Kwanini Kikwete kamteua Lawrence Mafuru kuwa Msajili wa Hazina?

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
Kwanini Kikwete kamteua Lawrence Mafuru kuwa Msajili wa Hazina? Penye moshi???

stay tuned


B4uqTWmCAAAAfd7.jpg:large

======================================

UPDATES


RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (PDB). Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wakati huohuo, Taarifa ya Balozi Sefue inasema Rais Kikwete amemteua Bibi Beng'i Mazana Issa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bibi Mazana Issa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Dominic M. Kambarage kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kipya cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Kambarage alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Taarifa ya Balozi Ombeni Sefue imesema kufuatia kuanzishwa kwa Chuo hicho kingine cha Umma, Rais Kikwete pia amemteua Profesa Lesakit S. Mellau kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa Taaluma kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014, na kabla ya uteuzi wake, Profesa Mellau pia alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.

Aidha Taarifa ya Balozi Sefue imesema Rais Kikwete amemteua Profesa Msafiri M. Jackson kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Utawala) kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Profesa Jackson alikuwa Mratibu wa Masomo ya Taaluma za Shahada za Juu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.

Vilevile katika Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Desemba,2014

 
Huyu rahis naye amezidi, mwishowe atateua mpaka watendaji Wa kata, bora muda wake uishe!!
 
Huyu jamaa alikuwa Nbc akaboronga,akapelekwa PDB/BRN nako hapakukaa vzr na kuhamishiwa fbme. Kwa ufupi huyu jamaa huwa ni mtekelezaji wa mafisadi. Ni mpiga dili kama walivyo wengine. Kwa muda mfupi aliokaa fbme ni balaaa,ni ufisadi mtupu.
Ingawa huyu jamaa ana mazuri yake akiamua kufanya kazi ni mzuri kikazi asipotumiwa kwa ufisadi
 
Riziwani Kikwete alimuharibia kazi Mafuru kule NBC kwa kulazimisha mikopo ya kipuuzi na benki inazama, but is a competent learned brother. Kabila yake Sospeter Muhongo
 
Huyu rahis naye amezidi, mwishowe atateua mpaka watendaji Wa kata, bora muda wake uishe!!

Mm pia naona kama its too much and too far jamani. Eti anateua mpk mkuu wa utawala wa chuo, mkuu wa taaluma wa chuo hili jipya kwangu. So atawaapisha pia au akiteua basi wanaingia mzigoni? Hizi mbona ni nafasi za kiueledi kwanini Utumishi wasizihandle hizo positions?

On the other hand, ni nani aliwaambia ili tuendelee tunahitaji utitiri wa vyuo vikuu? Kwanini utendaji na maamuzi yetu ni kama vile tunaishi Us so hatujui tatizo hasa la mkwamo wetu ni nini?

Mafuru naye kwa upande wake aliifanyia nini ccm alipokuwa nbc? Naona kama ni lazima abebwe tu kwa gharama yeyote ile, ikifail mbeleko moja anaandaliwa nyingine fasta fasta. Anyway time will tell kwani hakunaga linalofichika forever duniani humu.
 
Kaa karibu na mpishi uwe waonjweshwa japo mchuzi kujua kama munyu umekoa...
 
Kwa historian ya uadilifu hana NBC ametoka kwa kashifa name nimsingi alitakiwa apelekwe mahakamani,najua kuna wakubwa walimkingia kifua. Fbme nako ni benki miongoni zilizotuhumiwa zilizotakatisha pesa .na kipindi zikilalamikiwa sana alikuwa yuko pale.lakini bot ilikaa kimya Kumlinda.salsa usalama wa taifa haya hawayakuyachunguza mpaka wanampeleka jina lake kwa JK?au JK mwenyewe kaamua kumfadhili Vila kujali udhaifu wake?
 
Kuna Mkuu wa mkoa mmoja kutoka kanda ya ziwa(Name withheld) alihamishwa kienyeji juzi juzi nae Moshi mweupe unanukia.
Tukipata vijimemo mapema tutavipost.
 
Mbona JK anaangaika sana na mafuru,au alishiriki kumuaribia kazi Ikulu sasa analazimisha kumpoza.

Mafuru aliondoka nbc kwa kashfa ya ukopeshaji magari makubwa ya mazigo.

Na Ridhiwan hutajwa kuwa transporter.
Pia alikuwa anafadhili miradi ya WAMA kwa idhinisha fedha zilizokuwa zinatengwa kwa ajili ya shughuli zingine za kibank!! ni tetesi tu lakini.
 
Tatizo watu mlio wengi hamjui Mafuru..kwanza Mafuru hajatoka kwa kashfa Nbc ..kwani uchunguzi huru ulifanywa na tena na wachunguzi kutoka ABSa na Barclays ambao ndiyo wamiliki wakubwa wa Nbc na wakaridhika na kumrudisha kazi na kwa Sababu aliona kuna wapuuzi wamepanga kumharibia kazi akasepa...kuhusu BRN ipo vizuri kuliko unavyofikiri mtafute ceo wake akupe habari kamili Fbme Mafuru hakuwahi kufanya kazi pale hata siku moja alipelekwa pale sio na Kikwete Bali BOT nenda pale uone bank ilivyoo kaa vizuri sass na hajakaa azidi ya siku 160 .
Muuache Mafuru apige mzigo
Yupo fit
 
Kuna Mkuu wa mkoa mmoja kutoka kanda ya ziwa(Name withheld) alihamishwa kienyeji juzi juzi nae Moshi mweupe unanukia.
Tukipata vijimemo mapema tutavipost.


Unamuongelea Kanali aka Mulukozi. Yeye atakuwa waziri wa Maliasili na Utalii
 
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi, Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na Mashauri.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa Naibu Mkuu TEWW.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Desemba,2014


Hivi Mahakama kuu kuna Mahakimu?
 
Back
Top Bottom