hawakumsema kabisa...
Nadhani anafaa kama mwenye kiti kukiongoza chama lakini asiwe na ndoto za urais, hapa kidogo hana mvuto ...na ushawishi. Yeye ndie mwanzilishi wa ukawa pale alipo liongoza kundi la wabunge wa upinzani kutoka bunge la katiba..ni yeye alipo maliza hotuba na kusema tunatoka wote wakatoka na ndio mwanzo wa kuasisiwa kwa ukawa ambao umeleta faida kubwa katika siasa za upinzani Tanzania.

Cha kufanya sasa hivi hawa UKAWAa wache siasa za bungeni..wakae wafanye Tathmini ya kisayansi wapi walikosea. Watafute political consultant afanye utafiti huu kwa kupita nchi nzima na kujua wapi walishinda, wapi walishindwa, sababu gani wanapendwa zaidi na Mijini kuliko vijijini.
Wakae waangalie namna ya kushawishi watanzania kujiunga katika mabadiliko na kutafuta vijana makini waje kugombes ubunge...
Lazima baada ya uchaguzi chama chochote kijithamini...na waanze sasa kuanza kusaka wagombes wa urais.....watafute watu makini hata kama kuwatoa ndani ya CCM ....wakipanga sawa sawa bila ya ubinafsi mbona CCM nyepesi tu
 
kwa wale mnaohisi Mhe.Lipumba hakufanya lolote ndani ya CUF zaidi ya kuisadia CCM,je ni nani aliyejenga chama mpaka kufika hapo kilipo??
na kama hafai mhe.lipumba anayestahili kwa sasa kuchukua uongozi ni nani kwa maoni yenu na kwanini??
 
Sasa kwann uwaite wenzio nyumbu? Hiyo inadhihirisha una malezi mabovu na kichwan kwako uko mweupe, ban ni halali yako
Upstairs im well up equipped with high understanding and thinking ability/capacity..... Kuna siku ulifukuliwa Uzi mmoja hivi wa Lowasa, kuna jamaa walikuwa wakimtusi na sasa wamebadili msimamo bila any critical reason.....wanastahili kuitwa "nyumbu"
 
kwa wale mnaohisi mhe.lipumba hakufanya lolote ndani ya CUF zaidi ya kuisadia CCM,je ni nani aliyejenga chama mpaka kufika hapo kilipo??
na kama hafai mhe.lipumba anayestahili kwa sasa kuchukua uongozi ni nani kwa maoni yenu na kwanini??
Aendelee Twaha Taslima aliyehakikisha CUF inarudi tena juu kwa kulamba viti vingi vya ubunge oct 25.
 
Back
Top Bottom