Viongozi wa CUF, wanachama na wapenda mabadiliko nchini mpuuzeni Prof. Lipumba na genge lake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMM A NA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe 25 June, 2017

VIONGOZI WA CUF, WANACHAMA NA WANAPENDA MABADILIKO NCHINI MPUUZENI KIBARAKA LIPUMBA NA GENGE LAKE.

Tumepokea taarifa za kusajiliwa kwa BODI FEKI ya Lipumba na genge lake na baadae jana tarehe 24/6/2017 tumemsikia Lipumba akidai eti anataka kumuhoji Katibu Mkuu, Maalim Seif, Mhe Nassor Mazrui (Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar) na viongozi wengine waliowataja na anayoiita Kamati yake ya Maadili na Nidhamu.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF –CHAMA CHA WANANCHI) Tunapenda kuwajulisha Wanachama na viongozi wetu wote wa Chama,-Wabunge, Madiwani, Viongozi wa Halmashauri zote, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji nchini, Wapenda mabadiliko na watanzania kwa ujumla kuwa Chama cha Wananchi CUF kupitia vikao halali vya Chama vilishafanya maamuzi juu ya Lipumba na wenzake. Kibaraka Lipumba si Mwenyekiti wa CUF. Anachofanya ni muendelezo wa kuhakikisha kuwa dhamira yake ya kujaribu kutaka kukivuruga Chama na kuzuia haki na maamuzi ya Wazanzibar ya Oktoba 25, 2015 isipatikane ili kuwafurahisha wanaomtumia. CUF NA Viongozi wake wamejipanga vyema kukabiliana na Usaliti huo tunapenda kuwajulisha rasmi wanachama wetu kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayekwenda kuhojiwa na Kibaraka Lipumba na genge la lake.

Tunawapongeza wanachama NA Viongozi wote kwa utulivu NA subra mnayoionyesha katika kipindi hiki wakati Viongozi wenu wakibeba jukumu adhiimu la kulishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa huku ikitambua adui yetu.

Tunawahakikishia kuwa dhamira ya Kibaraka Lipumba NA genge lake kutaka kuvuruga mapambano ya kujenga misingi imara ya demokrasia nchini, utawala wa sheria na haki za binaadamu kwa nguvu ya pamoja chini ya UKAWA kamwe haitafanikiwa. Muda si mrefu haki itapatikana na ushindi kwa Taasisi ni suala lisilo na shaka yeyote juu ya njama na mipango yao dhidi ya CUF na viongozi wake.

HAKI SAWA KWA WOTE

-------------------------------------
SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA, CUF-TAIFA

MAWASILIANO: 0777414112
 
Salim Bimani katoka Nje Mchana wa Jua kali huku kafumba Macho na kusema Haoni Jua!
Ni Kweli Haoni Jua kwa kuwa kafumba Macho Ila hiyo kutoona Jua haimaanishi Jua Hakuna !

Kwa heri ni ya kuonana Vibaraka wa Seif Sharif Msaliti halisi wa Serikal tatu January 1984 kule Dodoma chini ya Comrade Aboud Jumbe Mwinyi!
 
Hii taarifa mbona ni ya kitoto sana!!? CUF ya maalim seif jibuni hoja ya Lipumba,ipi bodi iliyosajiliwa na Rita,ni hii ya kwenu au ya Lipumba!!? Km lipumba kapata anzisheni chama kingine,hiki kimeshakufa!!
 
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMM A NA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe 25 June, 2017

VIONGOZI WA CUF, WANACHAMA NA WANAPENDA MABADILIKO NCHINI MPUUZENI KIBARAKA LIPUMBA NA GENGE LAKE.

Tumepokea taarifa za kusajiliwa kwa BODI FEKI ya Lipumba na genge lake na baadae jana tarehe 24/6/2017 tumemsikia Lipumba akidai eti anataka kumuhoji Katibu Mkuu, Maalim Seif, Mhe Nassor Mazrui (Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar) na viongozi wengine waliowataja na anayoiita Kamati yake ya Maadili na Nidhamu.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF –CHAMA CHA WANANCHI) Tunapenda kuwajulisha Wanachama na viongozi wetu wote wa Chama,-Wabunge, Madiwani, Viongozi wa Halmashauri zote, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji nchini, Wapenda mabadiliko na watanzania kwa ujumla kuwa Chama cha Wananchi CUF kupitia vikao halali vya Chama vilishafanya maamuzi juu ya Lipumba na wenzake. Kibaraka Lipumba si Mwenyekiti wa CUF. Anachofanya ni muendelezo wa kuhakikisha kuwa dhamira yake ya kujaribu kutaka kukivuruga Chama na kuzuia haki na maamuzi ya Wazanzibar ya Oktoba 25, 2015 isipatikane ili kuwafurahisha wanaomtumia. CUF NA Viongozi wake wamejipanga vyema kukabiliana na Usaliti huo tunapenda kuwajulisha rasmi wanachama wetu kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayekwenda kuhojiwa na Kibaraka Lipumba na genge la lake.

Tunawapongeza wanachama NA Viongozi wote kwa utulivu NA subra mnayoionyesha katika kipindi hiki wakati Viongozi wenu wakibeba jukumu adhiimu la kulishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa huku ikitambua adui yetu.

Tunawahakikishia kuwa dhamira ya Kibaraka Lipumba NA genge lake kutaka kuvuruga mapambano ya kujenga misingi imara ya demokrasia nchini, utawala wa sheria na haki za binaadamu kwa nguvu ya pamoja chini ya UKAWA kamwe haitafanikiwa. Muda si mrefu haki itapatikana na ushindi kwa Taasisi ni suala lisilo na shaka yeyote juu ya njama na mipango yao dhidi ya CUF na viongozi wake.

HAKI SAWA KWA WOTE

-------------------------------------
SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA, CUF-TAIFA

MAWASILIANO: 0777414112

Du huku kwetu kitaa kuna tabia ya kusimama juu ya kimlima na kuanza kushusha matusi kwa mtu unayemuogopa kwa sababu ya hofu, kwani ukiwa jirani anaweza kukutembezewa kichapo na kwa desturi mambo haya hufanywa na watu wachonganishi (wambeya) wasio na hoja na wasio na nguvu, walichojaliwa watu hawa ni mdomo, huwa wanamudu sana kuongea na haswa matusi.
 
Lipumba ana shabihana na jina lake, ni mzee asiye kuwa na hata chembe ya aibu, heshima yake imeshuka sana kwa kuendekeza njaa.
 
Hii taarifa mbona ni ya kitoto sana!!? CUF ya maalim seif jibuni hoja ya Lipumba,ipi bodi iliyosajiliwa na Rita,ni hii ya kwenu au ya Lipumba!!? Km lipumba kapata anzisheni chama kingine,hiki kimeshakufa!!
Hivi uliwahi kuona Marehemu akigombea urithi ? Lipumba alifukuzwa Cuf na vikao halali vya chama mithili ya paka aliyekunywa maziwa ya mtoto , analindwa na Mutungi kwa maelekezo maalum , lakini ya kiwango cha chini sana .
 
Ya Bimani ni sawa na ya Sefu kuwaambia manyumbu subirini napewa urais wiki hii,mpaka leo hakuna dalili yoyote
 
Hii taarifa mbona ni ya kitoto sana!!? CUF ya maalim seif jibuni hoja ya Lipumba,ipi bodi iliyosajiliwa na Rita,ni hii ya kwenu au ya Lipumba!!? Km lipumba kapata anzisheni chama kingine,hiki kimeshakufa!!
Wako CCM wanaolazimisha kusubiri meli Dodoma! Kimbunga kijacho hakitaiacha CCM na ngoma yake wala huyo Polopesa anayebebwa!! CUF yake ambayo analazimishwa kupewa nina hakika haitopata kiti cha ubunge hata kimoja! Tuombe uzima ni suala la muda tu.
 
Matahira tu ndiyo watakao muunga mkono lipumba na vibaraka wake, ccm inacheza mchezo wa kitoto sana
Inawezekanaje mtu aliye telekeza chama kwa kujihuzulu akarudi toka uganda aliko kimbilia na kuanza kufanya kazi ya usaliti hivi?
 
Back
Top Bottom